Skip to main content

Kilimo Bora cha Pilipili Mtama


Utangulizi
Jina la kitalaam ni Piper nigram na kwa kiingereza ni black pepper. Zao hili asili yake ni Mashariki ya Mbali, na linalimwa zaidi katika mkoa wa Tanga na Zanzibar.

Matumizi
Pilipili nyeusi na nyeupe zote hutumika kwa mapishi ya nyama, samaki na kwa mapishi mengine mbalimbali. Nchi za magharibi zina matumizi makubwa ya viungo hivi. Aidha pilipili mtama nyeusi
ndiyo huzalishwa zaidi hapa nchini. 

Uzalishaji
  • Hali ya hewa na udongo
    Viungo vingi humea katika maeneo yenye joto la wastani kati ya nyuzi joto 24-26 na huzalishwa maeneo ya mwambao. 
    Udongo wenye rutuba na unaopitisha maji na wenye uchachu wa kiasi cha pH 6.5. 
    Mahitaji ya mvua ni mililita 1500- 2000 kwa mwaka.
  • Uchaguzi wa mbegu
    Uchaguzi huzingatia mambo yafuatayo:-
    a) Urefu wa pingili na ukubwa wa majani
    b) Ufupi wa pingili unaoambatana na majani madogo.
    Tofauti iko hadi kwenye umbile la matunda.  Majani ya mche mama sehemu  kinapokatwa kipando huondolewa wiki mbili kabla ya kukata. Vipando vyenye macho (nodes) 3-4 humika. Macho mawili huzikwa kwenye udongo na kipando kiwekewe kivuli. Inashauriwa kuweka mbolea ya samadi wakati wa kupanda.\
  • Nafasi ya upandaji
    Nafasi ya kupanda ni mita 2-3 kati ya mmea na mmea endapo miche imepandwa na miti inayotakiwa kupogolewa mara kwa mara.
  • Mahitaji ya mbolea
    Matumizi ya mbolea hapa Tanzania si makubwa katika kilimo cha viungo. Ingawa kiasi cha kilo 0.4 cha Urea, kilo 0.3 cha Superphosphate na kilo 0.3 cha Potash ya Muriate kinaweza kutumika kwa miche mikubwa.
  • Miti ya kusimikia miche
    Miche hupandwa kwa kusimikiwa nguzo ili ikue kwa kujizungusha kwenye miti kama mijenga ua, n.k. Mti huo wa kusimikia nao pia hupaswa kupunguziwa majani ili kupunguza giza. Kila kabla ya msimu miti hiyo hupaswa kupunguziwa matawi (pruning).
Kupogolea miche ya pilipili mtama
Mche ukifikia miezi 18 inapaswa kupogolea kwa kukata sehemu ya juu ya mche ili kufanya matawi mengine yachipue chini ya mche. Inashauriwa mche kuwa na urefu wa mita 3-3.5.

Uvunaji
Maua ya kwanza hutoka baada ya miaka miwili. Matunda hukomaa miezi tisa (9)
hadi kumi (10). Uvunaji ni mizunguko 5 hadi 6 kwa mwaka. Pilipili mtama inaweza
kuvunwa kwa misimu miwili. Mavuno ni kati ya tani 0.35-3.75 kwa hekta.

Kuhifadhi
Pilipili mtama inaweza ikawekwa  kwenye chombo kisichopitisha hewa na kudumu kwa miaka 20 bila kuharibika.

Mashambulizi ya wadudu na magonjwa
Hapa nchini hakuna matatizo makubwa ya wadudu na magonjwa.

Masoko 
Soko la pilipili matama linapatikana ndani ya nchi na nje pia. Bei ya ndani ni kati ya Sh1,000-1,500. Zao hili huuzwa katika nchi za Uganda, Kenya, Uingereza, Ujerumani, Mashariki ya Kati, n.k. Bei ya Nje ni wastani wa dola za kimarekani 1,985 kwa tani. 

Imetolewa na Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika

Comments

Popular posts from this blog

Utengenezaji wa Chakula cha Kuku wa Nyama (Bloilers)

Utangulizi Kuku wa nyama wana mahitaji yafuatayo ya viinilishe katika chakula ili wakue vizuri Viinilisha vya wanga 60-65%   Protini 30-35%   Madini 2-8% Chakula cha Vifaranga Chakula hiki hutengenezwa katika namna ya kumsaidia kifaranga aweze kumeza vizuri na hivyo hakitakiwi kuwa katika punje punje. Hata kama utanunua pumba, ni vema kuzipitisha kwenye mashine ili ziwe laini zaidi.  Mahitaji (kgs)  Unga wa dona wa nafaka kama mahindi au mtama 40  Pumba za mtama au mahindi au uwele 27  Mashudu ya alizeti au ufuta, au pamba au karanga n.k. 20  Unga wa mifupa au chokaa ya kuku (DCP) 2.25  Dagaa au mabaki ya samaki (sangara fish meal) 10  Chumvi ya jikoni 0.5  Virutubisho (Broiler premix) 0.25  Jumla utapata 100Kg. Chakula cha kukuzia – growers mash Mahitaji (Kg) Mahindi yaliyobarazwa au mtama au uwele 25   Pumba za mtama au mahindi au uwele 44   Mashudu ya alizeti au ufuta, au pamba au karanga n.k. 17   Unga wa mifupa a...

Aina Za Miti ya Minazi

AINA ZA MINAZI Inafaa mkulima kufahamu kuna aina mbali mbali za minazi na ina mahitaji tofauti katika ukuaji. Ujuzi huu utamsaidia katika kuchagua aina ya minazi itakayofaa kwa eneo lake na kwa kiwango chake cha utunzaji. KUNA AINA TATU ZA MINAZI Minazi mirefu ya asili Minazi mifupi Minazi chotara MINAZI MIREFU YA ASILI (EAT) Minazi ya aina hii ndiyo inayojulikana na wakulima wengi kwa vile ni ya kiasili na imezoea mazingira yetu. Minazi hii huchukua miaka 6-8 tangu kupandikizwa hadi kuzaa. Minazi ya aina hii huvumilia ukame na inao uwezo wa kutoa wastani wa nazi 40 kwa mwaka. Nazi huwa kubwa na zenye nyama nene ambayo inafaa kwa kupikia na kukamua mafuta. Minazi hii huishi kad ya miaka 60 na kuendelea. Nchini Tanzania, minazi hii hustawi vyema ukanda wa pwani sehemu zisizo na mawe na ambazo hazituamishi maji. MINAZI MIFUPI (DWARF) Minazi ya aina hii huzaa mapema kuanzia miaka miwili. Huzaa nazi nyingi na ndogo. Nazi hizi huwa na nyama nyembamba hivyo hutumika kwa nnadafu. Minazi huhit...

Kilimo Bora cha Migomba

UTANGULIZI Hapa Tanzania kilimo cha migomba kimekuwepo Kwa miaka mingi. Kilimo hiki ni maarufu sana kwa sababu zao la ndizi limekuwa likitumika kama chakula kikuu kwa baadhi ya mikoa kama vile Kagera, Kilimanjaro na Mbeya na hivyo kulifanya muhimu, kufuatia mazao ya mahindi, mpunga, mtama, muhogo,viazi na mazao ya jamii ya kunde kama vile maharage. Zao la ndizi linaweza kuwa moja kati ya mazao ya biashara iwapo litazalishwa kwa kufuata kanuni bora za uzalishaji wa zao hilo, ikwa ni pamoja na kupanda aina bora ya migomba inayozaa ndizi zinazotambulika katika masoko ya kimataifa. ASILI YA MIGOMBA Asili ya migomba ni nchi za Malaysia na India ambazo ziko Kusini Mashariki mwa Asia. Migomba inayolimwa sasa imetokana na migomba ijulikanayo kama Musa balbisiana ambayo asili yake ni India, na Musa acuminata ambayo asili yake ni Malaysia. Kutoka Malaysia na India migomba ilifika Afrika Mashariki katika karne ya tano MAENEO YANAYOLIMWA MIGOMBA NCHINI Nchini Tanzania mikoa inayoshughulika na kili...