Skip to main content

Upandaji wa Miche ya Minazi

UPANDAJI BORA WA MICHE

Ili kupata mnazi ulio bora mkulima ni lazima awe muangalifu wakati wa kupanda. Mche uliopandwa vibaya huchelewa kukua na hata wakati mwingine hufa. Mazingira kama vile aina ya udongo, kiasi cha mvua, joto, na mwinuko lazima yaangaliwe kwa makini kabla ya kupanda.

MAZINGIRA YANAYOFAA KULIMA MINAZI
Sehemu zinazofaa kulima zao la minazi lazima ziwe na mvua ya kutosha au ziwe na mabonde yenye unyevu ardhini. Kwa kifupi mvua isipungue milimita 1000 hadi 2000 kwa mwaka na kiangazi kisichozidi miezi mitatu.
Sehemu hiyo vilevile iwe na joto la kutosha (23 hadi 30 nyuzi joto) na mwinuko kutoka usawa wa bahari usiozidi mita 600. Minazi inapendelea mwangaza wajua, kwa hivyo isipandwe chini ya miti kama vile miembe au mikorosho.

UCHAGUZI WA ARDHI
Ni vyema kufanya uchaguzi wa ardhLinayofaa kwa minazi kabla ya kupanda.

ARDHI ISIYOFAA KUPANDA MINAZI
Haifai kupanda minazi kwenye ardhi yenye mawe, miamba, jasi na maji yaliyotuama. Sehemu hizi hazifai kwa sababu mizizi ya minazi inapokutana na moja ya hivi, husababisha minazi kudumaa, kubadilika rangi ya makuti kuwa njano badala ya kijani, huacha kuzaa na hatiinaye hufa. Vile vile ardhi yenye kutuanusha maji zaidi ya siku mbili haifai, kwani husababisha mizizi ya minazi kuoza, hivyo kushindwa kupata chakula na mara nyingi niinazi kufa.

ARDHI INAYOFAA KUPANDA MINAZI
Minazi inaweza kustawi katika aina nyingi za udongo, lakini hupendelea zaidi kichanga, tifutifu au kinongo.
Katika seheinu zinazoathiriwa na ukame minazi inaweza kupandwa kwenye maeneo ambayo kina cha maji ardhini wakati wa kiangazi hakizidi mita 3.5 kutoka usawa wa ardhi.

KUTAYARISHA SHAMBA
Baada ya kuchagua sehemu ambayo minazi itapandwa mkulima ni lazima atayarishe shamba mapema kabla ya mvua kuanza. Matayarisho hayo ni pamoja na kufyeka, kung'oa visiki na kuondoa takataka. Kufanya hivi hurahisisha kazi za badaaye hasa upirnaji, palizi na kuzuia wadudu kama vile chonga.

UPIMAJI WA SHAMBA
Upimaji wa shamba ni muhimu kabla ya kupanda miche ya minazi.
·Mkulima anaweza kupima shamba lake kwa kuzingatia mambo yafuatayo:
(1) Iwapo mkulima anataka kuchanganya mazao mengine kwenye shamba la minazi kama vile michungwa, minanasi, mipera na migomba, inashauriwa kutumia mita 9 kati ya mnazi na mnazi. Mstari hadi mstari mita 15.
(2) Iwapo mknlima atapendelea kupanda minazi peke yake shambani inabidi atumie nafasi ya mita 9x9x9 pembe tatu. Nafasi ya aina hii inafaa kwenye sehemu zenye mvua ya kutosha kama Zanzibar, Tanga, Pangani, bonde la Ng'apa na Mikindani. Sehemu zenye mvua chache kama vile Mtwara, Lindi, Kisarawe, Kibaha na Morogoro inashauriwa kutumia nafasi ya mita 10 kutoka mnazi hadi mnazi na mita 10, kati ya mstari na mstari.
MICHE BORA KWA UPANDAJI
Kabla ya mkulima kupanda miche ya minazi hana budi kuchagua miche iliyo bora. Uwe haukushanibuliwa na wadndu au magonjwa. Uwewenyeafyanamajani yakeyawe kijani. Uwe wenye majani yapatayo sita na uwe nmekaa kitaluni kwa miezi 9.

UCHIMBAJI WA MASHIMO NA UPANDAJI
Ni vizuri mashimo yachimbwe kabla ya mvua'. Kipimo cha kila shimo ni sentimita 60 kwa urefu, upana na kina. Shimo linapochimbwa udongo wajuu utengwe mbali na udongo wa chini. Baadae changanya udongo wa juu na debe moja la samadi au mboji (compost) kama inapatikana. Weka udongo wajuu wenye rutuba zaidi kwanza kwenye shimo, halafu panda mche wako katika shimo. Rudishia udongo wa chini na kuhakikisha kuwa mche wako umeshindiliwa ili usimame barabara.

UCHAGUZI WA ARDHI

Ardhi inayofaa kupanda minazi ni tifutifu, kichanga na kinongo.

Mawe, mwamba najasi huwia minazi kupata chakula cha kutosha kutoka ardhini.

Maji yaiwyotucima husababishu kuow mizizi na minazi kufa.
UPIMAJI WA PEMBE MRABA KWA KUPANDA MINAZI NA MAZAO MENGINE

Kubla ya kuanza, tengeneza pembe mruba katika sehemu ya kuumia upimaji.

BAADA YA UPIMAJI WA PEMBE TATU MRABA
UPIMAJI WA PEMBE TATU KWA KUPANDA MINAZI TU

Upimaji huu lazima wapatikane watu watatu. Kila mmoja ashikefundo. Mambo zichomekwe kujuatana na majundo ya kamba. Upimaji huu ni kwu mirwzi pekee au na mmao ya msimu.

BAADA YA UPIMAJI WA PEMBE TATU
UCHIMBAJI WA SHIMO LA MNAZI

Shimo huchimbwa kwa kutofautisha tabaka za udongo. Udongo wajuu huchimbwa ukawekwa upande.

Udongo wa chini huchimbwa ukawekwa upande mwengine ili usichanganyike na tabaka ya udongo wajuu.

Wakati wa kupandu tanguliza uclongo wa tabaka ya juu.

Pandikiza mche wako na kumalma udongo wa tabaka la chini.
UPANDAJI MZURI NA MBAYA

Upandaji huu ni mzuri, majani hayakufimikwa na udongo.

Upandaji huu husababisha baada ya muda mche hutoka ardhini na kuanguka kwa upepo au kuvutwa na wanyama.

Comments

Popular posts from this blog

Utengenezaji wa Chakula cha Kuku wa Nyama (Bloilers)

Utangulizi Kuku wa nyama wana mahitaji yafuatayo ya viinilishe katika chakula ili wakue vizuri Viinilisha vya wanga 60-65%   Protini 30-35%   Madini 2-8% Chakula cha Vifaranga Chakula hiki hutengenezwa katika namna ya kumsaidia kifaranga aweze kumeza vizuri na hivyo hakitakiwi kuwa katika punje punje. Hata kama utanunua pumba, ni vema kuzipitisha kwenye mashine ili ziwe laini zaidi.  Mahitaji (kgs)  Unga wa dona wa nafaka kama mahindi au mtama 40  Pumba za mtama au mahindi au uwele 27  Mashudu ya alizeti au ufuta, au pamba au karanga n.k. 20  Unga wa mifupa au chokaa ya kuku (DCP) 2.25  Dagaa au mabaki ya samaki (sangara fish meal) 10  Chumvi ya jikoni 0.5  Virutubisho (Broiler premix) 0.25  Jumla utapata 100Kg. Chakula cha kukuzia – growers mash Mahitaji (Kg) Mahindi yaliyobarazwa au mtama au uwele 25   Pumba za mtama au mahindi au uwele 44   Mashudu ya alizeti au ufuta, au pamba au karanga n.k. 17   Unga wa mifupa a...

Aina Za Miti ya Minazi

AINA ZA MINAZI Inafaa mkulima kufahamu kuna aina mbali mbali za minazi na ina mahitaji tofauti katika ukuaji. Ujuzi huu utamsaidia katika kuchagua aina ya minazi itakayofaa kwa eneo lake na kwa kiwango chake cha utunzaji. KUNA AINA TATU ZA MINAZI Minazi mirefu ya asili Minazi mifupi Minazi chotara MINAZI MIREFU YA ASILI (EAT) Minazi ya aina hii ndiyo inayojulikana na wakulima wengi kwa vile ni ya kiasili na imezoea mazingira yetu. Minazi hii huchukua miaka 6-8 tangu kupandikizwa hadi kuzaa. Minazi ya aina hii huvumilia ukame na inao uwezo wa kutoa wastani wa nazi 40 kwa mwaka. Nazi huwa kubwa na zenye nyama nene ambayo inafaa kwa kupikia na kukamua mafuta. Minazi hii huishi kad ya miaka 60 na kuendelea. Nchini Tanzania, minazi hii hustawi vyema ukanda wa pwani sehemu zisizo na mawe na ambazo hazituamishi maji. MINAZI MIFUPI (DWARF) Minazi ya aina hii huzaa mapema kuanzia miaka miwili. Huzaa nazi nyingi na ndogo. Nazi hizi huwa na nyama nyembamba hivyo hutumika kwa nnadafu. Minazi huhit...

Kilimo Bora cha Migomba

UTANGULIZI Hapa Tanzania kilimo cha migomba kimekuwepo Kwa miaka mingi. Kilimo hiki ni maarufu sana kwa sababu zao la ndizi limekuwa likitumika kama chakula kikuu kwa baadhi ya mikoa kama vile Kagera, Kilimanjaro na Mbeya na hivyo kulifanya muhimu, kufuatia mazao ya mahindi, mpunga, mtama, muhogo,viazi na mazao ya jamii ya kunde kama vile maharage. Zao la ndizi linaweza kuwa moja kati ya mazao ya biashara iwapo litazalishwa kwa kufuata kanuni bora za uzalishaji wa zao hilo, ikwa ni pamoja na kupanda aina bora ya migomba inayozaa ndizi zinazotambulika katika masoko ya kimataifa. ASILI YA MIGOMBA Asili ya migomba ni nchi za Malaysia na India ambazo ziko Kusini Mashariki mwa Asia. Migomba inayolimwa sasa imetokana na migomba ijulikanayo kama Musa balbisiana ambayo asili yake ni India, na Musa acuminata ambayo asili yake ni Malaysia. Kutoka Malaysia na India migomba ilifika Afrika Mashariki katika karne ya tano MAENEO YANAYOLIMWA MIGOMBA NCHINI Nchini Tanzania mikoa inayoshughulika na kili...