Skip to main content

Ufugaji wa Samaki - Kambale



Utangulizi
Kambale (Ietalurus Punetaus), ni aiana ya samaki ambao wana majina mengi kulingana na eneo na jamii husika. Samaki hawa unaweza kusikia wakitajwa kwa majina mengine kama vile, kambale channel, koleo, samaki kidevu n.k.
  
kambaleAsili ya samaki hawa ni Amerika ya Kaskazini. Samaki hawa hukua kwa haraka sana, na kuwa na uzito mkubwa. Aina hii ya samaki hupendwa na watu wengi kwa kuwa nyama yake ina ladha nzuri na ni laini sana.
Samaki hawa huzaliana vizuri zaidi wanapokuwa mtoni au sehemu ambayo wanapata tope. Mfugaji anapokusudia kufuga aina hii ya samaki kibiashara, ni lazima kusakafia bwawa ili kuepuka uharibifu unaoweza kusababishwa na samaki hawa.

Umbile
Samaki aina ya kambale wana umbo refu, mpana kuanzia shingoni, ingawa kichwa ni kidogo, na upande wa mkia ni mwembamba. Samaki hawa wana rangi ya kijivu na wengine nyeusi.

Kulisha
Unaweza kulisha kambale kwa kutumia unga wa samaki, maharagwe yaliyosagwa, mahindi, mchele pumba, ngano na bidhaa nyingine. Unaweza kujenga mfumo ambao utawawezesha samaki hawa kupata aina mbalimbali za wadudu, pamoja na majani, ili kusaidia wapate mlo kamili.

Ukuaji na uvunaji
Aina hii ya samaki, wakitunzwa vizuri, wanaweza kukua kwa haraka na kuwa na uzito mzuri unaoweza kumpatia mfugaji faida nzuri. Unaweza kuanza kuvuna kambale baada ya miezi sita tangu walipopandikizwa kwenye bwawa.

Fikiria soko la samaki kabla ya kuanza kuzalisha
Wafugaji walio wengi, wamekuwa wakianzisha miradi ya ufugaji wa samaki kwa kufuata mkumbo bila kutambua kwanza soko watakalozalishia samaki hao. Jambo hili huwafanya wafugaji kuwa na kipato kidogo tofauti na nguvu waliyotumia kuzalisha.

Inapofikia wakati wa kuvuna samaki, kiasi kikubwa huuzwa papo hapo bila kufika kwenye soko halisi, jambo linalosababisha kipato kuwa duni. Ni vyema mfugaji akawa na soko maalumu ambalo atazalishia. Unaweza kuzalisha kwa ajili ya shule, hospitali, vyuo, au taasisi yoyote. Halikadhalika jamii inayokuzunguka na taasisi nyinginezo.

Ni vizuri kuzingatia yafuatayo kabla ya kuanza uzalishaji wa samaki 
  • Fahamu ni aina gani ya samaki inayopendwa zaidi katika eneo ulipo.
  • Samaki wanaopendwa wanatakiwa wawe na ukubwa gani.
  • Kiasi cha samaki kinachohitajika katika soko ulipo.
  • Ni kipindi gani ni kizuri kwa uvunaji wa samaki.
  • Ni wakati gani mzuri wa kuuza samaki.
  • Je, katika eneo lako kuna mfugaji mwingine anaezalisha samaki kwa ajili ya soko hilo?.
  • Bei ya aina ya samaki unaozalisha ikoje?
Wasikilize wateja
Wakati wote mfugaji anapouza samaki, ni lazima kusikiliza kwa umakini, wateja wako wanasemaje.
  • Je, wanapendelea samaki unaouza.
  • Je, samaki wako ni wadogo sana au ni wakubwa sana.
  • Wakija kununua wananunua kwa kiasi gani, kikubwa au kidogo.
  • Je, wanapendelea uzalishe zaidi?
  • Je, kuna wafanyabiashara wanataka uzalishe zaidi ili nao wanunue.
  • Wanataka samaki wawe kwenye ubora gani.
  • Wanaridhika na bei unayowauzia.
Fuata haya kwa ufanisi wa soko la samaki
  • Hakikisha samaki wako katika hali ya usafi na vyombo salama unapovua tayari kwa kupeleka sokoni.
  • Samaki ni bidhaa inayoharibika kwa haraka, hivyo hakikisha unawapeleka sokoni mara tu baada ya kuwavua.
  • Hakikisha gharama za usafiri, utunzaji na uhifadhi, zinalipwa kutokana na bei ya soko.
  • Kumbuka gharama za uhifadhi wa bidhaa inayoharibika haraka kama samaki ni kubwa, hivyo vua kwa awamu kulingana na mahitaji.
  • Unaweza kuongeza thamani ya samaki kwa kufanya mambo ya msingi yanayohitajika kwenye uandaaji wa samaki, kama vile kuparua na kutumbua.
  • Unaweza kuwasafisha, na pia kuwakaanga kulingana na soko husika.
Kwa kuzingatia mambo hayo machache, mfugaji anaweza kufanya maamuzi sahihi kabla ya kuwekeza kwenye mradi wa ufugaji wa samaki. Pia ni muhimu kuzingatia mahitaji muhimu ya ufugaji wa samaki, ili kuepuka gharama zisizo za lazima.

Tengeneza chakula cha samaki mwenyewe
Mfugaji anaweza kupunguza gaharama za kununua chakula kwa ajili ya samaki, kwa kutengeneza chakula mwenyewe kwa kutumia malighafi ulizo nazo katika eneo lako. Tumia resheni rahisi ambayo itakupatia chakula cha kutosha na kwa gharama nafuu.
 Mahitaji
  • Pumba ya mahindi sadolini 1.
  • Pumba ya ngano au mpunga sadolini 1.
  • Dagaa sadolini 1.
  • Kilo moja ya soya.
  • Robo kilo ya mashudu ya pamba au alizeti
Namna ya kuandaa
  • Changanya malighafi hizo kwa pamoja.
  • Saga hadi zilainike.
  • Kanda kama vile unga wa kutengenezea chapati.
  • Weka kwenye mashine ya kusaga nyama au kutengenezea tambi.
  • Anika kwenye jua la wastani.
  • Baada ya kukauka, vunja vunja kwenye vipande vidogo vidogo hasa kwa kuzingatia umri wa samaki unaokusudia kuwalisha.
  • Tumia lishe hiyo kwa samaki mara tatu kwa siku.



Comments

Popular posts from this blog

How to Save Watermelon Seeds for Planting on Small Garden

Watermelon seeds from this year's garden can be planted next year. Seeds saved from the fruits of your garden's non-hybrid watermelon plants (Citrullus lanatus) can grow into new plants the following season. Different varieties of watermelons can cross-pollinate, which results in seedlings that aren't exactly like their parent plants. So grow only one watermelon variety in the garden if you want to save the seeds. The large seeds separate from the fruits easily, but they require some preparation to store well. Properly saved watermelon seeds can remain viable up to four years. Cut open a ripe watermelon. Scoop the seeds from the melon's flesh, and place them in a strainer. Rinse the seeds with warm tap water, removing most of the pulp. Add one drop of liquid dish soap, and wash the seeds gently to remove the remaining watermelon juice. Rinse the seeds thoroughly with only water. Spread the seeds on a sheet of wax paper. Dry the seeds for one week, turning them once each...

Ufugaji wa Samaki na Aina Zake

  Aina za ufugaji Zifuatazo ni aina/level za ufugaji ambazo mkulima anaweza kufanya kulingana na malengo na uwezo wake: 1. Huria (Extensive farming) Idadi ya samaki wanaopandikizwa: samaki 2-3 kwa mita ya mraba Samaki hutegemea chakula cha asili (mimea ya majini-phytoplankton, wadudu/viumbe vidogo vya majini-zooplankton) Hauitaji ubadilishaji wa maji Hauihitaji huduma ya ziada ya hewa   2. Kati ya huria na nusu shadidi (Modified extensive: Samaki, 4-7 kwa mita ya mraba Chakula cha asili na chakula cha ziada huitajika Maji hubadilishwa sentimenta 10-20 kila baada ya 3-4weeks kulingana na hali ya samaki na maji yako Huduma ya hewa ya ziada sio ya ulazima 3. Nusu shadidi (Semi-intensive) Idadi ya samaki kwa mita ya mraba ni 10-25 C hakula cha asili na cha ziada Huduma ya hewa ya ziada lazima Maji hubadilishwa kila siku au kila baada ya siku kadhaa (15-25 cm) 4. Shadidi (Intensive) Idadi ya samaki ni zaidi ya 25 kwa mita ya mraba 100% chakula cha kutengenezwa Maji ni kuingia na ku...

Kilimo Bora cha Alizeti - Uzalishaji, Uangalizi, Uvunaji na Uhifadhi

Utangulizi Alizeti hulimwa kwa wingi katika mikoa ya Shinyanga, Singida, Dodoma, Iringa, Tabora, Morogoro, Ruvuma, Mbeya, Arusha, Manyara, na RukwaZao hili hulimwa kwa ajili ya chakula na biashara. Mambo muhimu ya kuzingatia wakati wa uzalishaji Kuchagua aina bora ya mbegu Chagua aina bora ya mbegu inayovumilia magonjwa, wadudu, inayotoa mazao mengi na kiwango kikubwa cha mafuta. Vilevile chagua aina ya mbegu ambayo hukomaa kwa wakati mmoja ili kurahisisha uvunaji. Kuweka mbolea Rutubisha udongo kwa kutumia mbolea za mboji na samadi ili kupata mazao mengi na bora. Kudhibiti wadudu na magonjwa Alizeti hushambuliwa na magonjwa ya majani, mizizi na masuke ambayo husababisha upungufu wa mavunoHivyo ni muhimu kuyadhibiti ili kupata mavuno mengi na boraPia ndege hupunguza mavuno kwa kiasi cha asilimia 50 au zaidiNjia ya kudhibiti ndege ni kwa kuwafukuza na kupanda mbegu zinazokomaa mapema. Maandalizi kabla ya kuvuna;  Ukaguzi  Kagua shamba kuona kama alizeti imekomaaAlizeti hukomaa ...