Utangulizi Vitunguu ni zao muhimu sana hapa Tanzania. Mikoa ya Arusha, Manyara, Iringa, Mbeya, Tanga, Singida na Kilimanjaro ni maarufu sana kwa kilimo cha vitunguu na ni zao la chakula na biashara kwa mkulima mdogo. Uzalishaji wa vitunguu bado ni mdogo (tani nne kwa hekta) na upotevu wa mazao baada ya kuvuna ni mkubwa (50 %– 80%) kutokana na hifadhi duni hivyo wakulima wanahitaji utaalamu wa kilimo bora na hifadhi ya vitunguu ili kuongeza uzalishaji na kipato. Uzalishaji wa vitunguu Zao la vitunguu linazalishwa kutokana na mbegu na miche inakuzwa kwenye kitalu kabla ya kupandikizawa shamban. Miche inakuwa na kuzaa vitunguu.Vitunguu vikikomaa, vinavunwa na kuhifadhiwa vikiwa katika hali ya kulala bwete. Katika hali hii vitunguu vinaweza kuhifadhiwa kwa muda mrefu aitha kwa ajili ya kuzalisha mbegu msimu unaofuata au kuuza. Wingi na ubora wa zao la vitunguu hutegemea; hali ya hewa, aina ya vitunguu, upatikanaji wa mbegu bora, kilimo bora, uangalifu wakati wa kuvuna, usafirishaji na hif