AINA ZA MINAZI
Inafaa mkulima kufahamu kuna aina mbali mbali za minazi na ina mahitaji tofauti katika ukuaji. Ujuzi huu utamsaidia katika kuchagua aina ya minazi itakayofaa kwa eneo lake na kwa kiwango chake cha utunzaji.
KUNA AINA TATU ZA MINAZI
- Minazi mirefu ya asili
- Minazi mifupi
- Minazi chotara
MINAZI MIREFU YA ASILI (EAT)
Minazi ya aina hii ndiyo inayojulikana na wakulima wengi kwa vile ni ya kiasili na imezoea mazingira yetu. Minazi hii huchukua miaka 6-8 tangu kupandikizwa hadi kuzaa. Minazi ya aina hii huvumilia ukame na inao uwezo wa kutoa wastani wa nazi 40 kwa mwaka. Nazi huwa kubwa na zenye nyama nene ambayo inafaa kwa kupikia na kukamua mafuta. Minazi hii huishi kad ya miaka 60 na kuendelea. Nchini Tanzania, minazi hii hustawi vyema ukanda wa pwani sehemu zisizo na mawe na ambazo hazituamishi maji.
MINAZI MIFUPI (DWARF)
Minazi ya aina hii huzaa mapema kuanzia miaka miwili. Huzaa nazi nyingi na ndogo. Nazi hizi huwa na nyama nyembamba hivyo hutumika kwa nnadafu. Minazi huhitaji mvua nyingi na huduma zaidi, kwa sababu hii minazi hupandwa kama mapambo karibu na nyumba. Kwa kawaida minazi hii huishi kati ya miaka 40-50.
MINAZI CHOTARA (HYBRID)
Minazi chotara hutokana na mchanganyiko wa minazi mifupi na mirefu, hivyo ina sifa za minazi aina zote mbili, Sifa hizo ni:
Kukua haraka na huanza kuzaa kati ya miaka 4-5. Kwa kawaida mnazi huzaa zaidi ya nazi 60 kwa mwaka. Nazi huwa kubwa zenye nyama nene hivyo hutumika kwa kupikia na kukamua mafuta. Minazi hii huishi kati ya miaka 60 na kuendelea. Inahitaji udongo ulio na rutuba na uangalizi wa hali yajuu. Minazi hii inashauriwa kupandwa sehemu zenye udongo tifutifu na zinazo pata mvua za kutosha tu kama baadhi ya sehemu za visiwa, mkoa wa Tanga, Pwani na kwenye mabonde ya mikoa ya Kusini.
Taswira
Mpaka sasa kuna aina mbili za chotara ambazo ni MAWA na CAMWA ambazo ubora wake umethibitishwa. Mbegu aina hizi hupatikana katika mashamba ya mbegu yaliopo Zanzibar ambayo yanamilikiwa na Mradi wa Taifa wa Uendelezaji Minazi.
Nahitaji kufahamu ya kuwa hekari moja inachukua miche mingapi ya minazi
ReplyDelete37
DeleteAsante kwa elimu nzuri ila naomba unifahamishe kuwa ekari moja ya shamba la minazi linalotunzwa vizuri linatoa tani ngapi za minazi?
ReplyDeleteVP mkoa wa arusha unafaaa kwa kilimo cha Nazi?
ReplyDeleteJe kwa mkoa wetu wa dar es salaam nazi hizi huweza kulimwa sehem za miinuko??
ReplyDeleteSwali langu ni kwamba Kilimanjaro unaweza ukapanda miti ya minazi na ikazaa vizuriii...??
ReplyDelete