Utangulizi
Kuku wa nyama wana mahitaji yafuatayo ya viinilishe katika chakula ili wakue vizuri
- Viinilisha vya wanga 60-65%
- Protini 30-35%
- Madini 2-8%
Chakula hiki hutengenezwa katika namna ya kumsaidia kifaranga aweze kumeza vizuri na hivyo hakitakiwi kuwa katika punje punje. Hata kama utanunua pumba, ni vema kuzipitisha kwenye mashine ili ziwe laini zaidi.
Mahitaji (kgs)
- Unga wa dona wa nafaka kama mahindi au mtama 40
- Pumba za mtama au mahindi au uwele 27
- Mashudu ya alizeti au ufuta, au pamba au karanga n.k. 20
- Unga wa mifupa au chokaa ya kuku (DCP) 2.25
- Dagaa au mabaki ya samaki (sangara fish meal) 10
- Chumvi ya jikoni 0.5
- Virutubisho (Broiler premix) 0.25
- Jumla utapata 100Kg.
Chakula cha kukuzia – growers mash
Mahitaji (Kg)
- Mahindi yaliyobarazwa au mtama au uwele 25
- Pumba za mtama au mahindi au uwele 44
- Mashudu ya alizeti au ufuta, au pamba au karanga n.k. 17
- Unga wa mifupa au chokaa ya kuku (DCP) 3.25
- Dagaa au mabaki ya samaki (fish meal) 10
- Chumvi ya jikoni 0.25
- Virutubisho (Broiler premix) 0.5
- Jumla utapata 100Kg.
Chakula cha kumalizia kukuzia (Growers finishers)
Mahitaji (Kg)
- Mahindi yaliyobarazwa au mtama au uwele 31
- Pumba za mtama au mahindi au uwele 38
- Mashudu ya alizeti au ufuta, au pamba au karanga n.k. 18
- Unga wa mifupa au chokaa ya kuku (DCP) 2.25
- Dagaa au mabaki ya samaki (fish meal) 13
- Chumvi ya jikoni 0.5
- Virutubisho (Broiler premix) 0.25
- Jumla utapata 100Kg.
Ukishachanganya Kuna tatizo wakila hivo hivo mpk iwe mfumo wa peleti
ReplyDeletehttps://www.poultry1.com
ReplyDelete