Skip to main content

kilimo cha Matunda - Mapapai


UTANGULIZI
Mapapai ni matunda ambayo wengi tunayafahamu. Ekari moja ya papai inachukua miche 1000-1200. Kwa maana ya mita mbili kwa mbili kutoka mti hadi mti na hii ni kwa ile mbegu fupi. Ukilima kwa kufuata utaalamu ni kwamba mti mmoja wa papai unaweza kutoa matunda 86 hadi 100 kwa msimu.Kutoka kupandikiza shambani hadi kuanza kuvuna mavuno ya kwanza, papai zinachukua miezi nane hadi kumi tu. Ikiwa unamwagilia papai ni tunda lisilo na msimu, yaani unavuna mfululizo......

Mti mmoja unatoa matunda 86 hadi 100 sasa kwa ajili ya kustandadaizi tuchukulie kwamba mti umekupatia matunda 80 pekee. Tunda moja la papai, kwa pale sokoni linauzwa kuanzia 1000, hadi elfu 4,000 kutegemea na ukubwa, lakini ni nadra kupata papai chini ya shilingi 1,000 kule sokoni, si ndio jamani? 

Sasa ukilima chukulia kwamba unauza 500 kila tunda kwa bei ya kujumlishia pale pale shambani (yaani hutaki mausumbufu ya kupeleka sokoni, unawaita wajumuaji wanunulie hapo hapo shambani). Ikiwa mti mmoja unatoa papai 80 maana yake kila mti utakupatia shilingi elfu arobaini, 40,000/=. 

Kitaalamu inashauriwa kwamba miti ya mipapai inatakiwa kukaa shambani kwa miaka isiyozidi mitano na baada ya hapo ing'olewe na kubadilishwa mingine. Pia inaelezwa kwamba mavuno makubwa zaidi(maximum production) unaipata kuanzia mwaka wa pili wa mavuno. Maana yake ni kwamba shamba la papai unaweza kukodi ama kununua.

MAHITAJI
Hali ya hewa inayofaa kwa mipapai ni ya kitropik ambayo haina baridi kali na joto kiasi . Udongo usiotuamisha maji maji yakisimama kwa masaa 48 tu mpapai unaweza kufa, wenye ruruba ya kutosha kwa sababu mipapai haina mzizi mkuu haihiyaji udongo wenye kina kirefu, kipindi cha jua kali mpapai usiachwe zaidi ya wiki 8 bila kumwagiliwa maji kama hakuna mvua ingawa wakati wa mapapai kuiva kama kuna ukame basi hii huongeza ubora wa papai ikiwamo kutooza mapema sokoni

Mipapai ipandwe sehemu ambazo hazina upepo mwingi kwani huvunjika kirahisi, kama unashamba la mipapai itakubidi kupanda miti ya kukinga upepo kuzunguka shamba lako, miti kama miparachichi, migravilea, vibiriti (leucaena Spp) na miembe pia inafaa. Hakikisha miti ya kukinga upepo inakuwa mirefu kuzidi mipapai kwa mita 10 mpaka 20 juu zaidi.

Kuendelea kupanda mipapai kwenye shamba moja kunaweza kusababisha usugu wa magonjwa, nashauri baada ya miaka 3 – 5 ubadilishe zao hili angalau kwa msimu mmoja ili kuua mzunguko wa magonjwa
Mipapai inaweza kuchanganganywa na miembe na mimea jamii ya michungwa, pia mazao ya msimu kama mahindi, mtama, ufuta , alizeti na mboga mboga yanaweza kulimwa

Kwa kaida kwenye mipapai kuna mipapai dume, majike na yenye jinsia zote (multiplesex/hermaphrodite) ambayo huwa na mapapai marefu zaidi, na pia kuna isiyoeleweka ambayo huwa na mapapai mafupi sana.

MBEGU
Kusanya mbegu toka kwenye mapai makubwa na yaliyo komaa na kuiva, kausha mbegu vizuri kbla ya kupanda, kama utapata mbegu za kununua ni vizuri zaidi, baada ya kukausha hakikisha unazipanda ndani ya wiki moja
  • Papai lililokomaa linaweza kutumika kama mbegu
KUOTESHA MBEGU
Kuna wanaopendelea kuotesha mbegu kwanza na kisha kuhamishia miche shambani, sehemu ya kuoteshea iandaliwe miezi miwili kabla, mbegu zioteshwe kwenye kina kati ya sentimeta 1 chini ya udongo wenye rutuba au pakiti za plastiki, kiwango bora cha joto ni sentigredi 21 na 27 na itachukua kati ya wiki 1 mpaka 4 kwa mbegu kuota, kwenye kila pakiti weka mbegu 2 au 3. Panda mbegu zako kwenye kitalu kwa umbali wa sentimeta 3 toka shimo hadi shimo na sentimeta 15 kati ya mistari, hakikisha maji hayatuami kabisa, pia unaweza kupiga dawa ya copper oxychloride gramu moja katika lita moja ya maji ilikukinga miche yako na fangasi.

UOTESHAJI WA MOJA KWA MOJA
Kabla ya kupanda mbegu weka mchanganyiko wa majivu na mbolea ya kuku sehemu ya kupandia, mbolea husaidia ukuaji haraka na jivu husaidia kukinga mipapai na magonjwa. Panda mbegu 3 mpaka 5 kila shimo maana miche mingine inaweza kufa kwa magonjwa, kuliwa na wadudu au ikaota dume

KUHAMISHA MICHE TOKA KWENYE KITALU
Miche ihamishiwe shambani ikiwa na urefu wa sentimeta 20 – 40, kama udongo unatuamisha maji panda kwenye matuta yenye urefu wa sentimeta 40 – 60 mashimo yawe na ukubwa wa sentimeta 45 upana na sentimeta 30 kina na shimo lichanganywe na udongo na samadi bila kuacha kisahani cha maji, umbali ni mita 3 kwa 3 kwani mipapai inahitaji jua la kutosha.

KUPUNGUZA MIPAPAI
Baada ya miezi 3 mpaka 5 baada ya kupanda mipapai itatoa maua na hapo jinsia ya mipapai itajulikana na mingine itabidi ipunguzwe na hasa midume, mipapai yenye jinsi zote inatakiwa isizidi asilimia 10 au; 20 na midume ibaki mmoja katika kila mijike 25, mimea yenye magonjwa pia inabidi ing';olewe

RUTUBA YA UDONGO
Weka kiasi cha kilo 2 mpaka 5 za samadi kwenye kila mpapai kwa mwaka ili kuongeza ukuaji na uzazi, mabaki ya mimea yanaweza pia kuwekwa kama matandazo na h ii ni muhimu zaidi kipindi cha kiangazi ili kuzuia unyevu usipotee.

MAGUGU
Mipapai inapopandwa tu inaweza kuwekewa matandazo kuizunguka ili kuzuia uoataji wa magugu, magugu yang'olewe yakiwa machanga na epuka kuchimbua chini sana maana mizizi ya mipapai huwa juu juu, njia nzuri ni kuweka matandazo kwenye shamba lote ili kuzuia outaji wa magugu

UANGALIZI
  • Mipapai iangaliwe dhidi ya magonjwa, ing'olewe na kuchomwa au kufukiwa chini ikiwa itabainika kuwa na maonjwa, piga dawa dhidi ya magonjwa ya fangasi na virusi mara yanapoibuka ili kuongeza uzaaji nakipato chako.
  • Ondoa matawi yote yatakayojitokeza pembeni ya mpapai wako, na hii ifanyike mapema kabla ya tawi kuwa kubwa.
  • Ondoa mapapi yote ambayo yatakuwa hayakuchavuliwa vizuri na acha yale yenye afya tu.
  • Weka miti ya kuegemea kama mpapai utazaa matunda mengi na hasa wakati wa upepo mwingi ili kuzuia mipapai isivunjike.

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

Utengenezaji wa Chakula cha Kuku wa Nyama (Bloilers)

Utangulizi Kuku wa nyama wana mahitaji yafuatayo ya viinilishe katika chakula ili wakue vizuri Viinilisha vya wanga 60-65%   Protini 30-35%   Madini 2-8% Chakula cha Vifaranga Chakula hiki hutengenezwa katika namna ya kumsaidia kifaranga aweze kumeza vizuri na hivyo hakitakiwi kuwa katika punje punje. Hata kama utanunua pumba, ni vema kuzipitisha kwenye mashine ili ziwe laini zaidi.  Mahitaji (kgs)  Unga wa dona wa nafaka kama mahindi au mtama 40  Pumba za mtama au mahindi au uwele 27  Mashudu ya alizeti au ufuta, au pamba au karanga n.k. 20  Unga wa mifupa au chokaa ya kuku (DCP) 2.25  Dagaa au mabaki ya samaki (sangara fish meal) 10  Chumvi ya jikoni 0.5  Virutubisho (Broiler premix) 0.25  Jumla utapata 100Kg. Chakula cha kukuzia – growers mash Mahitaji (Kg) Mahindi yaliyobarazwa au mtama au uwele 25   Pumba za mtama au mahindi au uwele 44   Mashudu ya alizeti au ufuta, au pamba au karanga n.k. 17   Unga wa mifupa au chokaa ya kuku (DCP) 3.25   Dagaa au mabaki ya samaki (fish meal) 1

Aina Za Miti ya Minazi

AINA ZA MINAZI Inafaa mkulima kufahamu kuna aina mbali mbali za minazi na ina mahitaji tofauti katika ukuaji. Ujuzi huu utamsaidia katika kuchagua aina ya minazi itakayofaa kwa eneo lake na kwa kiwango chake cha utunzaji. KUNA AINA TATU ZA MINAZI Minazi mirefu ya asili Minazi mifupi Minazi chotara MINAZI MIREFU YA ASILI (EAT) Minazi ya aina hii ndiyo inayojulikana na wakulima wengi kwa vile ni ya kiasili na imezoea mazingira yetu. Minazi hii huchukua miaka 6-8 tangu kupandikizwa hadi kuzaa. Minazi ya aina hii huvumilia ukame na inao uwezo wa kutoa wastani wa nazi 40 kwa mwaka. Nazi huwa kubwa na zenye nyama nene ambayo inafaa kwa kupikia na kukamua mafuta. Minazi hii huishi kad ya miaka 60 na kuendelea. Nchini Tanzania, minazi hii hustawi vyema ukanda wa pwani sehemu zisizo na mawe na ambazo hazituamishi maji. MINAZI MIFUPI (DWARF) Minazi ya aina hii huzaa mapema kuanzia miaka miwili. Huzaa nazi nyingi na ndogo. Nazi hizi huwa na nyama nyembamba hivyo hutumika kwa nnadafu. Minazi huhit

Kilimo cha Miti ya Mbao - Uwekezaji wa Muda wa Kati na Mrefu

Utangulizi Kilimo cha miti ni uwekezaji wa muda wa kati na mrefu (mid & long term investments). Ila kwa kawaida jamii nyingi hasa za kiafrika huwa hazivutiwi na uwekezaji wa muda mrefu. Hata hivyo kama una mpango wa kuwa imara kiuchumi inashauriwaau yakupasa kufikiria na kujifunza aina za uwekezaji wa muda mrefu. Miti hutumika kwa matumizi mengi mfano mbao, nguzo za umeme na kujengea, mapambo, kuni na mkaa, kuzalisha matunda, mitishamba na madawa,  utengenezeaji wa karatasi n.k.  Mchanganuo Ekari moja ya shamba unaweza kupanda miti mia sita (500) mpaka mia saba (700). Gharama za kununua mashamba au maeneo ya kupandia miti hutegemea na eneo. Kwa  sehemu nyingi za vijijini maeneo kwa ekari moja hayazidi laki 5.  Miche ya kununua mfano Mitiki huuzwa kuanzia elfu moja (1000) kwa mche mmoja Gharama ya kununua miche =  1000 * 600 = 600,000   Pia unaweza kuokoa gharama za kununua miche kwa kuioteshe mwenyewe ktk vitalu na kuiamishia shambani baada ya kustawi vizuri na kuwa imara.  Mf. Mbe