Skip to main content

Magonjwa ya Kuku - Chanjo, Kinga na Matibabu




Utangulizi
Tunashauri jamii kufuga kuku wa kuchanganya damu (cross breed) yaani pandisha kuku wa kienyeji na wale wa kisasa (indigenous + Pure breeds) ili kuweza kupata kuku ambao kwa kiasi fulani huhimili magonjwa. Wafugaji wengi wanakosea sana taratibu za kuwalisha kuku kitu ambacho kinawapa hasara lakini kama akiwa ni mtu wa kuzingatia anaepukana na magonjwa yanayoweza kujitokeza kutokana na uzembe wake. Chakula nacho ni tatizo watu wengi wanakosea vipimo, kuku anayetaga anatakiwa ale kwa kiwango maalum kinachotakiwa.kuku akila na kupitiliza kiwango au kupunguza hatagi kwa kiwango kinachotakiwa au asitage sana itategemea ameathirika kwa kiwango gani kwa sababu akiwa na mafuta kwa wingi hatagi,akipungukiwa na chakula hatagi.
Minyoo na utitiri nalo ni tatizo linachangia kuku kutokutaga, unashauriwa kumpa kuku dawa za minyoo na utitiri kwa wakati. Inashauriwa kutumia mabanda ya ghorofa kwa ajili ya vifaranga ili kuepukana na bacteria wanatokana maranda kwetu utajionea na ni faida kwako.

Magonjwa yanayosababishwa na virusi
  1. Mdondo (Newcastle):
    Dalili zake:
    kuku kukohoa,kuhema kwa shida,kutokwa na ute mdomoni na puani,hupatwa na kizunguzungu, kuharrisha mharo wa kijani na manjano na hatimaye kuku hufa ghafla. Vifo huweza kufikia asilimia90
  2. Ndui ya kuku: fowlpox)
    Kuku hupatwa na vipele vya mviringo kwenye upanga, (masikio,miguu na sehemu zisizo na manyoya.vifo vichache kwa kuku wakubwa, wadogo huweza kufa nusu ya kundi.CHANJO WIKI YA NANE (wapewe antibiotic na vitamini) hakuna tiba)
  3. Mahepe (.marek’s disease)Kuku kupooza miguu, mabawa na shingo huweza kupinda, mara nyingi huwapata kuku wenye umri wa wiki ya 16 hadi 30.kiasi cha robo ya mitemba wanaweza kufa. (chanja vifaranga wakiwa na umri wa siku moja)
  4. Gumboro :vifaranga huharisha mharo mweupe,huhangaikahangaika, hushindwa kuhema, manyoya husimama, hudumaa, hutetemeka na hatimaye hufa.vifo vyaweza kufikia 5% hadi 10%. (Hakuna tiba wapatiwe chanjo ya gumburo)
  5. Magonjwa yashambuliayo mfumo wa hewa
    (Infectious bronchitis, laryngotracheitis or chicken influenza) 
    upungufu wa mayai kwa kuku wanaotaga,vifaranga hupata matatizo ya kupumua na kupiga chafya na hufa kwa wingi
     
    (huzuiwa kwa chanjo, hakuna tiba.)
  6. Mafua makali ya ndege:
    kupumua kwa shida, kukohoa na kupiga chafya, sehemu za kikole(kidevu na kishungi) hubadilika na kuwa rangi ya zambarau,kutokwa na machozi,kupinda shingo na kuanza kuzunguka, kuvimba kichwa, kuharisha kinyesi chenye majimaji, rangi ya kijani na baadaye kinyesi cheupe.
    (hakuna tiba muone daktari)
  7. Homa ya matumbo: (salmonella gallinarum)
    ugonjwa huu unaweza kurithiwa kupitia kwenye mayai au kuambukizwa kutokana na kuku wagonjwa, kinyesi, kudonoana, na mazingira machafu, 
    Kuku huharisha mharo wa kijani, vilemba na upanga hupauka kutokana na upungufu wa damu, manyoya husimama.vifo huweza kufikia 50%. Weka banda katika hali ya usafi,ondoa kuku waliougua,usitumie mayai yenye ugonjwa kuangulia.
  8. Pullorum bacillary white diarrhea (bacteria salmonella pullorum)huathiri zaidi vifaranga(kabla ya umri wa wiki 4) vifaranga hujikusanya pamoja na kutetemeka kama waliopatwa na baridi.huharisha mharo mweupe hamu ya kula hupungua,manyoa hunyea na hupumua kwa taabu.vifo huweza kufikia asilimia 50.
  9. Kipindupindu cha kuku(Fowl cholera)
    kuku kuhara mharo wa rangi ya njano.husinzia na kulegea,hulala kichwa kikining’inia kwenye mabawa.manyoya husimama,kuhema kwa shida,hushindwa kusimama na hatimaye hufa.vifo huweza kufikia asilimia 50 
    Usafi wa banda
    (huweza kutibika kwa dawa ya sulfa)
  10. Ugonjwa unaoshambulia mfumo wa hewa (chronic respiratory)
    Kuku kupata mafua, kukohoa kushindwa kupumua, kutokwa na makamasi,vifaranga hudumaa,utagaji hupungua na viungo vya mifupa huweza kuvimba
    Tiba: antibiotic hutibu,usafi wa banda.
  11. Ugonjwa wa kuhara damu:
    Kuku huharisha kinyesi kilichochanganyika na damu na mara nyingine damu tupu,hudhoofisha kuku, huteremsha mabawa na hatimaye kuku huweza kufa. 
    Usafi wa banda,hutibiwa kwa kutumia dawa kama vile Amprolium.salfa na Esb3.Muone daktar.i
[Imetolewa na TAVEPA]

Comments

Popular posts from this blog

Utengenezaji wa Chakula cha Kuku wa Nyama (Bloilers)

Utangulizi Kuku wa nyama wana mahitaji yafuatayo ya viinilishe katika chakula ili wakue vizuri Viinilisha vya wanga 60-65%   Protini 30-35%   Madini 2-8% Chakula cha Vifaranga Chakula hiki hutengenezwa katika namna ya kumsaidia kifaranga aweze kumeza vizuri na hivyo hakitakiwi kuwa katika punje punje. Hata kama utanunua pumba, ni vema kuzipitisha kwenye mashine ili ziwe laini zaidi.  Mahitaji (kgs)  Unga wa dona wa nafaka kama mahindi au mtama 40  Pumba za mtama au mahindi au uwele 27  Mashudu ya alizeti au ufuta, au pamba au karanga n.k. 20  Unga wa mifupa au chokaa ya kuku (DCP) 2.25  Dagaa au mabaki ya samaki (sangara fish meal) 10  Chumvi ya jikoni 0.5  Virutubisho (Broiler premix) 0.25  Jumla utapata 100Kg. Chakula cha kukuzia – growers mash Mahitaji (Kg) Mahindi yaliyobarazwa au mtama au uwele 25   Pumba za mtama au mahindi au uwele 44   Mashudu ya alizeti au ufuta, au pamba au karanga n.k. 17   Unga wa mifupa a...

Aina Za Miti ya Minazi

AINA ZA MINAZI Inafaa mkulima kufahamu kuna aina mbali mbali za minazi na ina mahitaji tofauti katika ukuaji. Ujuzi huu utamsaidia katika kuchagua aina ya minazi itakayofaa kwa eneo lake na kwa kiwango chake cha utunzaji. KUNA AINA TATU ZA MINAZI Minazi mirefu ya asili Minazi mifupi Minazi chotara MINAZI MIREFU YA ASILI (EAT) Minazi ya aina hii ndiyo inayojulikana na wakulima wengi kwa vile ni ya kiasili na imezoea mazingira yetu. Minazi hii huchukua miaka 6-8 tangu kupandikizwa hadi kuzaa. Minazi ya aina hii huvumilia ukame na inao uwezo wa kutoa wastani wa nazi 40 kwa mwaka. Nazi huwa kubwa na zenye nyama nene ambayo inafaa kwa kupikia na kukamua mafuta. Minazi hii huishi kad ya miaka 60 na kuendelea. Nchini Tanzania, minazi hii hustawi vyema ukanda wa pwani sehemu zisizo na mawe na ambazo hazituamishi maji. MINAZI MIFUPI (DWARF) Minazi ya aina hii huzaa mapema kuanzia miaka miwili. Huzaa nazi nyingi na ndogo. Nazi hizi huwa na nyama nyembamba hivyo hutumika kwa nnadafu. Minazi huhit...

Kilimo Bora cha Migomba

UTANGULIZI Hapa Tanzania kilimo cha migomba kimekuwepo Kwa miaka mingi. Kilimo hiki ni maarufu sana kwa sababu zao la ndizi limekuwa likitumika kama chakula kikuu kwa baadhi ya mikoa kama vile Kagera, Kilimanjaro na Mbeya na hivyo kulifanya muhimu, kufuatia mazao ya mahindi, mpunga, mtama, muhogo,viazi na mazao ya jamii ya kunde kama vile maharage. Zao la ndizi linaweza kuwa moja kati ya mazao ya biashara iwapo litazalishwa kwa kufuata kanuni bora za uzalishaji wa zao hilo, ikwa ni pamoja na kupanda aina bora ya migomba inayozaa ndizi zinazotambulika katika masoko ya kimataifa. ASILI YA MIGOMBA Asili ya migomba ni nchi za Malaysia na India ambazo ziko Kusini Mashariki mwa Asia. Migomba inayolimwa sasa imetokana na migomba ijulikanayo kama Musa balbisiana ambayo asili yake ni India, na Musa acuminata ambayo asili yake ni Malaysia. Kutoka Malaysia na India migomba ilifika Afrika Mashariki katika karne ya tano MAENEO YANAYOLIMWA MIGOMBA NCHINI Nchini Tanzania mikoa inayoshughulika na kili...