Unaweza kutumia mimea fulani kupunguza idadi ya wadudu waharibifu shambani mwako. Panda mimea ambayo huepukwa na wadudu waharibifu karibu na mimea inayohitaji kulindwa. Kwa mfano, minyoo fulani ambayo hula na kudhoofisha mizizi ya mimea mingi haiwezi kukaribia mimea ya matageta. Na vipepeo fulani ambao huharibu kabichi hawakaribii kabichi zilizopandwa karibu na mimea ya rosemary, sage, au thyme.Hata hivyo, tahadhari hii yafaa: Mimea fulani huwavutia wadudu waharibifu.
JINA | TIBA | UTUMIAJI |
Mnyaa | Kuua Mchwa | Matone 10 ya mnyaa + maji lita moja. Koroga. Nyunyuzia/ Pulizia kwenye mchwa |
Utupa | Wadudu wanaoshambulia mboga | Twanga kiganja kimoja cha majani. Loweka kwenye lita 1 ya maji kwa masaa 24. Chuja. Ongeza 1/8 ya kipande cha mche wa sabuni. Pulizia kwenye mboga |
Muarobaini – Majani | Wadudu wa mboga | Ponda ganja mkona 1 wa majani. Changanya kwenye lita 1 ya maji. Loweka kwa siku mbili , halafu ongeza sabuni 1/8 ya kipande mche. Nyunyuzia kwenye mboga. |
Muarobaini - Mbegu | Wadudu wanaoshambulia mboga | Twanga mbegu kilo 5 (kisado kimajo). Loweka kwenye maji lita 15 kwa masaa 24. Chuja na pulizia/ nyunyuzia kwenye mboga |
Papai | Kuua mchwa Ponda majani laini ya mpapai. | Ongeza lita 1 ya maji. Chuja na pulizia/ nyunyuzia kwenye mchwa |
Bangi Mwitu | Kuhifadhi vyakula vya nafaka (food grains) | Sambaza halafu weka gunia juu yake. Endelea hivyo hivyo. |
Mkojo wa n’gombe | Kuua mchwa/ wadudu wa mboga | Uache mkojo kwa siku 10 –14. Kwa kila lita 1 ya mkojo ongeza lita 2 za maji na 1/8 sabuni ya mche. Nyunyuzia kwenye mchwa au mboga |
Mnanaa (mbarika mwitu) | Kuua wadudu wanaoshambulia mboga | Gram 100 mbegu + lita 1 maji + 1/8 sabuni mche. Pulizia/ nyunyizia kwenye mboga |
Kitunguu saumu | Kuua wadudu wanaoshambulia mboga | Gram 100 (3-4) twanga. Ongezea lita 1 ya maji. Acha kwa saa 24. Chuja na ongeza 1/8 ya kipande cha mche wa sabuni. Pulizia/ Nyunyuzia kwenye wadudu |
Pilipili Kali | Kuua wadudu kwenye mboga | Changanya vijiko 3 vya chakula na lita 1 ya maji. Acha kwa saa 12. Ongezea 1/8 ya kipande cha sabuni mche. Nyunyizia kwenye mimea |
Mashona nguo | Kuua wadudu | Chemsha mbegu kikombe 1 na lita 1 ya maji kwa dakika 10 au loweka siku moja na ongezea 1/8 ya kipande cha sabuni mche. Nyunyuzia kwenye mboga |
Muarobaini Kideri | (New Castle disease) | Twanga majani 1kg, ongeza maji lita 1. Wanyweshe kuku asubui. Fanya hivi kila mwezi |
Majivu | Kuua wadudu mafuta (aphids) | Nyunyizia majivu kwenye wadudu wanaoshambulia mboga |
Majivu | Kuhifadhi mazao | Changanya majivu + pilipili kichaa + Cyprus. Sambaza kwenye gunia halafu weka gunia juu yake. Endelea hivyo hivyo. |
Marejea | Mbolea | Panda shambani na baadaye limia chini ardhini |
naomba kuuliza mbolea ya kuku inakaa baada ya muda gani kabla ya kupanda mchicha? maana niliweka mbolea saatano nililushia mbegu saa kumi na moja zikaungua naomba Elimu
ReplyDeleteMbolea ya kuku inatakiwa kuwekwa shambani endapo itakuwa full decomposed (imeiva vizuri).Na inatakiwa ikae angalau wiki moja shambani kabla ya kusia au kupanda mazao
DeleteDawa gani za asili za kuua wadudu pilipili kichaa zangu zina waiki mbili sasa
ReplyDelete