Maandalizi ya kitalu
- Tumia matuta ya mwinuko yenye upana wa mita 1 hadi mita 1.5 kutoka
- kati ya tuta na tuta na upana wa mita 1
- Siha mbegu katika mistari yenye upana wa sentimita 15
- Kiasi cha gramu 100 ya mbegu hutosha kwa ekari
- Tumia mbolea ya DAP wakati wa kusiha mbegu
- Dhibiti wadudu kama wapo, wasiliana na Bw, shamba kwa ushauri
- Miche huwa tayari kwa kupandikiza baada ya wiki 4
- Matumizi ya trei za miche kwa vitalu ni bora kuliko vitalu vya matuta
Maandalizi ya shamba
- Lima shamba kwa trekta, kwa ng’ombe ama kwa jembe la mkono kwa kina cha sentimita 30 hadi 45
- Weka matuta ya mwinuko
- Weka miche katika makundi kulingana na ukubwa na panda kadri ya makundi hayo
- Tumia fimbo-alama kuweka alama za kupandia
- Hakikisha shamba lina unyevu wa kutosha kabla ya kupanda ama tumia mbolea
- kianzio
- Panda sentimita 40 hadi 50 pande mbili za tuta kwa mfumo wa zig-zag
Palizi
- Palilia shamba mara kwa mara ili kuhakikisha shamba halina magugu
- Magugu hudhibitiwa kwa palizi ya jembe, kung’oa kwa mkono ama matumizi ya viuagugu
Mbolea
- Tumia mbolea ya DAP wakati wa kupanda, CAN ama SA wiki tatu baadaye na kisha tumia NPK wiki sita baada ya kupanda. Matumizi ya mbolea za maji yafanyike kila baada ya wiki mbili kutegemea na mahitaji
- Tumia nguzo na kamba mita mbili kutoka nguzo na nguzo pande mbili za tuta zigzag na pitisha kamba kuunganisha nguzo kila baada ya sentimita 20 kwenda juu
Matumizi ya viuatilifu
- Matumizi ya viuatilifu yafanyike kila baada ya wiki mbili kwa ushauri wa wataalam
- Pili pili hoho hukomaa na kuwa tayari kwa kuanza kuvuna siku 60 baada ya kupanda
[Imetolewa na HOT CONSULTANTS FIRM
Comments
Post a Comment