Skip to main content

Ufugaji wa Samaki na Aina Zake


 Aina za ufugaji
Zifuatazo ni aina/level za ufugaji ambazo mkulima anaweza kufanya kulingana na malengo na uwezo wake:

1. Huria (Extensive farming)
  • Idadi ya samaki wanaopandikizwa: samaki 2-3 kwa mita ya mraba
  • Samaki hutegemea chakula cha asili (mimea ya majini-phytoplankton, wadudu/viumbe vidogo vya majini-zooplankton)
  • Hauitaji ubadilishaji wa maji
  • Hauihitaji huduma ya ziada ya hewa
 2. Kati ya huria na nusu shadidi (Modified extensive:
  • Samaki, 4-7 kwa mita ya mraba
  • Chakula cha asili na chakula cha ziada huitajika
  • Maji hubadilishwa sentimenta 10-20 kila baada ya 3-4weeks kulingana na hali ya samaki na maji yako
  • Huduma ya hewa ya ziada sio ya ulazima
3. Nusu shadidi (Semi-intensive)
  • Idadi ya samaki kwa mita ya mraba ni 10-25
  • Chakula cha asili na cha ziada
  • Huduma ya hewa ya ziada lazima
  • Maji hubadilishwa kila siku au kila baada ya siku kadhaa (15-25 cm)
4. Shadidi (Intensive)
  • Idadi ya samaki ni zaidi ya 25 kwa mita ya mraba
  • 100% chakula cha kutengenezwa
  • Maji ni kuingia na kutoka
  • Hewa ya ziada masaa yote
  • Eneo linalotumika ni dogo ukilinganisha na mifumo mingine
Miundombinu ya ufugaji
Samaki wanaweza kufugwa katika miundombinu mbalimbali kama ifuatayo 
Bwawa
  • Kina 0.8-1.5m
  • Ukubwa 100 mita za mraba- 1ha
Matanki
  • Umbo-mstatili au mviringo nk
  • Kina 1-1.5m
  • Kipenyo kwa lile la mduara 3-10m
  • Ukubwa kwa la mstatili inategemea na uwezo lakini lisiwe kubwa ili kuhimili nguvu ya maji
Materials: Plastic, cement, chuma nk
NB: Simtank linafaa( Faida inapatikana kama utalitumia kwa intensive system)

Vizimba (Fish cages)
  • Huwekwa katika maji ya asili kama vile ziwani, baharini au katika bwawa. Vipo vinavyoundwa kwa local materials kama mianzi na vipo vya aluminium.
Eneo linalofaa kwa ufugaji
Baadhi ya maeneo yanayofaa ni yale mashamba ya mpunga, na maeneo yaliyo karibu na vyanzo vya maji. Zifuatazo ni sifa za maeneo yanayofaa:
  1. Udongo: Mfinyanzi husaidia kupunguza gharama za ujenzi wa bwawa na maji kwakuwa linaweza kutuamisha maji na kuruhusu maji yasipotee. Likiwa la kichanga bwawa ni lazima lijengewe au kuwekwa nylon sheet ili kuzuia upotevu wa maji. Unaweza ukahamisha udongo wa mfinyanzi kutoka sehemu moja hadi nyingine ili kuzuia upotevu wa maji (muone mtaalamu kwa ushauri zaidi juu ya mbinu ya kuhamisha udongo).
  2. Chanzo cha maji ya uhakikaEneo liwe na maji ya uhakika. Vyanzo vya maji ni kama vile mito, bahai, maziwa, chem chem., kisima, maji ya dawasco na mvua. Maji yasiwe na kemikali hatarishi kwa viumbe.
  3. Miundombinu ya barabara: Inasaidia kwa ajili ya usafirishaji wa bidhaa na samaki wakati wa kuvuna.
  4. Eneo lisiwe na historia ya mafuriko ili kuzuia athari za mafuriko kwa miundombinu yako. Utatumia gharama nyingi katika kuimarisha miundombinu yako.Jamii/aina ya samaki
  5. Eneo lenye mwinuko wa wastani husaidia katika ujenzi wa bwawa.
  6. Miundombinu ya umeme ni sifa ya ziada hususan kwa mkulima wa kati na wajuu kwa ajili ya kutumika katika kuendesha visambaza hewa.
  7. Ulinzi ni muhimu
Angalizo: Aina ya eneo lako ndilo linaweza kukufanya uchague muundombinu gani wa kufugia utumie

Aina ya samaki unaoweza kufuga Tanzania kwa sasa
Maji baridi
Sato/Perege, Kambale, Kambamiti wa maji baridi na Trout 
maeneo ya baridi kama vile 
  • Iringa
  • Kilimanjaro
  • Arusha
  • Mbeya
Maji bahari
Kambamiti wa maji bahari, mwatiko, chewa, kaa, chaza wa lulu

Upatikanaji wa Vifaranga vya samaki husika
Vyanzo vya vifaranga ni kutoka katika mito, bahari, maziwa na wale wa kuzalishwa katika vituo vya kuzalishia vifaranga.

Sato na Kambale. Kifaranga huuzwa Tsh. 50-100 kwa kifaranga.
Vituo vya serikali Utapata sato wa kike na kiume mixed sex). 
  • Kingolwira - Morogoro
  • Luhira - Songea
  • Mbegani - Bagamoyo . 
Vituo binafsi kama vile Faith aquaculture-Kibamba (DSM) (utapata monosex sato), Peramiho Songea (mixed sex). Monosex huuzwa Tsh. 200 kwa kifaranga, na mixed ni100 kwa kifaranga.

Trout
Mayai huagizwa toka Marekani, Israel
Kambamiti wa baharini Alphakrust “Mafia.

Chakula cha samaki
Chakula cha asili
Hurutubishwa kwa mbolea ya wanyama kama vile kuku, ngombe, mbuzi nk. Kwa kiwango cha 1000kg/ha. Mbolea ya kuku ni kali hivyo unaweza punguza ikawa 250-500kg/ha.

Chakula cha kutengeneza
Samaki huitaji protein ili akuwe na kila samaki ana mahitaji yake hivyo ni species specific. Formula zipo kwa wale wanaotaka kutengeneza. Tanzania hakuna kiwanda kinachotengeneza. Ingredients zake ni kama vile dagaa, pumba, soya, unga wa ngano, unga wa muhongo nk.

Uvunaji
Kwa kawaida ni miezi 4-6 amabapo unapata 250-400g kulingana na ulishaji wako. Kwa prawns ni miezi 3-6 wanafikia 30-50g ambayo ni ukubwa wa soko.

Tathmini ya uchumi
Perege/Sato Mfano:
Ukubwa wa bwawa ni 20m by 30m= 600 mita za mraba
Idadi ya samaki (7 kwa mita ya mraba) kwa monosex tu= 600 x 7=4200 fish
Uzito hadi kuvuna (4-6months)- 250g= 4200 x 250g= 1050kg (Nimesha convert gram to kg) Bei kwa kilo ni 6000-8000 kulingana na mahali= 6milion-8milion.

Gharama unazoweza kutumia
Ujenzi wa bwawa
Kuchimba kwa vibarua ni 500,000-600,000
Kuchimba kwa machine ni 1,000,000-1,500,000 kulinganana mahali ulipo

Kama udongo ni kichanga itabidi ujengee (kujengea ni gharama na inaweza ikafika3.5-4m kwa gharama zote kuanzia kuchimba hadi kujengea).

Chakula cha kutengeneza tani 1 inaweza kugharimu laki 7-9. Hapa ili uweze kuzalisha tani 1 ya samaki aina ya perege utahitaji tani 1-1.5 ya chakula.
Gharama ya vibarua 150,000-250,000 kwa mwezi.
Utakuwa na gharama ya chokaa kwa ajili ya kuua vidudu (100,000-200,000), mbolea kuzalisha chakula cha asili (gharama ni 50,000).



Comments

  1. thank you very much..binafsi sijawahi kufanya shughuli hii lakin imenivutia sana..nahitaji kujifunza zaid

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

Utengenezaji wa Chakula cha Kuku wa Nyama (Bloilers)

Utangulizi Kuku wa nyama wana mahitaji yafuatayo ya viinilishe katika chakula ili wakue vizuri Viinilisha vya wanga 60-65%   Protini 30-35%   Madini 2-8% Chakula cha Vifaranga Chakula hiki hutengenezwa katika namna ya kumsaidia kifaranga aweze kumeza vizuri na hivyo hakitakiwi kuwa katika punje punje. Hata kama utanunua pumba, ni vema kuzipitisha kwenye mashine ili ziwe laini zaidi.  Mahitaji (kgs)  Unga wa dona wa nafaka kama mahindi au mtama 40  Pumba za mtama au mahindi au uwele 27  Mashudu ya alizeti au ufuta, au pamba au karanga n.k. 20  Unga wa mifupa au chokaa ya kuku (DCP) 2.25  Dagaa au mabaki ya samaki (sangara fish meal) 10  Chumvi ya jikoni 0.5  Virutubisho (Broiler premix) 0.25  Jumla utapata 100Kg. Chakula cha kukuzia – growers mash Mahitaji (Kg) Mahindi yaliyobarazwa au mtama au uwele 25   Pumba za mtama au mahindi au uwele 44   Mashudu ya alizeti au ufuta, au pamba au karanga n.k. 17   Unga wa mifupa a...

Aina Za Miti ya Minazi

AINA ZA MINAZI Inafaa mkulima kufahamu kuna aina mbali mbali za minazi na ina mahitaji tofauti katika ukuaji. Ujuzi huu utamsaidia katika kuchagua aina ya minazi itakayofaa kwa eneo lake na kwa kiwango chake cha utunzaji. KUNA AINA TATU ZA MINAZI Minazi mirefu ya asili Minazi mifupi Minazi chotara MINAZI MIREFU YA ASILI (EAT) Minazi ya aina hii ndiyo inayojulikana na wakulima wengi kwa vile ni ya kiasili na imezoea mazingira yetu. Minazi hii huchukua miaka 6-8 tangu kupandikizwa hadi kuzaa. Minazi ya aina hii huvumilia ukame na inao uwezo wa kutoa wastani wa nazi 40 kwa mwaka. Nazi huwa kubwa na zenye nyama nene ambayo inafaa kwa kupikia na kukamua mafuta. Minazi hii huishi kad ya miaka 60 na kuendelea. Nchini Tanzania, minazi hii hustawi vyema ukanda wa pwani sehemu zisizo na mawe na ambazo hazituamishi maji. MINAZI MIFUPI (DWARF) Minazi ya aina hii huzaa mapema kuanzia miaka miwili. Huzaa nazi nyingi na ndogo. Nazi hizi huwa na nyama nyembamba hivyo hutumika kwa nnadafu. Minazi huhit...

Kilimo Bora cha Migomba

UTANGULIZI Hapa Tanzania kilimo cha migomba kimekuwepo Kwa miaka mingi. Kilimo hiki ni maarufu sana kwa sababu zao la ndizi limekuwa likitumika kama chakula kikuu kwa baadhi ya mikoa kama vile Kagera, Kilimanjaro na Mbeya na hivyo kulifanya muhimu, kufuatia mazao ya mahindi, mpunga, mtama, muhogo,viazi na mazao ya jamii ya kunde kama vile maharage. Zao la ndizi linaweza kuwa moja kati ya mazao ya biashara iwapo litazalishwa kwa kufuata kanuni bora za uzalishaji wa zao hilo, ikwa ni pamoja na kupanda aina bora ya migomba inayozaa ndizi zinazotambulika katika masoko ya kimataifa. ASILI YA MIGOMBA Asili ya migomba ni nchi za Malaysia na India ambazo ziko Kusini Mashariki mwa Asia. Migomba inayolimwa sasa imetokana na migomba ijulikanayo kama Musa balbisiana ambayo asili yake ni India, na Musa acuminata ambayo asili yake ni Malaysia. Kutoka Malaysia na India migomba ilifika Afrika Mashariki katika karne ya tano MAENEO YANAYOLIMWA MIGOMBA NCHINI Nchini Tanzania mikoa inayoshughulika na kili...