Skip to main content

Kutunza Bustani Kwaweza Kukunufaisha

JE, WEWE hufurahia kutunza bustani? Huenda unanufaika hata zaidi kutokana na utendaji huo. Kulingana na gazeti moja la London (Independent), watafiti wamegundua kwamba “kutunza bustani hukusaidia kuwa na afya nzuri zaidi, hupunguza mifadhaiko, hushusha shinikizo la damu na hata kukusaidia kuishi kwa muda mrefu zaidi.”
Mhariri G. Search anasema: “Baada ya siku yenye shughuli nyingi na mambo mengi yenye kufadhaisha, kurudi nyumbani na kutunza bustani yako huburudisha sana.” Mbali na kuwa jambo lenye kuthawabisha na kupendeza, kutunza bustani kunakuwezesha kupata mazoezi mazuri zaidi ya mwili kuliko kwenda katika chumba cha mazoezi. Jinsi gani? Kulingana na Search, “utendaji kama vile kulima na kukusanya majani ni mazoezi mazuri yanayotumia kalori nyingi zaidi kuliko kuendesha baiskeli.”
Kutunza bustani huwanufaisha hasa wazee. Kusubiri chipukizi au mche mpya uibuke huwasaidia kutazamia wakati ujao wakiwa na uhakika. Pia, “bustani hutuliza maumivu na mfadhaiko” unaosababishwa na uzee, asema Dakt. Brigid Boardman wa Royal Horticultural Society. Mara nyingi wazee huvunjika moyo kwa sababu ya kuwategemea sana wengine. Hata hivyo, kama Dakt. Boardman anavyosema, “ile hisia ya kutaka kujitegemea inatoshelezwa kwa kuamua kitakachopandwa, mahali kitakapopandwa, na jinsi ya kuitunza bustani. Na ule uhitaji wa kutunza unatoshelezwa pia.”
Wale walio na matatizo ya akili mara nyingi hutulia wanapofanya kazi katika mazingira mazuri, matulivu. Isitoshe, kupanda maua au chakula kwa ajili ya wengine kwaweza kuwasaidia watu hao wajiamini tena na kujiheshimu.
Hata hivyo, wanaofaidika na bustani hizo si wale wanaozitunza tu. Profesa Roger Ulrich wa Chuo Kikuu cha Texas alifanya majaribio kwa kutumia kikundi cha watu waliokuwa wametiwa chini ya mkazo. Aligundua kwamba wale waliopelekwa mahali penye miti na majani mengi walipata nafuu haraka—kulingana na mpigo wa moyo na shinikizo la damu—kuliko wale ambao hawakuwekwa katika mazingira hayo ya asili. Jaribio kama hilo lilionyesha kwamba wagonjwa wanaoendelea kupata nafuu katika hospitali baada ya kufanyiwa upasuaji walinufaika kwa kukaa katika vyumba ambamo wangeweza kuona miti. Tofauti na wagonjwa wengine, “walipata nafuu haraka, wakarudi nyumbani mapema, hawakuhitaji dawa nyingi za kutuliza maumivu, na walikuwa na malalamiko machache zaidi.”

Comments

Popular posts from this blog

Kanuni za Ufugaji Bora wa Mbuzi na Kondoo

Utangulizi Mbuzi na kondoo wanaweza kufugwa kwa gharama nafuu na kuishi katika mazingira magumu kama ya maradhi na ukame ikilinganishwa na ng’ombe. Kutokana na umbile lao dogo wanaweza kufugwa katika eneo dogo na pia wanaweza kuhudumiwa na familia yenye nguvukazi na kipato kidogo. Uzao wa muda mfupi unamwezesha mfugaji kupata mbuzi/kondoo wengi kwa kipindi kifupi. Wanyama hao hufugwa kwa ajili ya nyama, maziwa, ngozi, sufu na mazao mengine kwa matumizi ya familia na kuongeza kipato.  Kanuni za kuzingatia Ufugaji bora wa mbuzi na kondoo uzingatie kanuni zifuatazo:- Wafugwe kwenye banda au zizi bora, Wachaguliwe kutokana na sifa za koo/aina na lengo la uzalishaji (nyama, maziwa au sufu), Wapatiwe lishe sahihi kulingana na umri na mahitaji ya mwili, Kuzingatia mbinu za kudhibiti magonjwa kama inavyoshauriwa na mtaalam wa mifugo, Kuweka na kutunza kumbukumbu sahihi za uzalishaji; na  Kuzalisha nyama, maziwa au sufu yenye ubora unaokidhi mahitaji ya soko Zizi au Banda la Mbuzi/Kond...

Kilimo Bora cha Alizeti - Uzalishaji, Uangalizi, Uvunaji na Uhifadhi

Utangulizi Alizeti hulimwa kwa wingi katika mikoa ya Shinyanga, Singida, Dodoma, Iringa, Tabora, Morogoro, Ruvuma, Mbeya, Arusha, Manyara, na RukwaZao hili hulimwa kwa ajili ya chakula na biashara. Mambo muhimu ya kuzingatia wakati wa uzalishaji Kuchagua aina bora ya mbegu Chagua aina bora ya mbegu inayovumilia magonjwa, wadudu, inayotoa mazao mengi na kiwango kikubwa cha mafuta. Vilevile chagua aina ya mbegu ambayo hukomaa kwa wakati mmoja ili kurahisisha uvunaji. Kuweka mbolea Rutubisha udongo kwa kutumia mbolea za mboji na samadi ili kupata mazao mengi na bora. Kudhibiti wadudu na magonjwa Alizeti hushambuliwa na magonjwa ya majani, mizizi na masuke ambayo husababisha upungufu wa mavunoHivyo ni muhimu kuyadhibiti ili kupata mavuno mengi na boraPia ndege hupunguza mavuno kwa kiasi cha asilimia 50 au zaidiNjia ya kudhibiti ndege ni kwa kuwafukuza na kupanda mbegu zinazokomaa mapema. Maandalizi kabla ya kuvuna;  Ukaguzi  Kagua shamba kuona kama alizeti imekomaaAlizeti hukomaa ...

Utengenezaji wa Chakula cha Kuku wa Nyama (Bloilers)

Utangulizi Kuku wa nyama wana mahitaji yafuatayo ya viinilishe katika chakula ili wakue vizuri Viinilisha vya wanga 60-65%   Protini 30-35%   Madini 2-8% Chakula cha Vifaranga Chakula hiki hutengenezwa katika namna ya kumsaidia kifaranga aweze kumeza vizuri na hivyo hakitakiwi kuwa katika punje punje. Hata kama utanunua pumba, ni vema kuzipitisha kwenye mashine ili ziwe laini zaidi.  Mahitaji (kgs)  Unga wa dona wa nafaka kama mahindi au mtama 40  Pumba za mtama au mahindi au uwele 27  Mashudu ya alizeti au ufuta, au pamba au karanga n.k. 20  Unga wa mifupa au chokaa ya kuku (DCP) 2.25  Dagaa au mabaki ya samaki (sangara fish meal) 10  Chumvi ya jikoni 0.5  Virutubisho (Broiler premix) 0.25  Jumla utapata 100Kg. Chakula cha kukuzia – growers mash Mahitaji (Kg) Mahindi yaliyobarazwa au mtama au uwele 25   Pumba za mtama au mahindi au uwele 44   Mashudu ya alizeti au ufuta, au pamba au karanga n.k. 17   Unga wa mifupa a...