Skip to main content

Maelezo ya Msingi Kuhusu Kilimo cha Mpunga



Utangulizi
Mpunga ni zao linalozalishwa kwa wingi barani Afrika. Mchele huliwa na watu wa jamii mbali mbali duniani kote na ni nafaka ya pili kuzalishwa kwa wingi baada ya mahindi. Mahindi huzalishwa kwaajili ya matumizi mengine zaidi ya chakula hivyo inawezekana mchele unaongoza kwa kutumiwa kama lishe.
Mpunga unaweza kutumika kama zao la chakula na biashara na ni muhimu katika kujenga afya ya mwili,
kuhakikisha ulinzi wa chakula na huchangia katika matumizi endelevu ya ardhi. Mpunga unaweza kutoa mavuno mengi kuliko mahindi na bei ya mchele mara nyingi huzidi bei ya mahindi.
Kilimo cha mpunga huendelea vizuri kama eneo lina mvua/maji ya kutosha pamoja na kuwa na watu wengi ili kuupa huduma mbalimbali kama vile kung’olea majani.
Namna ya kupanda mpunga

1.     Kuchagua mbegu
Chagua mbegu bora, nzuri ambazo hazina dalili yoyote ya kuathirika na ugonjwa, zilizojaa vizuri na zenye afya. Mfano wa aina za mbegu nzuri za mpunga ni; Supa, Kahogo Red, Rufiji na Saro.

2.     Matibabu ya mbegu kabla ya kupanda
Tibu mbegu kabla ya kuzipanda. Hii hufanya mbegu ziweze kuchipua vizuri na kuwa mimea mizuri. Njia zinazoweza kutumika kutibu mbegu ni kama:
·    Kusafisha mbegu kwa kutumia maji ya moto ambapo unaweka maji jikoni na kuyaacha yapate moto kiasi kisha weka mbegu kwenye mfuko wa pamba na tumbukiza kwenye maji.
·        Hakikisha joto halizidi wala kupungua na mfuko haufiki chini. Toa mfuko kutoka kwenye maji ya moto na hamishia kwenye maji safi ya baridi. Sambaza mbegu kwenye karatasi kavu ili kupoa na kukauka.
·   Inashauriwa kutokuhifadhi mbegu zilizotibiwa na baadala yake zipandwe mara moja kwenye kitalu au shambani. Njia hii huondoa vijidudu vinavyoweza kusababisha ugonjwa.
·        Kuloweka mbegu ili kuifanya ipate unyevu nyevu wa kutosha kuchipua, kupunguza muda wa kuanza kuota na kuzuia mbegu kuoza. Wakati wa kuloweka badilisha maji ili kuondoa viini venye sumu na kuwezesha hewa safi kuingia.
      Kabla ya kuchipuka: Kausha mbegu na zifunike na majani kwa masaa 24 hadi 48. Hii husaidia huhakikisha kuwa mbegu zinachipua kwa wakati mmoja, huzuia kuchipuka kuliko kithiri na huruhusu mzunguko wa hewa ambao unahitajika ili kuchipua.

3.     Kuotesha
·        Kwa kawaida gramu 80-100 za mbegu hupandwa kwenye mita 1 (80-100g/m2)
·        Tawanya/eneza mbegu kwa usawa katika kitalu
·        Usididimize kitalu baada ya kuotesha mbegu
·        Tumia kiasi cha mbegu angalau kilo 20 kwa ekari moja

4.     Kutayarisha kitalu
·        Lima angalau wiki mbili kabla ya kuotesha na kufurika.
·        Kandika/changanya tope angalau wiki moja kabla ya kuotesha na tengeneza kitalu kilichonyanyuka.
·        Ondoa maji kwenye kitalu siku moja kabla ya kuotesha ili kuimarisha sehemu ya juu ya udongo
·        Hakikisha udongo wa juu sio laini sana kwani itasababisha mbegu kuzama chini.
·        Mwagilia siku chache baada ya kuotesha ili udongo uwe na unyevu wa kutosha na hakikisha viwango cha kudidimia na maji havizidi agalau 1cm-3cm.
·        Siku moja kabla ya kung’oa na kupandikiza, ongeza kiwango cha maji kwenye kitalu kutoka 3 cm-10 cm ili kurahisisha ungo’aji na upandikizaji kwa kuondoa udongo ugandao kwenye mizizi.

5.     Kutayarisha shamba
Inashauriwa kulima shamba na kufurika angalau siku 15 kabla ya kupanda miche au mbegu moja kwa moja. Hii husaidia kuulinda mche kutokana na vijidudu visababishavyo maradhi kutoka kwenye udongo pia huzuia kupotea kwa nitrogen.

6.     Kupandikiza
Ni muhimu kuondoa miche kutoka kwenye kitalu na kuipanda shambani mara tuu inapofikia ukubwa wa kutosha. Miche inakuwa tayari kati ya wiki tatu hadi nne tangu kuotesha kutegemeana na mwanga wa jua, hali ya joto na aina ya mbegu. Nafasi ni kati ya 20×10 au 20×20 (Mstari kwa mstari na mmea kwa mmea) kutokana na aina ya mbegu. Kina cha upandaji cha 3 cm kinashauriwa ili kuwezesha mizizi kuchipua na kushika vizuri.

7.     Kupanda moja kwa moja
Njia hii imekuwa ikitumiwa na wakulima wengi kwa muda mrefu ambapo mbegu za mpunga hutawanywa shambani moja kwa moja. Kazi za shambani hupungua kwa kiasi kikubwa lakini pia uzalishaji hupungua kutokana na kuwa na magugu mengi na ugumu wa kuhudumia mimea shambani.

Uharibifu na magonjwa
Uharibifu wa mpunga hutokana na vijidudu, mimea au wadudu ambao wanauwezo wa kushusha kiwango cha uzalishaji wa mmea kwa mfano magugu, wadudu, panya buku na ndege. Sababu za kufumuka kwa magonjwa au wadudu zinaweza kuchangiwa na utumiaji wa madawa ya kuulia wadudu na utumiaji wa mbolea (nitrogen) kwa kiwango kikubwa au kwa muda mrefu sana.
Wadudu kama vile viwavi wanaweza kuzuilika kwa kupanda matembo tembo kando kando ya shamba la mpunga na magugu kuzuilika kwa kupandikiza miche shambani badala ya kupanda mbegu moja kwa moja.

Kuvuna
Kati ya miezi 4 hadi 6 (kutokana na aina) baada ya kupanda mpunga unakuwa umekomaa. Inashauriwa kuvuna katika muda muafaka ili kuzuia hasara itokanayo na wadudu, ndege, panya n.k.

Comments

Popular posts from this blog

Utengenezaji wa Chakula cha Kuku wa Nyama (Bloilers)

Utangulizi Kuku wa nyama wana mahitaji yafuatayo ya viinilishe katika chakula ili wakue vizuri Viinilisha vya wanga 60-65%   Protini 30-35%   Madini 2-8% Chakula cha Vifaranga Chakula hiki hutengenezwa katika namna ya kumsaidia kifaranga aweze kumeza vizuri na hivyo hakitakiwi kuwa katika punje punje. Hata kama utanunua pumba, ni vema kuzipitisha kwenye mashine ili ziwe laini zaidi.  Mahitaji (kgs)  Unga wa dona wa nafaka kama mahindi au mtama 40  Pumba za mtama au mahindi au uwele 27  Mashudu ya alizeti au ufuta, au pamba au karanga n.k. 20  Unga wa mifupa au chokaa ya kuku (DCP) 2.25  Dagaa au mabaki ya samaki (sangara fish meal) 10  Chumvi ya jikoni 0.5  Virutubisho (Broiler premix) 0.25  Jumla utapata 100Kg. Chakula cha kukuzia – growers mash Mahitaji (Kg) Mahindi yaliyobarazwa au mtama au uwele 25   Pumba za mtama au mahindi au uwele 44   Mashudu ya alizeti au ufuta, au pamba au karanga n.k. 17   Unga wa mifupa a...

Kilimo cha Miti ya Mbao - Uwekezaji wa Muda wa Kati na Mrefu

Utangulizi Kilimo cha miti ni uwekezaji wa muda wa kati na mrefu (mid & long term investments). Ila kwa kawaida jamii nyingi hasa za kiafrika huwa hazivutiwi na uwekezaji wa muda mrefu. Hata hivyo kama una mpango wa kuwa imara kiuchumi inashauriwaau yakupasa kufikiria na kujifunza aina za uwekezaji wa muda mrefu. Miti hutumika kwa matumizi mengi mfano mbao, nguzo za umeme na kujengea, mapambo, kuni na mkaa, kuzalisha matunda, mitishamba na madawa,  utengenezeaji wa karatasi n.k.  Mchanganuo Ekari moja ya shamba unaweza kupanda miti mia sita (500) mpaka mia saba (700). Gharama za kununua mashamba au maeneo ya kupandia miti hutegemea na eneo. Kwa  sehemu nyingi za vijijini maeneo kwa ekari moja hayazidi laki 5.  Miche ya kununua mfano Mitiki huuzwa kuanzia elfu moja (1000) kwa mche mmoja Gharama ya kununua miche =  1000 * 600 = 600,000   Pia unaweza kuokoa gharama za kununua miche kwa kuioteshe mwenyewe ktk vitalu na kuiamishia shambani baada ya kustawi v...

Uandaaji na Uoteshaji wa Mbegu za Mitiki

Utangulizi Mbegu za mitiki zinapatikana Tanzania Tree Seed Agency wako Msamvu Morogoro.Kilo moja ya mbegu za mitiki inatosha kuotesha kwenye shamba la hekta moja, ambayo ni wastani wa miti 1500 Matayarisho: Ganda la nje la mbengu ya mtiki ni gumu sana na lina sumu mbaya.Unatakiwa uloweke mbegu ya mitiki kwa masaa 72, na kila baada ya masaa 12 unatakiwa ubadilishe maji kwa kumwaga maji ya zamani na kuweka maji mapya. Baada ya masaa 72 anika mbegu zako juani kwa masaa 12 (zianikike ktk bati). Tengeneza kitalu, weka mbolea ya wanyama au mboji, kisha panda mbegu zako kwenye kitalu. Mwangilia maji kila siku asubuhi na jioni, mbegu zitaanza kuota baada ya siku 10 hadi 20. Miche ikifikia urefu wa futi moja, unaweza sasa kuiotesha kwenye shamba lako ulilotayarisha kwa ajili ya kuotesha miti. Kabla ya kung’'oa miche hakikisha unamwaga maji mengi, ili mizizi isikatike sana, kisha chukua kisu chenye makali ya kutosha na kata ncha ya juu ya mti na ondoa majani, hii inasaidia mti kuchipuka upya...