Utangulizi
Bamia ni zao linalolimwa sana nchi za joto. Zao hili hutumika kama mboga inayoliwa matunda. Asili ya mboga hii ni Afrika ya Kati na ya Mashariki, lakini kwa sasa zao hili limeenea katika sehemu nyingi za kitropiki, kama Visiwa vya Caribbean, Malaysia na Philipines. Zipo aina nyingi za bamia, aina zile za kiasili nazo hutofautiana kulingana na eneo moja na lingine.
Matumizi
Bamia hupikwa pamoja na nyama, samaki au mboga nyingine.
Upandaji
Aidha kuotesha ili kurahisisha uotaji.
• Mbegu mbili zipandwe kwenye shimo moja.
Nafasi
Nafasi ya upandaji iwe ni sentimita 30 toka shimo hadi shimo na sentimita 50 toka mstari hadi mstari.
Kwa zile aina zinazorefuka sana iwe sentimita 40 kati ya shimo na shimo na sentimeta 70 kati ya mstari na mstari.
Palizi
Hakikisha shamba ni safi wakati wote kwa kuondoa magugu mara tu unapoona yamejitokeza.
Umwagiliaji
Iwapo unyevu wa ardhi hautoshi, inapendekezwa kutumia mojawapo ya njia za kumwagilia maji bustanini.
Wadudu waharibifu
Wadudu wanaoshambulia zao hili la bamia kama vile kimamba, funza wa vitumba na utitiri mwekundu.
Magonjwa
Magonjwa kama ukungu, ubwiri poda na kunyauka huathiri zao la bamia hivyo ni vyema kuzuia kwa kufuata mzunguko wa mazao na kutumia dawa kulingana na ushauri wa wataalamu wa kilimo.
Mambo ya kuzingatia
- Tumia mbegu bora
- Panda kwa nafasi
- Mwagilia maji ya kutosha
- Palilia shamba vizuri
- Vuna kwa wakati unaotakiwa
- Bamia huvunwa kabla ya kukomaa yaani zikiwa bado changa.
- Kiasi cha kilo 8000 zaweza kupatikana katika ekari moja iwapo zitatunzwa vizuri.
- Hakikisha unavuna bamia na kikonyo chake, kisu kinaweza kutumika kwa kuvuna
Comments
Post a Comment