UTANGULIZI Bilinganya imo katika jamii ya mimea inayohusisha nyanya, pilipili, viazi mviringo na nyanya mshumaa. Mboga hii ina viinilishe muhimu kama vile madini aina ya chokaa na chuma, vitamini A, B na C, wanga, protni na maji. Mboga hii hutumika kutengeneza supu au kama kiungo katika vyakula mbalimbali. Vile vite huweza kuhifadhiwa kwa kukatakata vipande na kuwekwa kwenye makopo. Zao hili huhitaji hali yajoto la wastani, udongo wenye kina kirefu na rutuba ya kutosha na usiotuamisha maji. Kwa kawaida bilinganya hulimwa zaidi ya msimu mmoja, lakini katika nchi za Kitropild (joto) zao hili hulimwa kwa msimu mmoja. AINA Aina za bilinganya zinazolimwa kwa wingi katika nchi za ukanda wajoto ni kama zifuatazo:- Black Beauty Aina hii huzaa sana, matunda yake meusi, makubwa, na ya mviringo. Florida Market Matunda ya Florida Market yana umbo la yai. Aina hii pia huzaa sana, lakini hushambuliwa kwa urahisi na ugonjwa wa mnyauko bakiteria (Bacterial wilt). Florida High Bush: Matunda yake ni mak...