Utangulizi
Utunzaji wa nguruwe mara nyingi hutegemea aina ya nguruwe, njia na aina ya ufugaji. Kwa mfano nguruwe jike anayefugwa kwa ajili ya kuzaa anahitaji kutunzwa tofauti na wale wanaonenepeshwa kwa ajili ya nyama. Kadhalika nguruwe wanaweza kufugwa ndani ya banda au nje, kutegemea na ukubwa wa shamba, fedha zilizopo kwa shughuli za ufugaji na aina ya nguruwe.
Utunzaji wa Nguruwe Dume
Achaguliwe dume mwenye sifa bora ikiwa ni pamoja na kutokuwa na kilema au ugonjwa wowote. Dume aliyechaguliwa, atenganishwe na majike ili kuepusha kupanda wakati usiotakiwa. Inabidi nguruwe huyu asinenepeshwe, kwa hiyo alishwe chakula bora kiasi cha kilo mbili hadi tatu kwa siku. Vile vile apewe maji kila siku.
Kama anapanda chini ya mara tatu kwa wiki, alishwe kilo mbili na nusu na kama anapanda zaidi ya mara tatu, alishwe kilo tatu kwa siku. Ikiwa dume ni dhaifu, aongezewe nusu kilo ya chakula na kama amenenepa sana apunguziwe nusu kilo ya chakula kwa siku. Ni muhimu awe na eneo la mita mraba 9.3 ilikuwezakupata mazoezi ya mwili. Ikiwa sehemu ya kupanda imetenganishwa eneo livve la mita mraba saba.
Nguruwe dume anaweza kutumika kwa kupandajike akiwa na umri wa miezi minane hadi tisa. Kwa umri huu anaruhusiwa kupanda jike moja kwa juma. Afikiapo miezi 10 anaruhusiwa kupanda majike mawili hadi matatu kwa juma. Akiwa na umri wa mwaka mmoja au zaidi ana uwezo wa kupanda jike mmoja kila siku kwa majuma mawili hadi matatu, kisha apumzike kwa muda wa majuma mawili. Dume wakubwa wasitumike kupanda jike wadogo kwani wanaweza kuleta madhara kama vile kuwavunja mgongo.
Ni vizuri nguruwe dume mmoja apande jike 15 hadi 20 kwa mwaka. Dume akizeeka au kuwa na ubovu wa miguu, achinjwe mara moja. Ni muhimu dume aogeshwe kwa sabuni na dawa zinazoweza kuua wadudu na vijidudu vinavyoweza kusababisha magonjwa. Banda na vifaa vinavyotumika visafishwe kila siku.
Utunzaji Wa Nguruwe Jike
Ili mfugaji aweze kupata mazao mengi na bora hana budi kuchagua nguruwe jike mwenye sifa zinazotakiwa. Nguruwe huyu ni vizuri awe amezaliwa na mama anayezaa watoto wengi, mwenye kutoa maziwa mengi na mtunzaji mzuri wa watoto. Tabia hizi zinarithiwa hata navizazi vingine vijavyo. Vile vile awe na afyanzuri na chuchu nyingi zisizopungua 12.
Nguruwe jike anaweza kuzaa akiwa na umri wa miezi mitano hadi sita. Ili kumzuia asibebe mimba mapema, ni vizuri atenganishwe na dume afikiapo umri huo.
Afikiapo miezi nane hadi tisa au akiwa na uzito wa kilo 130 ahaweza kupandishwa. Kabla ya kupandishwa nguruwejike apewe kilo 2.5 hadi tatu za chakula kwa siku. Nguruwe asipelekwe kwa dume mpaka atakapoonyesha dalili zajoto.
Dalili za Joto:
- Kutopenda kula chakula.
- Kupiga kelele ovyo.
- Kuhangaika kila mara.
- Hupenda kupanda au kupandwa na nguruwe wenzake.
- Sehemu ya uke huvimba na huwa nyekundu.
- Hukojoa mara kwa mara na hutoa ute mweupe usiokatika.
- Hutulia anapokandamizwa mgongoni.
Dalili hizi sio lazima zionekane zote kwa wakati mmoja hivyo ni jambo la muhimu kuwa mwangalifu. Ili dalili hizi ziweze kuonekana vizuri, chumba cha majike yanayotarajiwa kupandwa kinatakiwa kiwe karibu na cha dume. Joto hudumu kwa muda wa siku mbili hadi tatu. Ngumwe Jike apandishwe mara anapokua kwenye joto na kumdia tena katika muda wa masaa 12. Baada ya kupandishwa huchukua miezi mitatu, wiki tatu, siku tatu (siku 114 hadi 119) hadi kuzaa. Ngumwejike wawekwe kwenye banda lenye nafasi, hewa ya kutosha na uzio wa kutosha kwa ajili ya mazoezi.
Kutunza Nguruwe Mwenye Mimba.
Nguruwe wenye mimba wanahitaji mazoezi zaidi ili kuimarisha miguu na misuli yao, hivyo banda liwe na uzio wanapoweza kutoka na kucheza. Sehemu ya uzio isiwe na unyevu ili wasipate magonjwa, ikiwezekana kuwe na kivuli cha kuwakingajua.
Mandalizi ya Chumba cha Kuzalia
Wiki mbili hadi tatu kabla ya nguruwe kuzaa andaa chumba cha kuzalia. Chumba hiki kiwekwe boriti au reli kuzunguka ili kutenga sehemu ambayo itahifadhi watoto wasilaliwe au kukanyagwa na mama yao (angalia mchoro sura ya tano). Vile vile chumba hiki kiwe na sehemu ya kuweka chombo cha kuongezeajoto, chakula na maji kwa ajili ya watoto.
Maandalizi Kabla ya Kuzaa
Wiki moja kabla ya kuzaa ngumwe aogeshwe vizuri kwa maji safi na sabuni. Baada ya kuogeshwa anyunyiziwe dawa ili kuzuia wadudu wa ngozi na apewe dawa ya minyoo. Kisha ahamishiwe kwenye chumba cha kuzalia. Nguruwe mwenye mimba anahitaji kupewa chakula kinacholeta nguvu na kujenga mwili. Katika mwezi wa kwanza apewe kilo 2 hadi 2.5 kwa nguruwe mwenye afya nzuri, akiwa dhaifu apewe kilo 3 kwa majuma matatu. Mwezi wa pili mpaka siku ya tatu kabla ya kuzaa alishwe kilo 3.5 za chakula. Siku ya tatu kabla ya kuzaa, chakula kipunguzwe hadi kufikia kilo 2 kwa siku. Siku ya kuzaa asipewe chakula bali apewe maji tu.
Dalili za Kuzaa
Kuna dalili ambazo nguruwe huonyesha kabla hajazaa. Dalili hizi zionekanapo kuna umuhimu wa kuwepo mwangalizl ili aweze kutoa msaada kama itabidi, hasa kwa nguruwe anayezaa kwa mara ya kwanza.
· Kiwele na chuchu huwa kubwa kwa kujaa maziwa.
· Njia ya uke huvimba na kuwa nyekundu na mara nyingine hutoa maji mazito.
· Nguruwe huhangaika na hupumua kwa nguvu,
· Maziwa yanaweza kutoka yenyewe kwenye chuchu
· Hukojoa mara kwa mara
· Hukusanya majani na kuandaa mahali pa kuzalia
· Tumbo linapwelea na baadhi hupbteza hamu ya kula.
Utunzaji Baada ya Kuzaa
Mwangalizi ahakikishe kuwa watoto wananyonya na kuwaweka mahali penyejoto la kutosha. Vitovu vikatwe na kuachwa sentimita tano kwa kutumia vifaa visafi, na kisha paka dawa yajoto (lodine tincture) kuzuia magonjwa. Kondo la nyuma likidondoka litupwe na hakikisha limetoka lote kwa kuhesabu vipande kulingana na idadi yawatoto. Endapo idadi haikulingana, unashauriwa kumwona mtaalam wa mifugo aliyekaribu nawe. Baada ya nguruwe kuzaa apewe ongezeko la kilo moja ya chakula kila siku hadi siku ya nne. Kuanzia siku ya tano hadi ya nane apewe hadi kilo nne. Baada ya hapo apewe kilo tatu na moja ya tatu ya kilo kwa kila mtoto. Kwa mfano nguruwe mwenye watoto 12 apewe chakula kiasi cha kilo saba; (kilo 3 + 1/3 x 12 = 7). Vile vile apewe maji ya kutosha wakati wote. Kumbuka nguruwe akilishwa chakula kingi, atanenepa sana na hatapata mimba kwa urahisi na akibahatika kupata huweza kuharibika. Akilishwa chakula kidogo hudhoofika, huzaa watoto dhaifu na hutoa maziwa kidogo. Siku ya kuwatenganisha watoto na mama yao punguza chakula mpaka kilo mbili kwa siku. Siku inayofuata ongeza hadi kufikia kilo 2.5 mpaka tatu kutegemea na afya ya mama.
Nguruwe hurudi kwenye joto baada ya siku tano hadi kumi baada ya kuachisha kunyonyesha.
Utunzaji wa Watoto
- Ulishaji wa Maziwa ya Kwanza
Mara tu baada ya kuzaliwa hakikisha kuwa vitoto vinanyonya maziwa ya kwanza. Maziwa haya ni muhimu kwani yana viinilishe vya kujenga mwili, kuleta nguvu na kuongeza kinga dhidi ya maradhi. Kama mama amekufa mara tu baada ya kuzaa na hakuna nguruwe mwingine anayeweza kuwanyonyesha, wapewe maziwa ya kwanza ya ng’ombe. Endapo yatakosekana wapewe mchanganyiko maalum wa maziwa ya ng’ombe. - Joto
Watoto wa nguruwe huzaliwa bila manyoya na huwa hawana mafuta mengi ya kutosha kuwapatiajoto mwilini. Kwenye sehemu za baridi ni jambo la muhimu kuwapatiajoto kwa kutumia umeme au chemli. - Kuzuia Upungufu wa Damu
Nguruwe huzaliwa wakiwa na upungufu wa madini ya chuma. Halikadhalika maziwa ya mama yao huwa na upungufu wa madini hayo, hivyo wasipopatiwa madini hayo hupata upungufu wa damu, hudhoofika na hatimaye hufa. Ili kuepuka tatizo hili watoto wapatiwe madini ya chuma kwa kutumia mojawapo ya njia zifuatazo:
- Kudunga sindano ya madini hayo kwenye misuli siku mbili hadi tatu baada ya kuzaliwa.
- Kupaka madini ya chuma kwenye chuchu za mama.
- Changanya kilo moja ya madini ya chuma kwenye lita mbili za majimoto.
- Kuwanywesha maji yenye madini ya chuma mililita moja na nusu kwa mwezi mmoja.
- Kuwapa udongo msafi.
- Watoto wanaotunzwa kwenye sakafu ya saruji au mbao waruhusiwe kutoka nje ili kuweza kupata madini hayo kutoka kwenye udongo.
- Kuwapa vidonge vya madini ya chuma.
- Utoaji wa Meno
Siku chache baada ya kuzaliwa; meno kama sindano huchomoza katika taya zote mbili; Meno haya humumiza na kusababisha vidonda kwenye chuchu za mama wakati wanaponyonya. Hali hii humfanya mama kuwanyima watoto maziwa na kuwapiga, hivyo husababisha vifo vya watoto. Vile vile wao kwa wao huumizana. Meno haya yafaa yakatwe kwa mkasi mkali na msafi. Kama yasipokatwa huweza kumuumiza hata mhudumiaji. - Kukata Mkia
Mkia wa nguruwe unaweza kukatwa mara tu baada ya kuzaliwa ili wenyewe kwa wenyewe wasichezeane na kutafunana. Dawa ya lodine 5% ipakwe penye kidonda mara tu baadaya kukata mkia. - Kulisha Chakula cha Kwanza.
Watoto wapewe chakula maalum kidogo kidogo kuanzia siku ya kumi baada ya kuzaliwa. Chakula hiki kinatakiwa kiwe na viinilishe vya kujenga mwili, kuleta nguvu na kuzuia maradhi. Wakiwa na umri wa wiki tatu wapewe gramu 450; wiki ya nne na ya tano wapewe gramu 680 kwa nguruwe kwa siku. Endelea kuwapa chakula hiki mpaka siku ya kuachishwa kunyonya, na vile vile wapewe maji kwa wingi. - Kuhasi
Watoto madume ambao hawahitajiki kwa ajili ya kuzalisha wahasiwe wakiwa na umri kati ya wiki tatu hadi sita. Nguruwe waliohasiwa huwa wapole, hunenepa haraka, huwa na nguvu na wazito kwa hiyo wanafaa kwa nyama na mafuta. Muone mtaalam wa mifugo kwa ajili ya kuhasi nguruwe wako - Vitambulisho
Ngumwe hupewa vitambulisho kabla ya kuwatenganisha na mama yao kwa kuwaweka nambari kwenye masikio. Unashauriwa kumuona mtaalam wa mifugo akupe ushauri wajinsi ya kuweka vitambulisho hivyo. - Kutenganisha Watoto na Mama Yao.
Watoto wakifikia wiki nane watenganishe na mama yao. Mama ahamishwe kwenye chumba na kuwaacha watoto ili kupunguza mgutusho wa kuhamia mahali pengine. Unapowatenganisha hakikisha unawapa dawa ya minyoo, unawakinga dhidi ya magonjwa na kuwatibu mara wanapougua.
- Walioachishwa Kunyonya
Nguruwe walioachishwa kunyonya wapewe chakula cha kukuzia. Badilisha chakula kwa utaratibu maalum kwani kubadilisha chakula ghafla kutoka cha watoto kuingia cha kukuzia kunaweza kusababisha matatizo ya tumbo. Changanya chakula cha watoto na cha kukuzia katika uwiano ufuatao: -
Inashauriwa kuwapa chakula kama ifuatavyo:-
Kiasi kwa Siku (kilo)
Wiki 8 - 12 ------ 1.0KG
Wiki 12 - 18 ----- 1.5KG
Wiki 18 - 23 ----- 2.0KG
Wiki 23 - 30 ----- 3.0KG (Lisha mara mbili kwa siku. Pia wapewe maji safi yakutosha wakati wote.)
Usafi wa chumba, vifaa na mazingira ni muhimu kila siku. Pawe na vitu vya kuchezea kama vile minyororo au matairi ili kumpa mazoezi, kuondoa upweke na kupunguza kupigana. Endapo mkulima atahitaji nguruwe kwa ajili ya kuzalisha, wakati mzuri wa kuchagua ni wanapofikia umri wa miezi mitatu na kuendelea. Nguruwe wanaweza kuchinjwa kwa ajili ya nyama wakiwa wamefikia uzito wa kilo 60 hadi 90. Ikiwa watakuwa wametunzwa vizuri watafikia uzito huo wakiwa na umri wa miezi 6 hadi 8.
Comments
Post a Comment