Skip to main content

Uandaaji na Uoteshaji wa Mbegu za Mitiki

Utangulizi
Mbegu za mitiki zinapatikana Tanzania Tree Seed Agency wako Msamvu Morogoro.Kilo moja ya mbegu za mitiki inatosha kuotesha kwenye shamba la hekta moja, ambayo ni wastani wa miti 1500

Matayarisho:
  1. Ganda la nje la mbengu ya mtiki ni gumu sana na lina sumu mbaya.Unatakiwa uloweke mbegu ya mitiki kwa masaa 72, na kila baada ya masaa 12 unatakiwa ubadilishe maji kwa kumwaga maji ya zamani na kuweka maji mapya.
  2. Baada ya masaa 72 anika mbegu zako juani kwa masaa 12 (zianikike ktk bati).
  3. Tengeneza kitalu, weka mbolea ya wanyama au mboji, kisha panda mbegu zako kwenye kitalu.
  4. Mwangilia maji kila siku asubuhi na jioni, mbegu zitaanza kuota baada ya siku 10 hadi 20.
  5. Miche ikifikia urefu wa futi moja, unaweza sasa kuiotesha kwenye shamba lako ulilotayarisha kwa ajili ya kuotesha miti.
  6. Kabla ya kung’'oa miche hakikisha unamwaga maji mengi, ili mizizi isikatike sana, kisha chukua kisu chenye makali ya kutosha na kata ncha ya juu ya mti na ondoa majani, hii inasaidia mti kuchipuka upya hasa eneo ambalo halina maji mengi.
  7. Otesha miti futi 6x6 mitiki inaposongamana, hurefuka haraka ikikimbilia jua angani, hivyo kwa vipimo hivyo miti yako itakuwa mirefu sana na iliyonyooka, baadaye unaweza kuipunguza na kuuza fito za kujengea.
  8. Ili upate mbao bora hakikisha unaondoa matawi yanayochipuka pembeni hadi mti ufike zaidi ya futi 10 kwani ndiyo yanafanya mbao kuwa na mabaka (vidonda)
Bei ya Kilogram Moja (Kg 1)  ya mbegu za Mitiki ni TZS 12,500
Tanzania Tree Seed Agency wapo Dodoma Rd, mkoa wa Morogoro kama unaenda Kihonda. Kituo kinaitwa "Misitu" au "Vybes"

Comments

Popular posts from this blog

Utengenezaji wa Chakula cha Kuku wa Nyama (Bloilers)

Utangulizi Kuku wa nyama wana mahitaji yafuatayo ya viinilishe katika chakula ili wakue vizuri Viinilisha vya wanga 60-65%   Protini 30-35%   Madini 2-8% Chakula cha Vifaranga Chakula hiki hutengenezwa katika namna ya kumsaidia kifaranga aweze kumeza vizuri na hivyo hakitakiwi kuwa katika punje punje. Hata kama utanunua pumba, ni vema kuzipitisha kwenye mashine ili ziwe laini zaidi.  Mahitaji (kgs)  Unga wa dona wa nafaka kama mahindi au mtama 40  Pumba za mtama au mahindi au uwele 27  Mashudu ya alizeti au ufuta, au pamba au karanga n.k. 20  Unga wa mifupa au chokaa ya kuku (DCP) 2.25  Dagaa au mabaki ya samaki (sangara fish meal) 10  Chumvi ya jikoni 0.5  Virutubisho (Broiler premix) 0.25  Jumla utapata 100Kg. Chakula cha kukuzia – growers mash Mahitaji (Kg) Mahindi yaliyobarazwa au mtama au uwele 25   Pumba za mtama au mahindi au uwele 44   Mashudu ya alizeti au ufuta, au pamba au karanga n.k. 17   Unga wa mifupa a...

Aina Za Miti ya Minazi

AINA ZA MINAZI Inafaa mkulima kufahamu kuna aina mbali mbali za minazi na ina mahitaji tofauti katika ukuaji. Ujuzi huu utamsaidia katika kuchagua aina ya minazi itakayofaa kwa eneo lake na kwa kiwango chake cha utunzaji. KUNA AINA TATU ZA MINAZI Minazi mirefu ya asili Minazi mifupi Minazi chotara MINAZI MIREFU YA ASILI (EAT) Minazi ya aina hii ndiyo inayojulikana na wakulima wengi kwa vile ni ya kiasili na imezoea mazingira yetu. Minazi hii huchukua miaka 6-8 tangu kupandikizwa hadi kuzaa. Minazi ya aina hii huvumilia ukame na inao uwezo wa kutoa wastani wa nazi 40 kwa mwaka. Nazi huwa kubwa na zenye nyama nene ambayo inafaa kwa kupikia na kukamua mafuta. Minazi hii huishi kad ya miaka 60 na kuendelea. Nchini Tanzania, minazi hii hustawi vyema ukanda wa pwani sehemu zisizo na mawe na ambazo hazituamishi maji. MINAZI MIFUPI (DWARF) Minazi ya aina hii huzaa mapema kuanzia miaka miwili. Huzaa nazi nyingi na ndogo. Nazi hizi huwa na nyama nyembamba hivyo hutumika kwa nnadafu. Minazi huhit...

Kilimo Bora cha Migomba

UTANGULIZI Hapa Tanzania kilimo cha migomba kimekuwepo Kwa miaka mingi. Kilimo hiki ni maarufu sana kwa sababu zao la ndizi limekuwa likitumika kama chakula kikuu kwa baadhi ya mikoa kama vile Kagera, Kilimanjaro na Mbeya na hivyo kulifanya muhimu, kufuatia mazao ya mahindi, mpunga, mtama, muhogo,viazi na mazao ya jamii ya kunde kama vile maharage. Zao la ndizi linaweza kuwa moja kati ya mazao ya biashara iwapo litazalishwa kwa kufuata kanuni bora za uzalishaji wa zao hilo, ikwa ni pamoja na kupanda aina bora ya migomba inayozaa ndizi zinazotambulika katika masoko ya kimataifa. ASILI YA MIGOMBA Asili ya migomba ni nchi za Malaysia na India ambazo ziko Kusini Mashariki mwa Asia. Migomba inayolimwa sasa imetokana na migomba ijulikanayo kama Musa balbisiana ambayo asili yake ni India, na Musa acuminata ambayo asili yake ni Malaysia. Kutoka Malaysia na India migomba ilifika Afrika Mashariki katika karne ya tano MAENEO YANAYOLIMWA MIGOMBA NCHINI Nchini Tanzania mikoa inayoshughulika na kili...