Ufugaji wa mbuzi hapa ni fursa nadra ambayo Watanzania wengi hawajaiona. Ni ufugaji ambao wenyewe kama mfugaji atazingatia kanuni na misingi ya ufugaji Bora, ni rahisi sana mfugaji kujiondoa kutoka kwenye umasikini na kuwa tajiri. Kitu cha msingi na muhimu ni kwamba,mfugaji lazima awe na eneo pamoja na mtaji wa kuanzia.
Hawa ni mbuzi bora walioboreshwa, wanapatikana dodoma. Ni matokeo ya cross breed iliyofanyika kati ya mbuzi wa kienyeji wa dodoma na exotic breed.Hivyo wengi wa uzao wao huzaa mapacha. Mbuzi hawa huuzwa tsh elfu 50, wakiwa na umri wa miezi 5.
Hawa ni mbuzi bora walioboreshwa, wanapatikana dodoma. Ni matokeo ya cross breed iliyofanyika kati ya mbuzi wa kienyeji wa dodoma na exotic breed.Hivyo wengi wa uzao wao huzaa mapacha. Mbuzi hawa huuzwa tsh elfu 50, wakiwa na umri wa miezi 5.
Sehemu ya kufugia
Mbuzi wanatakiwa kufugwa shambani. Shamba ambalo mbuzi wanatakiwa wafugwe linapaswa liwe na sehemu ambayo mbuzi wanaweza kwenda kuchungwa na pia kuwe na chanzo cha maji. Mbuzi kitabia hupenda kulala juu hivyo mabanda yao yanapojengwa lazima yainuliwe juu. Mabanda ya mbuzi si ghari,kwani hujengwa simple.
Uzaaji
Mbuzi kwa mwaka huzaa mara mbili na ukipata ile mbegu ya wanaozaa mapacha faida yake huwa ni kubwa zaidi, itategemea na mtaji wa mfugaji, lakini kama mfugaji ataweza kuanza na mradi wa mbuzi 50 inakuwa vizuri zaidi.
Ukinunua mbuzi 50@ tsh.50,000/= utapata Milioni 2 na nusu [2,500,000], madume 2 kila moja likanunuliwa kwa tsh 75000/= kwa madume mawili itagharimu tsh laki moja na nusu.
Usafirishaji wa mbuzi hauzidi laki tatu na nusu. Kwa hiyo utajikuta ukiwa na milion 5 utaweza kuanza na mradi wa ufugaji wa mbuzi majike 50 na madume mawili,pamoja na kuwajengea sehemu ya ya kulala.
Mbuzi kwa mwaka wao huzaa mara 2, hivyo kama kila mbuzi atazaa hebu chukulia kila mbuzi atazaa mbuzi mmoja tu, ingawa kuna wengine watazaa mapacha hasa ukipata ile mbegu ya mbuzi wanaozaa mapacha, mwishoni mwa mwaka utakuwa na idadi ya mbuzi 100 wapya waliozaliwa na ukujumlisha na mtaji ule wa mbuzi 50 utakuwa na jumla ya mbuzi 150, hii ni ndani ya mwaka mmoja, pata picha utakuwa na mbuzi Idadi gani baada ya miaka 3 hasa ukizingatia kuwa wale watoto wa mbuzi watakapofikia miezi 8 utaanza kuwapandisha nao watazaa nk.
Magonjwa
Magonjwa ya mbuzi mengi yanafahamika na ni rahisi kudhibitika,hivyo mbuzi si rahisi kufa hovyo.
Toka mbuzi anapata mimba mpaka anazaa,hutumia muda wa miezi mitano yaani siku 150.Magonjwa ya mbuzi mengi yanafahamika na ni rahisi kudhibitika,hivyo mbuzi si rahisi kufa hovyo.
Ya kuzingatia
Ili kufikia malengo, inashauriwa kuwa mbuzi wa mtaji wanaonunuliwa lazima wawe na umri mmoja ili kusudi waweze kupata mimba kwa wakati mmoja na waweze kuzaa kwa wakati mmoja pia.
DARASA zuri k a wafugaji na wajasiriamali
ReplyDelete