Skip to main content

Posts

Showing posts with the label Tiba za Asili

Tiba Asili Ya Magonjwa Ya Mifugo

UTANGULIZI Tiba asili kwa karne ya sasa imeonekana kuwa tiba mbadala ya dawa za hospitalini kwa sababu ya madhara yake kuwa madogo kwenye mwili mara baada ya kuyatumia. Madawa haya ya asili yamekuwa yakitumiwa na binadamu tangu enzi hata kabla ya madawa ya kikemikali kuvumbuliwa na mwanadamu. Lakini kasi ya madawa ya kikemikali yalishika kasi kwa sababu ya uharaka wake wa kutibu magonjwa kwa muda mfupi tena kiasi kidogo sana kikitumika. Tatizo la madawa ya asili ilikuwa kutokuwa na uhakika wa dosi na wakati mwingine mgonjwa alihitaji kunywa dawa nyingi sana pasipo mafanikio. Hata hivyo siku za hivi karibuni binadamu ameona ni vema kurejelea dawa za asili huku akifanya maboresho kwa kujua kiasi halisi cha dozi ya dawa. Dawa nyingine zimeboreshwa zaidi na kufanya kiasi kidogo cha dozi kutumika kama dawa za kikemikali tofauti ni madhara machache ya dawa za asili. Dawa za asili zinahitaji uvumilivu kiasi kwani zinachukua muda ili kufanya kazi huku zikiacha mdhara machache. Dawa hizi zimeku...