UTANGULIZI
Tunda hili lina faida nyingi sana, mbali ya kutumika kama zao la kiuchumi lakini pia hutumika kuimarisha afya ya mwili
1. Faida za Parachichi upande wa Lishe
Tunda lina vitamini zifuatazo
- Lina Vitamini A-husaidia sana kuimarisha Macho kuona vizuri
- Lina Vitamini B (B1-B12)- Husaidia sana mfumo wa misuli ya mwili kuwa sawasa na kuuepusha mwili na matatizo ya nerve
- Lina Vitamini C-Husaidia sana upande wa kuimarisha ngozi, kwa sababu liko na mafuta, lina zaidi ya mara 4 ya virutubisho vya vitamini C vinavyopatikana katika machungwa
- Lina vitamini D-ambapo husaidia sana kuimarisha mifupa ya mwili
- Lina vitamini E-hii husaidia sana kuimarisha seli za uzazi, linasaidia sana kuongeza nguvu na utengenezwaji wa seli za uzazi
- Lina vitamini K-Husaidia sana kuganda kwa damu, na kuongeza uzalishaji wa chembe hai nyekundu za damu
Ni tunda lenye
- Madini ya Chuma kwa wingi (Fe)-Haya huaidia sana utengenezwaji wa damu, na kuongeza uwezekano wa damu kuwa na oxygeni ya kutosha na kusafirishwa kwa urahisi
- Madini ya Calcium-Lina madini ya calcium, yanayosaidia kama ufanyaji wa kazi wa seli hai za mwili
- Lina virutubisho vingine vidogo vidogo vingi, vinavyotakiwa katika ufanyaji kazi mzuri wa selli hai za mwili
Ni tunda linalopenda sana sehemu za baridi, maeneo kama ya Rungwe-Mbeya, Njombe, Makete, linastawi vizuri sana, na huwa na Fatty Contenty kubwa
- Joto
Nyuzi 15-25 Sentigrade - Muinuko
Mita 1200-1800 kutoka usawa wa baridi - Udongo
Uwe kichanga tifutifu (Sandy loam), usiotuamisha maji
1. Zipo aina za kiasili
Kila sehemu kuna iana za parachichi ambazo ni za asili ya eneo husika, parchichi hizi, huwa ndefu sana, na mavuno machache
2. Zipo aina za kisasa (Chotara)
Ziko aina nyingi sana za Parachichi chotara, na hizi hapa chini ni baadhi ya zile maarufu hapa tanzania
i. Hass
- Hii ni aina maarufu sana katika aina za parachichi
- Ni tunda linalokuwa na vipere vipere
- Limechongoka juu na chini
- Linahifadhika kwa urahisi
- Hili ni aina ya parachichi lenye ngozi laini saini, ngozi yake inateleza kama imepakwa mafuta
- liko na mafuta mengi ila linawahi kuoza
- Ni zuri kwa matumizi ya kawaida , si kwa kusafirisha umbali mrefu
- Aina hii ikilimwa sehemu za miinuko na baridi sana, inafaa sana kutoa mafuta mengi yanayoweza kutumika kutengeza lotion na baadhi ya vyakula vya mifugo
- Ana hii ni maarufu sana kwa mikoa ya nyanda za juu kusini (Mikoa ya Njombe, Iringa, Mbeya na Ruvuma)
- Mti wa aina hii huwa na majani mapana kama mti wa embe
- Mti huu huchukua muda mrefu sana kustawi
- Tunda lake huwa ni kubwa, na lina gharama sana
Nafasi kati ya shimo na shimo
- Umbali wa kutoka shimo hadi shimo ni MITA 7
- UMbali wa kutoka mstari hadi mstari ni MITA 7
- Hivyo nafasi yaweza kuwa
AU 9M X 9M-KWA NAFASI HII UTAKUWA NA MICHE 49 KWA EKA 1
AU 10M X 10M- KWA NAFASI HII UTAKUWA NA MICHE 40 KWA EKA 1
Ukubwa wa shimo
- Shimo laweza kuwa futi 2.5 x futi2.5 x futi 2.5 = (sm 75 x sm 75 x sm 75) (Kimo x upana x urefu)
- Au kipimo cha futi 3 x futi 3 x futi 3= sm 90 x sm 90 x sm 90
- Mbolea za kupandia zitakazohitajika , ni moja wapo kati ya hizi
- Samadi, Mboji, DAP, au TSP-Lakini ni muhimu kupandia mbolea asilia kama samadi ukachanganya kidogo na TSP au DAP
- Kama ni mbolea za asili (Samadi au Mboji)-Kiasi cha kilo 16 hadi 20 kinapaswa kiwekwe katika shimo miezi 3 kabla ya kupanda mche
- Kama utapandia mbolea za viwandani (TSP, DAP, Minjingu, NPK etc) kiasi cha gramu 100 hadi 200 kiwekwe kwa kila shimo, ichanganywe vizuri na udongo, kisha mmea uwekwe na kumwagiliwa
- Parachichi hasa hizi za kisasa, huanza kuzaa baada ya miaka 3 na matunda yake hukomaa baada ya miezi 6 hadi 12. Tunda la aina ya HASS ndilo huchelewa zaidi kukomaa huchukua kati ya mizei 7 hadi 12 tangu lilipo jitengeneza katika mti.
- Kwa mara ya kwanza mti mmoja wa parachichi unaweza kukupa kati ya matunda 50 hadi 100 kwa mche mmoja.
- Mavuno hueongezeka kadri umri unavyoongezeka
- Mti wa parachichi ukifikia umri wa miaka 4 hadi 5, unakuwa full maturity, na hivyo mti mmoja unaweza kukupa hadi matunda 1200 kwa mwaka mzima '
kwa kipimo cha mita 10 x mita 10, katika eka mmoja utakuwa na mita 40
- Kila mti baada ya mika 5 unaweza kukupa wastani wa matunda 1000
- Hivyo kwa miti 40, utakuw na jumla ya matunda 40 x 1000= 40,000
- Kila tunda kwa bei ya shambani uuze tsh 250, na unamatunda 40,000
- Hivyo utapata jumla ya tsh 250 x matunda 40,000= 10,000,000tsh (MILIONI 10)
NAPATA VIPI MBEGU
ReplyDelete