Skip to main content

Posts

Showing posts with the label Kuku wa Kienyeji

Ufugaji Bora wa Kuku wa Kienyeji

UTANGULIZI Unaweza kuanza kwa mtaji wa Mil.1 mpaka laki tano au hata chini ya hapo. Mfano. Unaweza kutumia Tsh 250,000 kununua kuku 25 kwa bei ya Tsh 10,000 kwa kuku mmoja (kadirio la juu) Majogoo watakuwa 5 kwa uwiano wa 1:4 . Hii ina maana kuwa wakishaanza kutaga utakuwa na vifaranga 20 x 10 = 200 Watunze vizuri. Wale vifaranga tunakadiria kuwa makoo(majike) watakuwa 150 ambao ndani ya miezi 3 au zaidi nao wataanza kutaga. Utakuwa na kuku 200 + 25 =225 ndani ya miezi 6. Miezi 6 inayofuata 225 - (majogoo 55) = 170 Hii ina maana kuwa 170 x 10= 1,700. Ndugu mwanajamvi hayo niliyotoa ni makadirio ya chini sana hivyo mpaka mwisho wa mwaka utakuwa na kuku zaidi ya 2000. Mwaka utakaofuata utakuwa na kuku wangapi baada ya kuuza kuku 1,000. Mwaka 2. 750(majike) x 10 = 7500 (uza wengine) 3000 x 10 = 30,000. Kutegemea na uwezo wako mpaka mwisho wa mwaka wa pili utakuwa umefanikiwa sana. Kumbuka huu ni mwongozo tu, fanya utafiti na ufuatilie zaidi huku ukiacha kando uzushi wa vitabu vya wasanii ...

Utunzaji Bora wa Kuku wa Kienyeji

Utunzaji Bora wa Kuku wa Kienyeji Kuku wa kienyeji ni wale wa kiasili ambao hufugwa zaidi vijijini na wananchi ambao ni zaidi ya asilimia 80 ya idadi ya Watanzania wote. Kwa kawaida kuku hawa hujitafutia chakula chao wenyewe na wana uwezo wa kustahimili mazingira magumu. Vile vile wana uwezo wa kuatamia mayai na kutotoa vifaranga. Asilimia kubwa ya mayai na nyama inayotumika vijijini hutokana na kuku hawa na hata hivyo nyama na mayai yanayozalishwa ni kidogo kutokana na utaalamu duni. Ili kuongeza kiwango cha uzalishaji ni muhimu kufuata kanuni za ufugaji bora kama vile, banda bora, uchaguzi wa kuku walio bora, uanguaji na uleaji wa vifaranga, chakula bora na kuzuia magonjwa. Banda Bora Kuku wa kienyeji wanahitaji mahali safi na bora pa kulala. Kwa hiyo ni muhimu kuwajengea banda ambalo linaingiza hewa na mwanga wa kutosha. Banda liwe rahisi kusafishwa, na eneo la kutosha kufuatana na idadi ya kuku. Inafaa kuwawekea nyasi kavu au makapi ya mazao sakafuni. Eneo la kufugia lizungushiwe u...