Gharama Ununuzi wa ardhi kwa Tsh. 300,000-- Utayarishaji wa shamba Tsh 150,000/= kwa ekari - hatua 70x70 Gharama ya miche na upandaji miche 15,000 kwa ekari Tsh 750,000 (i.e.50 x 15,000 ikijumuisha ununuzi wa mbegu na upandaji), Mbolea 100,000. Matumizi mengine 200,000 (ikiwa ni pamoja ni vibarua, na kuleta mzigo sokoni). Jumla 1,500,000/- Mapato Nanasi unavuna baada ya miezi 18. kwa hesabu za chini kabisa unauza nanasi moja kwa Tsh 500 na assume unapata nanasi 12,000 utapata Tsh 6,000,000/=. (assumption ni kuwa si rahisi kupata mavuno 100%- bali inaweza kuwa 80%) Faida ukiondoa matumizi (Tsh 1,500,000) unapata faida 4,500,000 ukiwa na ekari tano bila shaka utapata zaidi ya milioni 20 (na hapo hujaweka economy of scale). --though unaweza kupunguza au kuongeza asilimia fulani kutegemeana na risks zilizopo na uzoefu wako katika kusimamia na kutafuta masoko.. Masoko Soko lipo huko huko shamba au unaleta mjini mfano kwa BAKHRESA anayenunua matunda kwa ajili ya kutengeneza juice....