Skip to main content

Kilimo Bora cha Alizeti - Uzalishaji, Uangalizi, Uvunaji na Uhifadhi


Utangulizi
Alizeti hulimwa kwa wingi katika mikoa ya Shinyanga, Singida, Dodoma, Iringa, Tabora, Morogoro, Ruvuma, Mbeya, Arusha, Manyara, na RukwaZao hili hulimwa kwa ajili ya chakula na biashara.
Mambo muhimu ya kuzingatia wakati wa uzalishaji
  • Kuchagua aina bora ya mbegu
    Chagua aina bora ya mbegu inayovumilia magonjwa, wadudu, inayotoa mazao mengi na kiwango kikubwa cha mafuta.
  • Vilevile chagua aina ya mbegu ambayo hukomaa kwa wakati mmoja ili kurahisisha uvunaji.
Kuweka mbolea
Rutubisha udongo kwa kutumia mbolea za mboji na samadi ili kupata mazao mengi na bora.
Kudhibiti wadudu na magonjwa
Alizeti hushambuliwa na magonjwa ya majani, mizizi na masuke ambayo husababisha upungufu wa mavunoHivyo ni muhimu kuyadhibiti ili kupata mavuno mengi na boraPia ndege hupunguza mavuno kwa kiasi cha asilimia 50 au zaidiNjia ya kudhibiti ndege ni kwa kuwafukuza na kupanda mbegu zinazokomaa mapema.
Maandalizi kabla ya kuvuna; 
Ukaguzi 
Kagua shamba kuona kama alizeti imekomaaAlizeti hukomaa kati ya miezi minne hadi sita tangu kupandaWakati huo punje huwa na unyevu wa asilimia 25Ni muhimu kuvuna alizeti mapema ili kuepuka mashambulizi ya panya, mchwa na ndege waharibifu
Dalili za alizeti iliyokomaa
  • Suke hubadilika rangi kutoka manjano na kuelekea kuwa nyeusi.
  • Viuwa vya pembeni mwa suke hunyauka na hubadilika kutoka rangi ya manjano na kuwa ya kahawia
Uvunaji, ukaushaji na ubebaji 
Vifaa vya kuvunia na kubebea kutoka shambani
  • Kisu
  • Vikapu
  • Magunia
  • Matenga Vifaa vya kukaushia
  • Maturubai
  • Mikeka
  • Kichanja bora Vyombo vya usafiri kutoka shambani
  • Matoroli
  • Matela ya matrekta
  • Mikokoteni ya kukokotwa na wanyama
  • Magari 

Kuvuna
Alizeti huvunwa kwa kutumia mikono ambapo suke hukatwa kwa kutumia kisuPia mashine (combine harvester) hutumika kuvunia alizeti katika nchi zinazolima alizeti kwa wingi. Masuke ya alizeti huwekwa kwenye vikapu ambavyo hutumika kusomba alizeti ndani ya shambaKisha alizeti hufungashwa kwenye magunia na kusafirishwa hadi nyumbani tayari kwa kukausha

Kukausha 
Kuna hatua mbili za kukausha alizeti; kukausha masuke na kukausha mbegu za alizeti
  • Kukausha masuke - Masuke hutandazwa kwenye kichanja bora katika kina kisichozidi sentimita 30 ili yaweze kukauka vizuri. 
    Vilevile huweza kutandazwa kwenye maturubai, mikeka au sakafu safi. Lengo la hatua hii ni kukausha masuke ya alizeti ili kurahisisha upuraji
    KUPURA 
    Upuraji hufanyika baada ya kuhakikisha kuwa masuke ya alizeti yamekauka vizuriMasuke ya alizeti hupurwa kwa kutumia mikono ambapo mbegu hutenganishwa kwa kupiga masuke taratibu kutumia mtiNi muhimu kupiga masuke taratibu ili kuepuka kupasua mbegu
    Pura kwenye kichanja bora, maturubai au mikeka
  • Kukausha mbegu 
    Mbegu za alizeti hukaushwa juani kwa kutandazwa kwenye vichanja bora, maturubai, mikeka au sakafu safi
    Tandaza mbegu katika kina kisichozidi sentimita 4 ili ziweze kukauka vizuri.
    Lengo la hatua hii ni kukausha mbegu baada ya kupura ili kufikia kiwango cha unyevu kinachotakiwa kwa hifadhi salama ambacho ni asilimia 8
Jinsi ya kutambua mbegu zilizokauka vizuri 
  • Kufikicha mbegu 
  • Mbegu zilizokauka maganda yake hutoka kwa urahisi zinapofikichwaKumimina kwenye chombo kama debe 
  • Mbegu zilizokauka hutoa mlio mkali zinapomiminwa kwenye vyombo hivyo
  • Mbegu zilizokauka hung'ara Kutumia kipima unyevu.
  • Mbegu zilizokauka vizuri kipimo huonyesha asilimia 8
Kupepeta na kupembua 
Kupepeta na kupembua hufanyika ili kuondoa takataka kama vile mawe, wadudu, mapepe, mbegu zilizooza au kupasukaMbegu za alizeti hupepetwa kwa kutumia ungo au mashine zinazoendeshwa kwa mkono, injini au umemeMashine hizi zina uwezo wa kupepeta na kupembua kilo 60 hadi 350 kwa saa kutegemea aina ya mashine na ukubwa wa mashine yenyewe
Kuhifadhi
Alizeti iliyopurwa huhifadhiwa katika hali ya kichele kwenye maghala bora, yaani vihenge, sailo au biniAlizeti ya kuhifadhi kwenye maghala ya nyumba ifungashwe kwenye magunia na ipangwe kwenye chaga kwa kupishanishaIli kurahisisha kazi ya kukagua ghala, acha nafasi ya mita moja kutoka kwenye ukutaZiba sehemu zote za ghala ili kuzuia panya kuingiaPanya hupenda sana kula punje za alizeti, na husababisha upungufu mkubwa wa punje ambao husababisha upotevu wa asilimia 30 kwa kipindi cha miezi mitatu ya hifadhiAsilimia ya upotevu inaweza kuwa kubwa zaidi kutegemea idadi ya panya na upatikanaji wa vyakula vingine kwa wakati huoMatumizi ya Mbegu za Alizeti Mbegu za alizeti hasa zenye mistari zinaweza kuliwa baada ya kukaangwa au kukaushwaPia zinatumika katika utengenezaji wa mikateMbegu za alizeti husindikwa kupata bidhaa ya mafuta
Kusindika mbegu za alizeti kupata mafuta
Vifaa
  • Mashine ya kukamua mafuta 
  • Chujio safi 
  • Ndoo 
  • Vifungashio
  • Sufuria
  • Mizani Malighafi 
  • Mbegu za alizeti 
  • Maji 
  • Chumvi 
Njia ya kukamua mafuta 
  • Chagua mbegu bora za alizeti
  • Zianike kwenye jua kwa muda wa saa 1 hadi 2
  • Weka kwenye mashine ya kukamulia ya daraja au Ram
  • Kamua mafuta
  • Chuja mafuta kwa kitambaa au chujio safi 
  • Pima mafuta yaliyokamuliwa
  • Ongeza maji na chumviKatika lita 10 za mafuta weka lita moja ya maji na gramu 200 za chumvi Weka mafuta kwenye chombo cha kuchemshia (sufuria)
  • Chemsha hadi maji yote yaishe 
  • Sauti ya kuchemka ikiisha ni dalili kuwa maji yamekwisha.
  • Ipua, acha yapoe, kisha chuja kwa kitambaa safi au chujio 
  • Fungasha kwenye vyombo safi na vikavu na vyenye mifuniko 
  • Weka lakiri na lebo  Hifadhi kwenye sehemu safi, kavu na yenye mwanga hafifu
Matumizi 
Mafuta hutumika katika mapishi mbalimbali na yana virutubishi vifuatavyo: - Mafuta gramu 100 Nguvu kilokalori 900

Comments

  1. Mafuta ya alizeti yanaweza kuhifadhiwa bila kuharibika kwa mda gani?

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

Utengenezaji wa Chakula cha Kuku wa Nyama (Bloilers)

Utangulizi Kuku wa nyama wana mahitaji yafuatayo ya viinilishe katika chakula ili wakue vizuri Viinilisha vya wanga 60-65%   Protini 30-35%   Madini 2-8% Chakula cha Vifaranga Chakula hiki hutengenezwa katika namna ya kumsaidia kifaranga aweze kumeza vizuri na hivyo hakitakiwi kuwa katika punje punje. Hata kama utanunua pumba, ni vema kuzipitisha kwenye mashine ili ziwe laini zaidi.  Mahitaji (kgs)  Unga wa dona wa nafaka kama mahindi au mtama 40  Pumba za mtama au mahindi au uwele 27  Mashudu ya alizeti au ufuta, au pamba au karanga n.k. 20  Unga wa mifupa au chokaa ya kuku (DCP) 2.25  Dagaa au mabaki ya samaki (sangara fish meal) 10  Chumvi ya jikoni 0.5  Virutubisho (Broiler premix) 0.25  Jumla utapata 100Kg. Chakula cha kukuzia – growers mash Mahitaji (Kg) Mahindi yaliyobarazwa au mtama au uwele 25   Pumba za mtama au mahindi au uwele 44   Mashudu ya alizeti au ufuta, au pamba au karanga n.k. 17   Unga wa mifupa a...

Aina Za Miti ya Minazi

AINA ZA MINAZI Inafaa mkulima kufahamu kuna aina mbali mbali za minazi na ina mahitaji tofauti katika ukuaji. Ujuzi huu utamsaidia katika kuchagua aina ya minazi itakayofaa kwa eneo lake na kwa kiwango chake cha utunzaji. KUNA AINA TATU ZA MINAZI Minazi mirefu ya asili Minazi mifupi Minazi chotara MINAZI MIREFU YA ASILI (EAT) Minazi ya aina hii ndiyo inayojulikana na wakulima wengi kwa vile ni ya kiasili na imezoea mazingira yetu. Minazi hii huchukua miaka 6-8 tangu kupandikizwa hadi kuzaa. Minazi ya aina hii huvumilia ukame na inao uwezo wa kutoa wastani wa nazi 40 kwa mwaka. Nazi huwa kubwa na zenye nyama nene ambayo inafaa kwa kupikia na kukamua mafuta. Minazi hii huishi kad ya miaka 60 na kuendelea. Nchini Tanzania, minazi hii hustawi vyema ukanda wa pwani sehemu zisizo na mawe na ambazo hazituamishi maji. MINAZI MIFUPI (DWARF) Minazi ya aina hii huzaa mapema kuanzia miaka miwili. Huzaa nazi nyingi na ndogo. Nazi hizi huwa na nyama nyembamba hivyo hutumika kwa nnadafu. Minazi huhit...

Kilimo Bora cha Migomba

UTANGULIZI Hapa Tanzania kilimo cha migomba kimekuwepo Kwa miaka mingi. Kilimo hiki ni maarufu sana kwa sababu zao la ndizi limekuwa likitumika kama chakula kikuu kwa baadhi ya mikoa kama vile Kagera, Kilimanjaro na Mbeya na hivyo kulifanya muhimu, kufuatia mazao ya mahindi, mpunga, mtama, muhogo,viazi na mazao ya jamii ya kunde kama vile maharage. Zao la ndizi linaweza kuwa moja kati ya mazao ya biashara iwapo litazalishwa kwa kufuata kanuni bora za uzalishaji wa zao hilo, ikwa ni pamoja na kupanda aina bora ya migomba inayozaa ndizi zinazotambulika katika masoko ya kimataifa. ASILI YA MIGOMBA Asili ya migomba ni nchi za Malaysia na India ambazo ziko Kusini Mashariki mwa Asia. Migomba inayolimwa sasa imetokana na migomba ijulikanayo kama Musa balbisiana ambayo asili yake ni India, na Musa acuminata ambayo asili yake ni Malaysia. Kutoka Malaysia na India migomba ilifika Afrika Mashariki katika karne ya tano MAENEO YANAYOLIMWA MIGOMBA NCHINI Nchini Tanzania mikoa inayoshughulika na kili...