Skip to main content

Kilimo cha Mboga Mboga - Bilinganya

UTANGULIZI
Bilinganya imo katika jamii ya mimea inayohusisha nyanya, pilipili, viazi mviringo na nyanya mshumaa. Mboga hii ina viinilishe muhimu kama vile madini aina ya chokaa na chuma, vitamini A, B na C, wanga, protni na maji. Mboga hii hutumika kutengeneza supu au kama kiungo katika vyakula mbalimbali. Vile vite huweza kuhifadhiwa kwa kukatakata vipande na kuwekwa kwenye makopo.
Zao hili huhitaji hali yajoto la wastani, udongo wenye kina kirefu na rutuba ya kutosha na usiotuamisha maji. Kwa kawaida bilinganya hulimwa zaidi ya msimu mmoja, lakini katika nchi za Kitropild (joto) zao hili hulimwa kwa msimu mmoja.

AINA
Aina za bilinganya zinazolimwa kwa wingi katika nchi za ukanda wajoto ni kama zifuatazo:-
  • Black Beauty
    Aina hii huzaa sana, matunda yake meusi, makubwa, na ya mviringo.
  • Florida Market
    Matunda ya Florida Market yana umbo la yai. Aina hii pia huzaa sana, lakini hushambuliwa kwa urahisi na ugonjwa wa mnyauko bakiteria (Bacterial wilt).
  • Florida High Bush:
    Matunda yake ni makubwa ycnye umbo la yai na rangi ya kijani kibichi iliyochanganyika na nyeusi.
  • NewyorkSpineless
    Matunda ya Newyork Spineless ni ya mviringo, makubwa na yana rangi ya zambarau.
  • Peredeniya
    Aina hii huzaa sana, matunda yake ni makubwa kiasi na yana umbo la yai.
Aina zingine za bilinganya ni Matale, Kopek na Rosita. Aina hizi huvumilia sana mashambulizi ya ugonjwa wa mnyauko bakteria.

KUOTESHA MBEGU
Mbegu huoteshwa kwanza kwenye kitalu na baadaye miche huhamishiwa shambani. Kabla ya kusia mbegu, tengeneza tuta lenye upana wa mita moja na urefa wowote. Weka mbolea za asili kama vile samadi au takataka zilizooza vizuri, kiasi cha ndoo moja au mbili katika eneo la mita mraba moja. Sia mbegu kiasi cha gramu mbili mpaka tatu (nusu kijiko cha chai chenye ujazo wa gramu tano) katika eneo hilo. Gramu 500 za mbegu zinatosha kupandikiza katika eneo la hekta moja. Nafasi kati ya mstari na mstari iwe sentimita 10 hadi 15, na kina kiwe sentimita 1.5. Baada ya kusia mbegu fukia na tandaza nyasi kavu na kisha mwagilia maji. Endelea kumwagilia Idtalu kila siku, asubuhi najioni, hadi mbegu zitakapoota. Mbegu huota baada ya siku 10 hadi 12.

KUHAMISHA MICHE:
Miche huwa tayari kwa kupandikizwa shambani baada ya wiki sita hadi nane. Wakati huu huwa na urefu wa sentimita 15 mpaka 20 (sawa na urefu wa kalamu ya risasi).
Mwezi mmoja kabla ya kupandikiza miche, rutubisha udongo kwa kuweka mbolea za asili zilizooza vizuri. Mbolea hizi ni kama samadi, mbolea vunde na mbolea ya kuku.
Weka kiasi cha tani 10 hadi 20 kwa hekta. Kiasi hiki ni sawa na kuweka ndoo moja hadi mbili zenye ujazo wa lita 20 katika eneo la mita mraba moja. Mbolea ya mchanganyiko aina ya N.P.K yenye uwiano wa 20:10:10 huwekwa kwenye shimo wakati wa kupandikiza mche. Kiasi kinachohitajika ni gramu tatu hadi tano (sawa na nusu kijiko mpaka kijiko kimoja kidogo cha chai) kwa kila shimo.
Nafasi ya kupandikiza hutegemea aina ya bilinganya. Aina ndogo hupandikizwa katika nafasi ya sentimita 80 mpaka 100 kutoka mstari hadi mstari na sentimita 50 mpaka 60 kutoka mche hadi mche. Aina kubwa hupandikizwa katika nafasi ya sentimita 80 mpaka 100 kutoka mstari hadi mstari na sentimita 80 mpaka 90 kutoka mche hadi mche. Kazi ya kuhamisha miche ifanyike kwa uangalifu mkubwa ili kuepuka kuikata mizizi.

KUTUNZA SHAMBA:
  • Kuweka Matandazo
    Mara baada ya kupandikiza miche, tandaza nyasi kavu. Matandazo husaidia kuhifadhi unyevu, huzuia magugu yasiote na huongeza rutuba ya udongo.
  • Palizi
    Hakikisha shamba ni safi wakati wote ili kuzuia ushindani wa chakula, maji na mwanga kati ya mimea na magugu. Usafi wa shamba pia huondoa maficho ya wadudu waharibifu na huzuia kuenea kwa magonjwa.
  • Mbolea
    Mbolea ya kukuzia aina ya S/A huwekwa wiki tatu baada ya mmea kuanza kutoa maua. Kiasi cha gramu tatu hadi tano huwekwa kuzungukia kila mche. Mbolea iwekwe katika umbali wa sentimita tano mpaka 15 kutoka kwenye shina, kutegemea ukubwa wa mche. Hakikisha mbolea haigusi mmea.
  • Kukata Kilele
    Wiki mbili baada ya kupandildza miche, kata sehemu yajuu ya mmea (kilele) kama umepanda aina ndefu ya bilinganya. Hii itasaidia kupata matawi matatu hadi manne na mmea kutengeneza umbile la kichaka. Matawi yakizidi manne yaondolewe ili kupata mazao mengi na bora.
  •  Kumwagilia
    Zao la bilinganya hustawi vizuri likipata maji ya kutosha. Umwagiliaji ufanyike kila siku asubuhi na jioni kutegemea hali ya hewa.
Kuzuia Wadudu Waharibifu na Magonjwa:

WaduduWaharibifu:
  • Vinyatomvu wa Bilinganya (Eggplant Lacebugs)
    Wadudu hawa hushambulia zaidi sehemu ya chini ya jani. Hufyonza utomvu wa majani na kusababisha majani kuwa na mabaka meupe au njano. Mashambulizi yakizidi majani huanguka chini. Vinyatomvu wanaweza kuzuiwa kwa kunyunyizia moja ya dawa zifuatazo:-
    Deltamethrin (Decis), Dimethoate (Sapa Dimethoate) Fenvalerate (Sumicidin), Lambda - Cyhalothrin (Karate).
  • Vidukari au Wadudu mafuta (Cotton Aphids)
    Hawa ni wadudu wadogo wenye rangi nyeusi. Hushambulia majani machanga na kuyasababisha kudumaa na kukunjamana. Zuia wadudu hawa kwa kutumia mojawapo ya dawa zifuatazo:- Dimecron 50% E.C, Lambda - Cyhalothrin (Karate) Dichlorvos (Nogos).
  • Utiriri wa Mimea (Red Spider Mites)
    Ni vidudu vidogo vyenye rangi nyekundu iliyoiva. Hushambulia majani kwa kufyonza utomvu. Majani yaliyoshambuliwa huonyesha utando kama wa buibui. Mashambulizi yakizidi mmea hudumaa, majani hukauka na hatimaye hufa.
    Utiriri unazuiwa kwa kutumia dawa zifuatazo:- Acrex, Karathane 25% W.P., Dimethoate, Ekalux, Kelthane.
  • Minyoo Fundo (Root knot nematodes)
    Wadudu hawa hushambulia mizizi. Hutoa kinyesi ambacho ni sumukwammea. Sumu hii husababisba mizizi kuwa na nundu kama ya mizizi ya maharagwe. Mashambalizi yakizidi mmea hudumaa, hunyauka na hatimaye hufa.
    Njia ya kuzuia wadudu hawa ni kubadilisha mazao. Kwa mfano; baada ya kuvuna zao hili, zao linalofuata lisiwe lajamii moja na bilinganya, kamavile nyanya, pilipili naviazi mviringo. Pia dawa aina ya Carbofuran (Furadan) inaweza kutumika.
Magonjwa
  • Mnyauko Bakteria (Bacterial Wilt)
    Ugonjwa huu husababishwa na backteria. Mmea ulioshambuliwa hunyauka ghafla hasa wakati wajua kali
    Mnyauko bakteria unaweza kuzuiwa kwa kubadilisha mazao shambani. Endapo ardhi itashambuliwa na ugonjwa huu zao la bilinganya lisipandwe katika eneo hilo kwa muda wa miaka mitatu hadi mitano.
    Njia nyingine ni kupanda aina za bilinganya kama vile Matale, Kopek, na Rosita ambazo huvumilia mashambulizi ya ugonjwa huu.
  • Phomopsis Vexans
    Ugonjwa huu husababishwa na bakteria na hushambulia majani, shina na matunda.
  • Verticillium Wilt
    Huenezwa na maji na husababisha mmea kudumaa, majani kukunjamana na kuanguka.
Magonjwa ya Phomopsis Vexans na Verticillium Wilt yanaweza kuzuiwa kwa kung'oa na kuchoma moto mimea iliyoshambuliwa, kubadilisha mazao, na kuweka shamba katika hali ya usafi wakati wote.

KUVUNA
Bilinganya huanza kutoa matunda yaliyokomaa baada ya miezi miwili hadi mitatu tangu kupandikiza. Uvunaji huendelea kwa muda wa zaidi ya miezi minne na hauna budi ufanyike mapema maramatundayanapokomaa. Matunda yaliyokomaa sana hayafai kuliwa kwa sababu huwa na kambakamba na mbegu zilizokomaa. Vuna mara mbili au tatu kwa wiki, kwa kutumia kisu kikali ili usiumize matunda.

MAVUNO
Kwa kawaida zao hili huzaa sana iwapo limetunzwa vizuri. Shamba lililotunzwa vizuri linaweza kutoa mavuno tani 50 hadi 60 kwa hekta. Hata hivyo mavuno mengi hutegemea aina ya bilinganya, umwagiliaji na rutuba ya udongo.

Comments

Popular posts from this blog

Utengenezaji wa Chakula cha Kuku wa Nyama (Bloilers)

Utangulizi Kuku wa nyama wana mahitaji yafuatayo ya viinilishe katika chakula ili wakue vizuri Viinilisha vya wanga 60-65%   Protini 30-35%   Madini 2-8% Chakula cha Vifaranga Chakula hiki hutengenezwa katika namna ya kumsaidia kifaranga aweze kumeza vizuri na hivyo hakitakiwi kuwa katika punje punje. Hata kama utanunua pumba, ni vema kuzipitisha kwenye mashine ili ziwe laini zaidi.  Mahitaji (kgs)  Unga wa dona wa nafaka kama mahindi au mtama 40  Pumba za mtama au mahindi au uwele 27  Mashudu ya alizeti au ufuta, au pamba au karanga n.k. 20  Unga wa mifupa au chokaa ya kuku (DCP) 2.25  Dagaa au mabaki ya samaki (sangara fish meal) 10  Chumvi ya jikoni 0.5  Virutubisho (Broiler premix) 0.25  Jumla utapata 100Kg. Chakula cha kukuzia – growers mash Mahitaji (Kg) Mahindi yaliyobarazwa au mtama au uwele 25   Pumba za mtama au mahindi au uwele 44   Mashudu ya alizeti au ufuta, au pamba au karanga n.k. 17   Unga wa mifupa au chokaa ya kuku (DCP) 3.25   Dagaa au mabaki ya samaki (fish meal) 1

Aina Za Miti ya Minazi

AINA ZA MINAZI Inafaa mkulima kufahamu kuna aina mbali mbali za minazi na ina mahitaji tofauti katika ukuaji. Ujuzi huu utamsaidia katika kuchagua aina ya minazi itakayofaa kwa eneo lake na kwa kiwango chake cha utunzaji. KUNA AINA TATU ZA MINAZI Minazi mirefu ya asili Minazi mifupi Minazi chotara MINAZI MIREFU YA ASILI (EAT) Minazi ya aina hii ndiyo inayojulikana na wakulima wengi kwa vile ni ya kiasili na imezoea mazingira yetu. Minazi hii huchukua miaka 6-8 tangu kupandikizwa hadi kuzaa. Minazi ya aina hii huvumilia ukame na inao uwezo wa kutoa wastani wa nazi 40 kwa mwaka. Nazi huwa kubwa na zenye nyama nene ambayo inafaa kwa kupikia na kukamua mafuta. Minazi hii huishi kad ya miaka 60 na kuendelea. Nchini Tanzania, minazi hii hustawi vyema ukanda wa pwani sehemu zisizo na mawe na ambazo hazituamishi maji. MINAZI MIFUPI (DWARF) Minazi ya aina hii huzaa mapema kuanzia miaka miwili. Huzaa nazi nyingi na ndogo. Nazi hizi huwa na nyama nyembamba hivyo hutumika kwa nnadafu. Minazi huhit

Kilimo cha Miti ya Mbao - Uwekezaji wa Muda wa Kati na Mrefu

Utangulizi Kilimo cha miti ni uwekezaji wa muda wa kati na mrefu (mid & long term investments). Ila kwa kawaida jamii nyingi hasa za kiafrika huwa hazivutiwi na uwekezaji wa muda mrefu. Hata hivyo kama una mpango wa kuwa imara kiuchumi inashauriwaau yakupasa kufikiria na kujifunza aina za uwekezaji wa muda mrefu. Miti hutumika kwa matumizi mengi mfano mbao, nguzo za umeme na kujengea, mapambo, kuni na mkaa, kuzalisha matunda, mitishamba na madawa,  utengenezeaji wa karatasi n.k.  Mchanganuo Ekari moja ya shamba unaweza kupanda miti mia sita (500) mpaka mia saba (700). Gharama za kununua mashamba au maeneo ya kupandia miti hutegemea na eneo. Kwa  sehemu nyingi za vijijini maeneo kwa ekari moja hayazidi laki 5.  Miche ya kununua mfano Mitiki huuzwa kuanzia elfu moja (1000) kwa mche mmoja Gharama ya kununua miche =  1000 * 600 = 600,000   Pia unaweza kuokoa gharama za kununua miche kwa kuioteshe mwenyewe ktk vitalu na kuiamishia shambani baada ya kustawi vizuri na kuwa imara.  Mf. Mbe