Skip to main content

Posts

Showing posts with the label kilimo cha Miti

Namna ya Kuandaa Kitalu cha Miche

Utangulizi Kitalu ni sehemu maalumu iliyopangiliwa kwa ajili ya kutunzia miche michanga kabla ya kuipeleka shambani ama bustanini. Sio mimea yote inahitaji vitalu ila mimea mingi inahitaji vitalu. Mimea kama mahindi, maharage, karoti, kunde na mchicha haihitaji vitalu. Mimea kama kabeji, vitunguu, sukuma wiki, chainizi, nyanya, bilinganya, hoho, matikiti, matango na mengineyo huhitaji kitalu. Pia miti mingi ya matunda, kuhifadhi mazingira, mbao, dawa nakadhalika huhitaji kitalu. Mimea ambayo inasumbua kupandikiza na ambayo inachipua haraka inashauriwa kupandwa moja kwa moja shambani ambapo haitasumbuliwa kuhamishwa. Mimea ambayo inachelewa kuchipua, kukua, na yenye kuhitaji matunzo au kuhudumiwa kwa karibu wakati ikiwa michanga inashauriwa ipandwe kwanza kwenye kitalu hadi itakapopata miche inayotakiwa kisha kupandikizwa bustanini au shambani. Aina za vitalu Vitalu vya kawaida vya matuta  Vitalu vya vimfuko (viriba) Vitalu vya boksi Namna ya kuchanganya na upandaji Weka udongo debe...

Upandaji wa Miche ya Minazi

UPANDAJI BORA WA MICHE Ili kupata mnazi ulio bora mkulima ni lazima awe muangalifu wakati wa kupanda. Mche uliopandwa vibaya huchelewa kukua na hata wakati mwingine hufa. Mazingira kama vile aina ya udongo, kiasi cha mvua, joto, na mwinuko lazima yaangaliwe kwa makini kabla ya kupanda. MAZINGIRA YANAYOFAA KULIMA MINAZI Sehemu zinazofaa kulima zao la minazi lazima ziwe na mvua ya kutosha au ziwe na mabonde yenye unyevu ardhini. Kwa kifupi mvua isipungue milimita 1000 hadi 2000 kwa mwaka na kiangazi kisichozidi miezi mitatu. Sehemu hiyo vilevile iwe na joto la kutosha (23 hadi 30 nyuzi joto) na mwinuko kutoka usawa wa bahari usiozidi mita 600. Minazi inapendelea mwangaza wajua, kwa hivyo isipandwe chini ya miti kama vile miembe au mikorosho. UCHAGUZI WA ARDHI Ni vyema kufanya uchaguzi wa ardhLinayofaa kwa minazi kabla ya kupanda. ARDHI ISIYOFAA KUPANDA MINAZI Haifai kupanda minazi kwenye ardhi yenye mawe, miamba, jasi na maji yaliyotuama. Sehemu hizi hazifai kwa sababu mizizi ya minazi i...

Kalenda Kilimo cha Minazi

KALENDA YA KILIMO CHA MINAZI Ili kuongeza ufanisi katika kilimo cha aina yoyote, shughuli zote lazima zifanyik kitaalamu na kwa wakati unaotakiwa. Kwa hivyo wakulima, mabwana shambe viongozi, makampuni yanayoshughulikia kilimo na taasisi inabidi waelewe shughu muhimu za zao la minazi kwa mwaka mzima. Katika kilimo cha minazi shughuli kama vile kutayarisha shamba, kupanda, kupali lia, kutandaza nyasi kavu kwenyejalbe n.k. huwa zina misimu maalumu. misimu hi hutofautiana kutoka sehemu hadi sehemu na mkoa hadi mkoa. Kalenda za kilimo hik zimegawanywa katika sehemu mbili. Kwa mfano mikoa ya Morogoro. Lindi n Mtwara imewekwa katika kundi moja, wakati Tanga, Pwani, Dar es Salaam n Zanzibar iko katika kundijingine. Hii inatokana na ukweli kwamba kila sehemu in wakati maalum wa mvua na kiangazi. Kalenda zilizoambatanisha zitatoa mangaz wakati gani kazi ipi ifanyike na ipi ifuate. Mabwana shamba wanashauriwa kufuat kalenda inayohusika kwa sehemu zao. KALENDA YA KILIMO BORA CHA MINAZI MIKOAYA DA...

Kilimo cha Miti ya Mbao - Uwekezaji wa Muda wa Kati na Mrefu

Utangulizi Kilimo cha miti ni uwekezaji wa muda wa kati na mrefu (mid & long term investments). Ila kwa kawaida jamii nyingi hasa za kiafrika huwa hazivutiwi na uwekezaji wa muda mrefu. Hata hivyo kama una mpango wa kuwa imara kiuchumi inashauriwaau yakupasa kufikiria na kujifunza aina za uwekezaji wa muda mrefu. Miti hutumika kwa matumizi mengi mfano mbao, nguzo za umeme na kujengea, mapambo, kuni na mkaa, kuzalisha matunda, mitishamba na madawa,  utengenezeaji wa karatasi n.k.  Mchanganuo Ekari moja ya shamba unaweza kupanda miti mia sita (500) mpaka mia saba (700). Gharama za kununua mashamba au maeneo ya kupandia miti hutegemea na eneo. Kwa  sehemu nyingi za vijijini maeneo kwa ekari moja hayazidi laki 5.  Miche ya kununua mfano Mitiki huuzwa kuanzia elfu moja (1000) kwa mche mmoja Gharama ya kununua miche =  1000 * 600 = 600,000   Pia unaweza kuokoa gharama za kununua miche kwa kuioteshe mwenyewe ktk vitalu na kuiamishia shambani baada ya kustawi v...