UTANGULIZI
Tiba asili kwa karne ya sasa imeonekana kuwa tiba mbadala ya dawa za hospitalini kwa sababu ya madhara yake kuwa madogo kwenye mwili mara baada ya kuyatumia. Madawa haya ya asili yamekuwa yakitumiwa na binadamu tangu enzi hata kabla ya madawa ya kikemikali kuvumbuliwa na mwanadamu. Lakini kasi ya madawa ya kikemikali yalishika kasi kwa sababu ya uharaka wake wa kutibu magonjwa kwa muda mfupi tena kiasi kidogo sana kikitumika. Tatizo la madawa ya asili ilikuwa kutokuwa na uhakika wa dosi na wakati mwingine mgonjwa alihitaji kunywa dawa nyingi sana pasipo mafanikio. Hata hivyo siku za hivi karibuni binadamu ameona ni vema kurejelea dawa za asili huku akifanya maboresho kwa kujua kiasi halisi cha dozi ya dawa. Dawa nyingine zimeboreshwa zaidi na kufanya kiasi kidogo cha dozi kutumika kama dawa za kikemikali tofauti ni madhara machache ya dawa za asili.
Dawa za asili zinahitaji uvumilivu kiasi kwani zinachukua muda ili kufanya kazi huku zikiacha mdhara machache. Dawa hizi zimekuwa zikitumika pia kutibu mifugo hasa kwa zile familia za kifugaji, lakini watu wengine walioibukia ufugaji hawajajua ujuzi huu. Hata hivyo watu mbalimbali wamekuwa wakiandika matumizi ya dawa za asili kwa ajili ya matibabu ya mifugo ili watu wengi zaidi waweze kuzitumia. Hapa chini ni orodha ya miti inayotumika kama dawa kwa ajili ya mifugo na aina ya magonjwa yanayoweza kutibiwa na hiyo miti.
Dawa za asili zinahitaji uvumilivu kiasi kwani zinachukua muda ili kufanya kazi huku zikiacha mdhara machache. Dawa hizi zimekuwa zikitumika pia kutibu mifugo hasa kwa zile familia za kifugaji, lakini watu wengine walioibukia ufugaji hawajajua ujuzi huu. Hata hivyo watu mbalimbali wamekuwa wakiandika matumizi ya dawa za asili kwa ajili ya matibabu ya mifugo ili watu wengi zaidi waweze kuzitumia. Hapa chini ni orodha ya miti inayotumika kama dawa kwa ajili ya mifugo na aina ya magonjwa yanayoweza kutibiwa na hiyo miti.
1. SHUBIRI MWITU (ALOE) TIBA YA MAGONJWA YA KUKU
Shubiri mwitu (Aloe) ni mmea ambao umekuwa ukitumika kwa kutibu magonjwa mbalimbali ya binadamu na mifugo. Mmea huu unatumika sasa kutengeneza sabuni, dawa za binadamu na wanyama na mambo mengine mengi. Na kwa sababu ya madawa mengi ya kiwandani kushindwa kutibu baadhi ya magonjwa kwa sababu wadudu wametengeza ukinzani, ipo haja kubwa ya kuweka umuhimu kwenye madawa ya asili yatokanayo na mimea. Mmea wa aloe vera unauwezo wa kutibu magonjwa ya kuku hasa coccidiosis na kwa kiasi fulani Newcastle disease. Tafiti zilifanyika kwa kutmia mti huu kutibu ugonjwa coccidiosis ambao unamadhara makubwa kwa wafugaji wa kuku zinaonyesha kuwa mti huu unaweza kutumiwa kama mbadala wa dawa za viwandani.
Maji maji ya mmea huu yanauwezo wa kutibu magonjwa na kuponyesha majeraha yanayotokana na maambukizi ya magonjwa pamoja na kupandisha kinga ya kuku kwa asilimia 50 dhidi ya maonjwa mbalimbali.
Mmea wa aloe vera unaweza kupandwa maeneo ya karibu na mabanda ya kuku ili kurahisisha upatikanaji wake na unakubali maeneo karibu yote.
Majina ya mmea huu kulingana na baadhi ya makabila na kimataifa
Jina la Mmea
- Shubiri mwitu Kiswahili
- Mkankiruri Kinyaturu
- Itembwe Kigogo
- Ibhata Kinyiha
- Litembwetembwe Kihehe
- Koli Kikaguru/Kinguu
- Aloe Kiingereza
- Aloe vera Kisayansi
Shubiri mwitu kwa ukuaji wa kuku
Kulingana na tafiti zilizofanywa na Bejar (Chuo kikuu cha Kilimo na Misitu cha Samar) na Clapo (Chuo Kikuu cha Ufilipino Mashariki) inaonyesha kuwa ziada ya Shubiri mwitu kwenye maji inasaidia kwa kiasi kikubwa kuku kukua haraka. Mililita 15 had 20 za maji ya shubiri mwitu yakichanganywa na lita tano za maji kila siku kwa kuku 90 yanauwezo wa kusaidia ukuaji wa kuku na kuongeza uzito wa ukilinganisha na wale ambao hawajapewa.
Uandaaji wa Shubiri mwitu
Kunjwa: Shubiri mwitu (moja) inaweza kukatwe vipande vipande na kulowekwa ndani ya maji ya kunywa kiasi cha lita 1-hadi 3 kutegemeana na idadi ya kuku. Viache humo kwa siku kadhaa hadi unapobadilisha maji ndipo uviweke vingine. Ukiweza kuchuja mchuzi wa shubiri mwitu basi unakuwa ukitumia mililita 15 ndani ya lita tano ya maji ya kunywa kuku kwa kuku 90 kama unakuku wachache basi punguza kiasi cha dawa au ongeza kama ni wengi.
Vidonda:Kuku wenye vidonda kama kwa ugonjwa wa mdondo (Newcastle Disease) inakubidi utengeneze unga. Kata vipande vidovidogo vya shubiri mwitu kisha changanya na pumba kidogo, vitwange na kuvichekecha ili upate unga laini. Uanike na kisha tunza vizuri tayari kwa kuutumia mara kuku wauguapo. Kuku wenye vidonda waoshwe vizuri kwa maji safi na sabuni pamoja na chumvi kidogo. Baada ya hapo paka unga wa shubiri kwenye vidonda hivyo.
2. MPAPAI (Carica papaya) DAWA YA KUTIBU MAGONJWA YA MIFUGO
Asili ya mpapai ni Amerika ya Kati. Matunda, majani na utomvu wake hutumiwa kama dawa maeneo mbalimbali ya dunia, matunda na utomvu wake umekuwa ukitumika kutengeneza bombe na waini. Mpapayi una viini hai vingi lakini hivi viwili ni muhimu kwa kutibu magonjwa na kusaidia mmeng’enyo wa chakula ufanyike vizuri: chymopapain and papain. Kiasi cha viini hai hivi hutofautiana kwenye matunda, utomvu, majani na mizizi lakini pia kutegemeana na umri wa mti na njia ya kutengeneza dawa yenyewe.
Matumizi kwa mifugo
- Kutibu magonjwa ya bakteria: Matawi na mbegu za mpapai vina uwezo wa kutibu magonjwa yanayoenezwa na bakteria hawa: Staphylococcus aureua, Escherichia coli, Salmonella typhi na Bacillus subtilis.
- Kutibu magonjwa ya fangasi: Utomvu wa mpapai unauwezo wa kutibu fangasi inayoenezwa na Candida albicans
- Magonjwa ya minyoo:Unga wa mbegu za mpapai unauwezo wa kutibu minyoo ya umbwa inayojulikana kama Dirofilaria immitis (inayoshambulia moyo). Wapewe dozi ya milligram 60 kwa kila kilo moja ya uzito wa mbwa kwa muda wa siku 30. Minyoo mingine pia inaweza kutibiwa na mmea wa mpapai kama Ascaris suum kwa nguruwe katika dozi kati ya milligram 4-8 kwa kila kilo moja ya uzito wa nguruwe kwa muda wa siku 7. Utibuji wa minyoo kwa mifugo ndiyo kivutiuo kwa wafugaji.
- Mpapai pia unauwezo wa kusaidia mnyama aharishe ili kutoa kitu ambacho hakifai tumboni.
Kwa binadamu mmea huu umekuwa ukitumika sehemu mbalimbali kutibu magonjwa/matatizo yafuatayo: Kuharisha na kuharisha damu, magonjwa ya figo, ini, kichaa, mafua, homa, kuongeza utoaji wa maziwa, matatizo ya mmeng’enyo wa chakula, vidonda na asthma.
Comments
Post a Comment