Viazi mviringo ni moja ya mazao muhimu katika mazao ya mizizi ambalo huzalishwa kwa wingi katika mikoa ya Mbeya, Iringa, Rukwa, Kilimanjaro, Arusha, Mara na Tanga. Uzalishaji wake ni wastani wa tani 340,000 kwa mwaka. Zao hili huchangia kwa kiasi kikubwa katika uchumi wa mkulima kama zao la biashara na chakula.
Mambo Muhimu ya Uzalishaji
Ubora wa zao la viazi mviringo hutegemea sana matunzo ya zao hilo wakati wa uzalishaji. Viazi vinavyopata matunzo mazuri hutoa mazao yenye ubora unaotakiwa katika hifadhi ya muda mrefu na usindikaji. Hivyo wakati wa uzalishaji ni muhimu kuzingatia yafuatayo:
Kuchagua mbegu
Chagua aina ya mbegu kufuatana na mahitaji ya soko na nayovumilia mashambulizi ya magonjwa. Tumia mbegu bora isiyo na magonjwa na inayozaa mazao mengi na bora.
Kuweka mbolea
- Viazi vinahitaji rutuba ya kutosha ili kutoa mazao mengi na bora.
- Tumia mbolea za asili ili kudumisha rutuba.
- Utayarishaji, Hifadhi na Usindikaji wa Mazao ya Mizizi baada ya Kuvuna
- Iwapo ni lazima kutumia mbolea za viwandani ni muhimu kupata ushauri wa
- kitaalam kuhusu aina na viwango vya mbolea.
- Palilia ili kuondoa magugu na kuruhusu mimea kutumia unyevu na rutuba vizuri.
- Wakati wa palizi pandishia udongo kwenye mimea ili kuepusha jua linaloweza kushusha ubora wa zao. Viazi vilivyopigwa na jua hubadilika rangi na kuwa vya kijani na ubora hushuka. Viazi vya namna hii huwa havihifadhiki kwa muda mrefu.
- Ni muhimu kuzingatia nafasi ya kupanda ili kupata mazao mengi na bora.
- Panda kwa nafasi kama inavyoshauriwa na wataalamu.
Zao la viazi mviringo huathirika kwa urahisi na magonjwa ya ukungu, bakteria na virusi ambavyo visipodhibitiwa huweza kuleta hasara kubwa kuanzia shambani hadi ghalani. Hivyo muhimu kukagua shamba ili kubaini na kudhibiti magonjwa kabla ya kusababisha upotevu wa zao.
Maandalizi kabla ya kuvuna
Ni muhimu kufanya maandalizi ya kutosha ili kupunguza upotevu wa mazao.
Kukagua shamba
Kagua shamba kuona kama viazi vimekomaa. Viazi mviringo hukomaa kati ya miezi mitatu hadi minne toka kupanda.
Dalili za viazi mviringo vilivyokomaa
- Udongo uliozunguka shina hupasuka
- Majani hubadilika rangi kutoka kijani kuwa ya manjano.
- Mizizi midogo midogo ya viazi hunyauka.
- Sehemu ya juu ya mmea hunyauka.
Vifaa vya kuvunia
- Majembe
- Magunia
- Vikapu
- Magari
- Matela ya matrekta
- Mikokoteni
- Magunia
- Viazi mviringo huweza kuvunwa kwa kutumia jembe la mkono na jembe maalum la kukokotwa na wanyama. Ni muhimu kuvuna wakati kuna unyevu kiasi kwenye udongo ili kurahisisha uvunaji.
- Kuvuna kwa kutumia mikono
Mashina ya viazi mviringo yanaweza kung’olewa kwa mkono au kuchimbuliwa kwa jembe kutegemea hali ya udongo. - Uangalifu ni muhimu ili kuepuka kukata au kuchubua viazi.
Ng’oa viazi na kung’uta udongo
Viache shambani kwa muda wa siku moja ili vinyauke na kuimarisha ngozi. (curing) - Weka kwenye magunia au kwenye vikapu na vipeleke sehemu ya kusafishia, kuchambulia na kufungashia
Comments
Post a Comment