Skip to main content

Upandaji na Utunzaji wa Miti



a)      Kutayarisha shamba
Inapendekezwa kuwa pale inapowezekana shamba lilimwe kabisa kabla ya kupanda. Gharama ya kulima inaweza ikapunguzwa kwa kuchanganya miti na mazao ya kilimo, yaani kilimo mseto (Agroforestry) kama vile pamba, mahindi, mtama, tumbaku n.k  Utaratibu huu pia unapunguza gharama ya kupalilia. Miti mingine kama vile migriveria, mijohoro, miarobaini na mikenge inaweza kupandwa moja kwa moja katika mbuga mradi eneo kuzunguka shimo la kupandia mche limelimwa kabla ya kupanda.

b)     Majira ya kupanda
Kupanda miti kufanyike wakati wa mvua, yaani, wakati udongo una unyevuunyevu wa kutosha. Katika sehemu zenye mvua nyingi, ni rahisi kutekeleza jambo hili kwa sababu hali hiyo inaendelea kwa muda mrefu baada ya kuanza mvua za masika, wakati huo ni Machi na Aprili. Katika maeneo hayo inashauriwa kufuata majira yaleyale ya kupanda mazao ya chakula. Ni vizuri zaidi kupanda mara tu mvua za masika zinapoanza kunyesha.

Kutayarisha Mashimo ya Kupanda
Umbali kati  mti na mti hutegemea aina ya mti na madhumuni ya kuipanda. Iwapo madhumuni ni kuanzaisha shamba la miti (msitu) kwa kawaida umabli unaofaa ni mita 2.5 x 2.5 ambalo ni sawasawa na miti 1,600 kwa hekta 1. Kwa miti ambayo haikupandwa katika shamba la miti katika mtindo wa kilimo mseto, miti ipandwe kwa nafasi kufuatana na aina ya miti na matumizi, mfano: nguzo, malisho na uzio.  
Mashimo yenye upana wa Sm 30 (ft 1) na kina Sm 30 yachimbwe kwa mstari kwa kutumia kamba kisha miche isafirishwe kwa unagalifu kutoka katika bustani na kupandwa katika shimo mara moja, Kiriba lazima kiondolewe kabla ya kupanda. Wakati wa kupanda ni vyema kufukia mche kwa kutumia udongo kuzunguka mche ushindiliwe kwa uangalifu bila kukata mizizi ya mche.

Kutunza Shamba la Miti
a)      Kupalilia
Miti ya aina karibu zote haiwezi kuvumilia magugu. Isipopaliliwa mapema hudhoofika na hata kama baadaye ikipaliliwa itachukua muda mrefu kurudia hali yake ya awali. Miti mingine hufa kwa sababu ya magugu. Njia nzuri ya kuthibiti magugu ni kulima shamba vizuri kabla ya kupanda. Pale ambapo hakuna mazao ya kilimo, ni vyema kupalilia eneo lenye kipenyo cha m1 kuzunguka mti na pia kufyeka majani marefu kati ya miti.

b)     Kukatia matawi na kupunguza miti
Kwa baadhi ya miti ni vyema kukatia matawi ya chini katika kipindi cha miaka miwili ya mwanzo. Hii inasaidia wafanyakazi kupitia kwa urahisi katika shamba. Pia inazuia moto usisambae iwapo utatokea. Miti ya mbao kama vile msindano (Pine) na msanduku (Cypress) ina utaratibu maalumu uliowekwa (Pruning Schedule) wa kukatia matawi kulingana na umri na mahali ulipopandwa. Aina nyingi za miti hazina utaraibu maalumu wa kuipunguza, lakini kila mti uliokufa sharti uondolewe ili kutoa nafasi ya miti iliyo na afya. Pia miti ya msindano na msanduku ina utaratibu maalumu wa kupunguza miti (Thinning schedule). Zoezi hili hutegemeana na matumizi yaliyokusudiwa k.m kuni, mbao na karatasi n.k

Comments

Popular posts from this blog

Utengenezaji wa Chakula cha Kuku wa Nyama (Bloilers)

Utangulizi Kuku wa nyama wana mahitaji yafuatayo ya viinilishe katika chakula ili wakue vizuri Viinilisha vya wanga 60-65%   Protini 30-35%   Madini 2-8% Chakula cha Vifaranga Chakula hiki hutengenezwa katika namna ya kumsaidia kifaranga aweze kumeza vizuri na hivyo hakitakiwi kuwa katika punje punje. Hata kama utanunua pumba, ni vema kuzipitisha kwenye mashine ili ziwe laini zaidi.  Mahitaji (kgs)  Unga wa dona wa nafaka kama mahindi au mtama 40  Pumba za mtama au mahindi au uwele 27  Mashudu ya alizeti au ufuta, au pamba au karanga n.k. 20  Unga wa mifupa au chokaa ya kuku (DCP) 2.25  Dagaa au mabaki ya samaki (sangara fish meal) 10  Chumvi ya jikoni 0.5  Virutubisho (Broiler premix) 0.25  Jumla utapata 100Kg. Chakula cha kukuzia – growers mash Mahitaji (Kg) Mahindi yaliyobarazwa au mtama au uwele 25   Pumba za mtama au mahindi au uwele 44   Mashudu ya alizeti au ufuta, au pamba au karanga n.k. 17   Unga wa mifupa a...

Aina Za Miti ya Minazi

AINA ZA MINAZI Inafaa mkulima kufahamu kuna aina mbali mbali za minazi na ina mahitaji tofauti katika ukuaji. Ujuzi huu utamsaidia katika kuchagua aina ya minazi itakayofaa kwa eneo lake na kwa kiwango chake cha utunzaji. KUNA AINA TATU ZA MINAZI Minazi mirefu ya asili Minazi mifupi Minazi chotara MINAZI MIREFU YA ASILI (EAT) Minazi ya aina hii ndiyo inayojulikana na wakulima wengi kwa vile ni ya kiasili na imezoea mazingira yetu. Minazi hii huchukua miaka 6-8 tangu kupandikizwa hadi kuzaa. Minazi ya aina hii huvumilia ukame na inao uwezo wa kutoa wastani wa nazi 40 kwa mwaka. Nazi huwa kubwa na zenye nyama nene ambayo inafaa kwa kupikia na kukamua mafuta. Minazi hii huishi kad ya miaka 60 na kuendelea. Nchini Tanzania, minazi hii hustawi vyema ukanda wa pwani sehemu zisizo na mawe na ambazo hazituamishi maji. MINAZI MIFUPI (DWARF) Minazi ya aina hii huzaa mapema kuanzia miaka miwili. Huzaa nazi nyingi na ndogo. Nazi hizi huwa na nyama nyembamba hivyo hutumika kwa nnadafu. Minazi huhit...

Kilimo Bora cha Migomba

UTANGULIZI Hapa Tanzania kilimo cha migomba kimekuwepo Kwa miaka mingi. Kilimo hiki ni maarufu sana kwa sababu zao la ndizi limekuwa likitumika kama chakula kikuu kwa baadhi ya mikoa kama vile Kagera, Kilimanjaro na Mbeya na hivyo kulifanya muhimu, kufuatia mazao ya mahindi, mpunga, mtama, muhogo,viazi na mazao ya jamii ya kunde kama vile maharage. Zao la ndizi linaweza kuwa moja kati ya mazao ya biashara iwapo litazalishwa kwa kufuata kanuni bora za uzalishaji wa zao hilo, ikwa ni pamoja na kupanda aina bora ya migomba inayozaa ndizi zinazotambulika katika masoko ya kimataifa. ASILI YA MIGOMBA Asili ya migomba ni nchi za Malaysia na India ambazo ziko Kusini Mashariki mwa Asia. Migomba inayolimwa sasa imetokana na migomba ijulikanayo kama Musa balbisiana ambayo asili yake ni India, na Musa acuminata ambayo asili yake ni Malaysia. Kutoka Malaysia na India migomba ilifika Afrika Mashariki katika karne ya tano MAENEO YANAYOLIMWA MIGOMBA NCHINI Nchini Tanzania mikoa inayoshughulika na kili...