Skip to main content

Posts

Showing posts with the label Shamba la Minazi

Upandaji wa Miche ya Minazi

UPANDAJI BORA WA MICHE Ili kupata mnazi ulio bora mkulima ni lazima awe muangalifu wakati wa kupanda. Mche uliopandwa vibaya huchelewa kukua na hata wakati mwingine hufa. Mazingira kama vile aina ya udongo, kiasi cha mvua, joto, na mwinuko lazima yaangaliwe kwa makini kabla ya kupanda. MAZINGIRA YANAYOFAA KULIMA MINAZI Sehemu zinazofaa kulima zao la minazi lazima ziwe na mvua ya kutosha au ziwe na mabonde yenye unyevu ardhini. Kwa kifupi mvua isipungue milimita 1000 hadi 2000 kwa mwaka na kiangazi kisichozidi miezi mitatu. Sehemu hiyo vilevile iwe na joto la kutosha (23 hadi 30 nyuzi joto) na mwinuko kutoka usawa wa bahari usiozidi mita 600. Minazi inapendelea mwangaza wajua, kwa hivyo isipandwe chini ya miti kama vile miembe au mikorosho. UCHAGUZI WA ARDHI Ni vyema kufanya uchaguzi wa ardhLinayofaa kwa minazi kabla ya kupanda. ARDHI ISIYOFAA KUPANDA MINAZI Haifai kupanda minazi kwenye ardhi yenye mawe, miamba, jasi na maji yaliyotuama. Sehemu hizi hazifai kwa sababu mizizi ya minazi i...