Katika uchaguzi wa eneo kwa ajili ya bustani zingatia yafuatayo:
- Mwinuko
Eneo lisiwe kwenye mwinuko mkali kwa sababu sehemu kama hizo zinaweza kusababisha mmomonyoko wa udongo. Endapo sehemu itakuwa ya mwinuko tengeneza matungazi (terrace) ili kuzuia mmomonyoko. - Udongo
Udongo unaofaa ni wenye rutuba, mboji nyingi na unaopitisha maji kwa kirahisi. Vilevile usiwe na historia ya magonjwa na wadudu waharibifu. - Chanzo cha Maji
Eneo la bustani liwe karibu na maji ya kudumu. Maji yasiwe na chumvi nyingi kwani huathiri ukuaji wa mimea. - Kitalu
Kitalu kisiwekwe mahali palipo na kivuli kingi kwa kuwa husababisha mimea kuwa dhaifu. - Kuzuia Upepo Mkali
Eneo la bustani lipandwe miti mipakani ili kuzuia upepo mkali. Upepo mkali huharibu mimea kwa kuvunja vunja majani na matawi na husafirisha vimelea vya magonjwa na wadudu. Pia hufanya udongo wa juu kukauka haraka na kuleta mmomonyoko.
KUTAYARISHA MATUTA
Ni muhimu udongo utifuliwe vizuri. Mabonge makubwa yavunjwe vunjwe ili Kurahisisha upitaji wa maji na hewa katika udongo. Matuta huinuliwa kidogo toka usawa wa ardhi ili kuzuia maji yasituame. Matuta haya yasitumike wakati wa kiangazi. Wakati wa kiangazi tengeneza matuta yaliyodidimia kidogo.
KUMWAGILIA MAJIHakikisha udongo una unyevu wa kutosha kwa kumwagilia siku moja kabla ya kuotesha mbegu. Pia baada ya kupanda mwagilia kitalu au shamba maji ya kutosha. Maji mengi husababisha mbegu au miche kuoza.
KUPANDA
Kina cha kupanda kitategemea ukubwa wa mbegu. Mbegu ndogo hupandwa katika kina kifupi zaidi kuliko mbegu kubwa. Upandaji wa baadhi ya mbegu unaweza kufanyika kila wiki ili kuweza kupata mboga mfululizo.
KUOTESHA MBEGU KWENYE KITALU
Baadhi ya mbegu za mboga huoteshwa kwanza kwenye kitalu na baadaye miche huhamishiwa shambani. Mbegu hizini kama vile za bilinganya, kabichi, nyanya, pilipili hoho na vitunguu. Kitalu kwa ajili ya kuotesha mbegu hakina budi kitayarishwe wiki moj a kabla ya kusia mbegu. Wakati wa kutayarisha kitalu, ardhi ikatuliwe katika kina cha kutosha sentimita 30 kwenda chini. Ili kuongeza mtuba ya udongo mbolea za asili kama vile samadi, takataka na mbolea vunde zilizooza vizuri ziwekwe kabla ya kusia mbegu.
KUTUMIA MBEGU BORA
Tumia mbegu bora zilizohifadhiwa kwenye dawa. Mbegu bora ni zile ambazo zimekomaa na kukauka vizuri, hazikushambuliwa na wadudu wala magonjwa na ambazo zina uwezo wa kuota vizuri. Inashauriwa kutumia mbegu zilizothibitishwa kitaalamu.
KUWEKA KIVULI NA MATANDAZO
Utandazaji wa majani makavu na uwekaj i wa kivuli ni muhimu ili kuzuia jua linaloweza kunyausha miche. Matandazo pia husaidia kuhifadhi unyevu, joto la udongo na hupunguza palizi ya mara kwa mara. Kivuli kiruhusu mwanga wa kutosha na kiondolewe kidogo kidogo kadiri mimea inavyokua.
Uwekaji wa kivuli ni muhimu ili kuzuia jua kali
KUITAYARISHA MICHE KABLA YA KUPANDIKIZA:
Wiki mbili kabla ya kuihamisha miche toka kitaluni, unashauriwa kupunguza kumwagilia ili kuizoesha iweze kustahimili hali ya sehemu inapohamishiwa. Mwagilia kitalu siku moja kabla ya kung'oa miche ili kurahisisha ung'oaji na kuepuka kuikata mizizi. Pia shamba kwa ajili ya kuhamishia miche limwagiliwe siku moja kabla ya kupandikiza ili kuloanisha udongo.
MATUMIZI YA MBOLEA
- Mboji, Samadi na Mbolea Vunde
Mboga hustawi, vizuri sana katika udongo wenye mbolea hizo. Hivyo ni vema mbolea hizo ziwekwe shambani kabla ya kupanda au kupandikiza. Kiasi kinachotakiwa ni ndoo moja kwa tuta lenye upana na urefu wa mita moja. - Mbolea za Viwandani
Mbolea za viwandani zimegawanyika katika makundi makuu matatu, nayo ni mbolea za chumvichumvi, chokaa na kijivu,
(a) Mbolea za Chumvichumvi
Mbolea hizi hujulikana kama mbolea za kukuzia na huwekwa shambani baada ya mimea kuota. Zina virutubisho vingi vya Naitrojeni ambavyo huifanya mimea kukua haraka.Pia zinahusika na utengenezaji wa kijani kibichi kwenye mmea.
Nchini Tanzania mbolea za chumvichumvi zinazotumika zaidi ni:-- Sulphate ofAmmonia (S/A) 21% N- Calcium Ammonium Nitrate (CAN) 26 % N- Urea 46% N.- Mbolea ya mchanganyiko N.P.K. 25.5.5 na 20.10.10
(b) Mbolea za Chokaa:Hizi ni mbolea zinazotumika kupandia mbegu au miche. Husaidia uotaji mzuri wa mimea, huimarisha mizizi, na hutumika katika utengenezaji wa chakula na mbegu kwenye tunda. Vilevile huhusika na usafirishaji wa nguvu kwenye mmea na hufanya mazao kukomaa haraka. Mbolea hizi huwekwa shambani wakati wa kupanda.Aina ya mbolea za chokaa zinazotumika hapa nchini ni Triple Super Phosphate (TSP) 46% P2O5. Vilevile unaweza kutumia N.P.K 6.20.18 kwa kupandia.
(c) Mboleaza Kijivu (Potashi):Potashi ni kirutubisho kinachosaidia mimea katika utengenezaji wa protini na wanga. Kadhalika huhusika na utumiaji wa madini muhimu kwa maisha ya mimea. Mbolea hii pia huwezesha matunda kukomaaa, kuiva haraka, na kutengeneza mbegu bora. Vilevile husaidia ongezeko la maji kwenye mmea na kuufanya ustahimili magonjwa, ukame, baridi na hali ya udongo wenye alkalini nyingi.Mbolea za Potashi zinazotumika ni:-- Muriate ofPotash 48 - 60% K2O- Sulphate ofPotash 48 - 50% K2O
KUBADILISHA MAZAO SHAMBANI
Kubadilisha mazao shambani ni utaratibu wa kuachs kupanda mfululizo aina ileile ya zao katika eneo hilo hilo. Iwapo eneo ni kubwa, bustani igawanywe katika sehemn tatu au nne ili kuepuka kupanda mfolulizo aina ileile ya zao. Katika kila sehemu panda aina nyingine ya mazao na ya familia tofauti kila baada ya kuvuna.
Baada ya kuvuna; mazao ya sehemu ya kwanza yapandwe katika sehemu ya pili, ya pili katika sehemu ya tatu na ya tatu yapandwe katika sehemu ya nne na yale ya nne yapandwe katika sehemu ya kwanza.
Kubadilisha mazao shambani huzuia ongezeko la wadudu na magonjwa yanayoshambulia jamii moja ya zao. Vilevile huhifadhi rutuba ya udongo na huzuia uotaji wa magugu. Utaratibu huu pia humwezesha mkulima kuweka kiasi cha mbolea kinachotakiwa shambani. Ufuatao ni mfano wa kubadilisha mazao.
MFANO WA KUDADILISKA MAZAO
Jamii ya Nyanya
- Bilinganya
- Nyanya
- Pilipili
- Viazi Mviringo
Jamii ya Matango
- Matango
- Maboga
- Matikiti Maji
Mimea ya Mizizi
- Karoti
- Vitunguu
MATUMIZI YA MADAWA
Ni muhimu kutumia madawa ili kukinga mimea kutokana na athari za wadudu na magonjwa. Hata hivyo madawa yatumike pale inapobidi kwani ni ghali na yana madhara kwa mazingira na watu.
Mambo yafuatayo yanatakiwa kuzingatiwa wakati wa kutumia madawa. Hakikisha unatumia dawa inayoshauriwa na wataalamu.
- Soma kwa uangalifu maelezo yanayoambatana na dawa toka kwa watengenezaji, kabla ya kutumia na yasikiukwe. Hii itakusaidia kujua vifaa, kiasi na jinsi ya kutumia. Madawa ni hatari kwa binadamu na wanyama kama yatatumika isivyopasa.
- Wakati wa kuchanganya na kunyunyizia dawa, vaa nguonavifaavyakinga. Vifaa hivi ni kofia, glovus, viatu (gumboots), kitambaa cha kufunika mdomo na pua, miwani na ovaroli.
- Tumia maji safi kuchanganya dawa.
- Epuka kuvuta hewa yenye dawa. Wakati wa kunyunyizia dawa usielekee upepo unakotoka bali elekea upepo unakoenda.
- Usile wala kuvuta wakati wa kuchanganya au kunyunyizia dawa.
- Baada ya kunyunyizia dawa osha mwili kwa sabuni na maji mengi na safi.
- Maji yanayotumika kusafishia bomba yasimwagwe katika maji yaliyotuama au yanayotembea kwani yanaweza kuleta madhara sehemu nyingine. Maji yamwagwe kwenye shimo na kufukiwa.
- Nguo na vifaa vingine vilivyotumika zifuliwe mara moja kwa sabuni na maji safi.
- Osha vizuri mikono kwa sabuni kabla ya kula, kunywa chochote au kuvuta sigara.
- Makopo au chupa zilizokuwa na dawa zisitumike bali ziharibiwe na kufukiwa.
- Hifadhi madawa mahali salama na pasipofikiwa na watoto kwa urahisi. Dawa ziachwe katika makasha., chupa au makopo yake zilimokuwemo. Hata siku moja madawa ya mimea yasitumike kwa kutibu binadamu.
- Endapo kutakuwepo na matatizo yeyote katika matumizi muone Mtaalamu kwa ushauri.
- Iwapo sehemu ya kutolea dawa itaziba, tumia nyasi au kijiti kuzibua. Kamwe usizibue kwa mdomo.
UTUMIAJI WA MBOGA BAADA YA KUNYUNYIZIA DAWA
Mboga zisitumike mara baada ya kunyunyizia dawa. Kila dawa ina siku zake za salama, lakini kwa madawa yaliyo mengi ni siku 14 toka kunyunyizia. Hivyo ni muhimu kusoma maelezo yanayoambatana na dawa. Ikiwa mboga zitatumika kabla ya muda huo huleta madhara kwa mlaji kama vile magonjwa ya kansa. Vilevile mbegu zilizowekwa dawa zisitumike kwa kula.
MAGONJWA NA WADUDU WAHARIBIFU
Ni muhimu kukinga mimea dhidi ya wadudu na magonjwa ili kupata mazao mengi na bora. Zifuatazo ni njia mbalimbali zinazoweza kutumika katika kuzuia magonjwa na wadudu waharibifu.
UTHIBITI SANGO
Njia hii hutumia mbinu zifuatazo
- Kupanda mbegu bora;
- Usafi wa bustani ambao ni pamoja na kuchoma takataka na kuondoa magugu yanayoweza kutunza wadudu na magonjwa.
- Kuchanganya mazao
- Kutumia samadi na mboji
- Kupanda kwa nafasi
- Kutumia aina ya mbegu zinazovumilia au kustahimili mashambulizi ya magonjwa na wadudu
UDHIBITI WA KITEKNOLOJIA
Kutumia aina mbalimbali za madawa
- Kutumia mimea inayoua wadudu, kama vile muarobaini, pilipili kali, aina fulani ya maua, marejea, tumbaku, wadudu kama vile walawangi, manyigu na mbawakau.
VIFAA VYA BUSTANI
Ili kuboresha kilimo cha mboga ni muhimu kuwa na jembe, kamba, reld, uma wa bustani, ndoo ya kumwagilia maji, bomba la kunyunyizia dawa, toroli, panga, kwanja, sepetu, beleshi karai na kadhalika.
Comments
Post a Comment