Utangulizi Kitalu ni sehemu maalumu iliyopangiliwa kwa ajili ya kutunzia miche michanga kabla ya kuipeleka shambani ama bustanini. Sio mimea yote inahitaji vitalu ila mimea mingi inahitaji vitalu. Mimea kama mahindi, maharage, karoti, kunde na mchicha haihitaji vitalu. Mimea kama kabeji, vitunguu, sukuma wiki, chainizi, nyanya, bilinganya, hoho, matikiti, matango na mengineyo huhitaji kitalu. Pia miti mingi ya matunda, kuhifadhi mazingira, mbao, dawa nakadhalika huhitaji kitalu. Mimea ambayo inasumbua kupandikiza na ambayo inachipua haraka inashauriwa kupandwa moja kwa moja shambani ambapo haitasumbuliwa kuhamishwa. Mimea ambayo inachelewa kuchipua, kukua, na yenye kuhitaji matunzo au kuhudumiwa kwa karibu wakati ikiwa michanga inashauriwa ipandwe kwanza kwenye kitalu hadi itakapopata miche inayotakiwa kisha kupandikizwa bustanini au shambani. Aina za vitalu Vitalu vya kawaida vya matuta Vitalu vya vimfuko (viriba) Vitalu vya boksi Namna ya kuchanganya na upandaji Weka udongo debe...