Skip to main content

Uandaaji Kitalu na Uoteshaji Miche ya Minazi


UTANGULIZI
Kitalu ni mahali pa kuotesba mbegu na kuimarisha miche kabla ya kwenda kuipanda shambani.

UCHAGUZI WA SEHEMU YA KITALU
Wakati wa kuchagua sehemu ya kitalu ni vizud kuzingatia mambo yafuatayo:
Pawe na maji ya kudumu kwa ajili ya umwagiliaji. Udongo uwe wa kichanga na wenye rutuba. Sehemu iwe tambarare na isiyotuamisha maji. Pasiwe na kokoto au mwamba kwa kiasi cha mita moja (mita 1) chini ya aidhi. Pasiwe na kivuli kikubwa.

UTAYARISHAJI WA MATUTA
Majani yote kwenye eneo yafyekwe. Visiki vyote vichimbi we na viondolewe. Matuta yatayarishwe yenye upana wa mita moja na urefu wowote lakini usizidi mita 10. Tuta linaweza likanyanyuliwa kiasi cha cm 15 (nusu futi).
KUMBUKA: kuacha nafasi ya cm 60 (futi mbili) kati ya tuta na tuta. Jenga wigo kuzuia wanyama waharibifu kama vile ngombe, mbuzi na kuku.

UTAYARISHAJI WA MBEGU ZA KUATIKA
Nazi zilizovunwa si lazima zote ziwe nzuri kwa kupanda, hivyo uchaguzi mwingine ufanywe kwenye fungu hilo kabla ya kuatika (angalia sura ya pili).
Nazi zote zilizochaguliwa kuwa mbegu zichongwe kwa kutumia kisu. Sehemu ndogo inayoangaliana na upande wa nazi uliyo bapa zaidi uchongwe kiasi cm 7.5 (inchi 3) ili kuharakisha kupenya kwa maji na kuchipua.

UATIKAJI
Ni vizuri kuatika mbegu za nazi miezi 9 kabla ya msimu wa kupanda. Mbegu ziatikwe kwa kuzilaza, sehemu bapa iwe chini na sehemu , iliyochongwa iwejuu. Mbegu ziatikwe kwenye mtaro na zifukiwe kwa udongo kiasi cha cm 3 (au inchi 1) chini. Mbegu huchipuabaada ya mwezi mmoja hadi mitatu (1-3) kutegemea aina ya mbegu na umwagiliaji wa maji.

AINA ZA VITALU
Kuna aina mbili za vitalu vya miche:
- Kitalu cha moja kwa moja
- Kitalu cha hatua mbili
KITALU CHA MOJA KWA MOJA
Katika kitalu cha aina hii mbegu huoteshwa bila kuhamishwa. Nazi huatikwa kwa kutumia nafasi za cm 45 x cm 45 (mraba au pembe tatu mraba).
Faida:
Watu wachache huhitajika kutoa huduma kwenye kitalu cha aina hii. Hakuna miche inayokufa kutokana na kuhamisha. Miche haiathiriki kwa kiangazi cha muda mrefu. Kwa hivyo aina hii ya kitalu kinapendekezwa kwa wakulima wa kawaida.
Hasara:
Uchaguzi wa miche hufanyika mara moja tu wakati wa kuihamishia shambani.

KITALU CHA HATUA MBILI
Katika kitalu cha aina hii miche hupitia hatua mbili. Hatua ya kwanza mbegu zinawekwa katika tuta la mbegu. Baada ya kuchipua rrnche inahamishiwa kwenye tuta la miche au kwenye mifuko (hatua ya pili).
Nazi ambazo zitakuwa hazijachipua baada ya miezi minne ziondolewe kitaluni.

KITALU CHA MIFUKO
Mifuko myeusi inapendekezwa na pia iwe imetobolewa matundu kwa ajili ya kupitisha maji. Mifuko iwe na vipimo vya cm 40 x cm 40. Mifuko ijazwe robo tatu mchanganyiko wa samadi sehemu 2, udongo wa mboji sehemu 1, mchanga sehemu 1. Baada ya kujaza udongo 3/4 kwenye nufuko, mifuko ipangwe kadka mistari umbali wa cm 60 x cm 60 pembe tatumraba. Pandildzamche mmojakatikakila mfuko ukianzia na mche mkubwa na kuishia mche mdogo (kwa kurahisisha uchaguzi wa miche baadaye). Jaza udongo robo iliyobakia, shindilia udongo ili mche ukae vizuri. Acha nafasi ya cm 1.5 kutoka ukingo wa mfuko.

TUTA LA MICHE
Kama mkulima hana mifuko anaweza kuhamishia miche yake kwenye tuta la miche mara baada ya mbegu kuota. Nafasi kati ya mche na mche iwe cm 50 x cm 50 pembe tatu mraba.
KUMBUKA:
Kuwa upandaji wa miche unaanza na miche mikubwa ikifuatiwa na midogo.
Faida:
Mkulima anayo nafasi ya kufanya uchaguzi wa miche mara mbili yaani wakati wa kuhamishia katika kitalu cha miche (mfuko au ardhini) na pia wakad wa kuipandikiza shambani. Hivyo miche bora na yenye afya ndiyo tu inayotunzwa.
Hasara:
Kitalu cha aina hii kinategemea sana maji, na kinahitaji uj uzi na huduma. Kwa hivyo aina hii ya kitalu kinapendekezwa kwa wakulima walio na ujuzi zaidi.

UTUNZAJI WA MICHE
Ili miche iweze kukua vizuri mkulima hana budi kuzingatia yafuatayo:
- Kumwagilia maji ya kutosha asubuhi najioni isipokua siku zenye mvua.
- Kupalilia kwa mkono mara kwa mara ili kujiepusha na magonjwa na wadudu.
- Kuweka mbolea zilizoshauriwa hasa kwenye miche iliyopandikizwa kwenye mifuko.
MBOLEA
Mbolea zinazoshauriwa ni samadi, mboji na NPK.

UCHAGUZI WA MICHE
Uchaguzi wa miche bora huanzia mapema kwenye Idtalu mara baada ya kuota na huendelea mpaka wakati wa kuihamishia shambani. Ng'oa na kuchoma miche ambayo ni:
- Zeru zeru
- Mapacha
- Iliyochelewa kuota
- Iliyopihda
- Iliyodumaa na iliyodhoofika.
WADUDU NA MAGONJWA
Miche ya minazi kama miche mingine pia hushambuliwa na wadudu na magonjwa.

WADUDU
MCHWA
Mara kwa mara mashambulizi ya mchwa yakaguliwe. Dawa aina ya Gammaline 20 (Gamma BHC) itumiwe.
WADUDU MAFUTA (APHIDS)
Dawa za kuzuia wadudu mafuta zitumiwe mara tu uonapo mashambulizi kitaluni. Dawa kama vile Dimethoate 40% au Sumithion itumiwe.
MAGONJWA
Miche ya minazi mara nyingi hushambuliwa na magonjwa yafuatayo:
1. MADOA YA MAJANI (LEAFSPOT)
Ugonjwa huu husababishwa na ukungu (fungus). Huonekana kama madoa ya kahawia kwenye majani. Madoa yakiungana yanasababisha kukauka kwa majani. Dawa aina ya Dithane M-45 au Daconil itumiwe.
2. UOZO MBICHI NA MKAVU (BLAST & DRY ROT)
Mara kwa mara ugonjwa huu huonekana kitaluni na si rahisi kuzuiwa. Majani hugeuka manjano kuanzia chini. Kilele huoza na huweza kuchomolewa kwa urahisi. Kama ni uozo mbichi kilele hutoa harufu mbaya, na kama ni uozo mkavu kilele haldtoi harufu. Magonjwa yote mawili huenezwa na wadudu wafyonzao. Zuia ugonjwa huu kwa kuweka kivuli kidogo kwa kutumia makuti 3 kwa Idla mita moja (au panda mjenga ua), kwa sababu wadudu hawapendi kivuli. Hakikisha kuwa hakuna magugu na vichaka umbali wa mita 10 kuzunguka kitalu, kwa sababu wadudu hawa huzaliana katika mazingira hayo.
UCHAGUZI WA ENlEO LA KITALU CHA MINAZI
Pawe na maji ya kudwna kwa umwagiliaji wa mbegu.
UTAYARISHA JI WA SEHEMU YA KITALU
Fyeka majani na ng'oa visiki. Tayarisha tuta. Jenga wigo kuzuia wanyama waharibifii.
Chonga nazi kabla ya kuatika. Kurahisisha uotaji.
Baada ya mbegu kuchongwa na kuatikwa, fukia udongo theluthi mbili ya ukubwa wa nazi.
UATIKAJI WA MBEGU KATIKA KITALU CHA MOJA KWA MOJA
Atika kwa masafa yafuti moja na nusu (cm 45) kutoka kaii yci nau nufuti mojci nu misu kuioku mstari hadi mstari.
Tuta lililoatikwa linavyoonekana kwajuu kwa pembe tatu.
UCHAGUZI WA AWALI
Baada ya nazi kuota, chagua iliyo na ajya. Miche zeru zeru, iliyodumaa na mapacha iondolewe kwenye kitalu.
UATIKAJI WA MBEGU KATIKA KITALU CHA HATUA MBILI
Hatua ya pili: tuta la miche au miche kwenye mifuko.
UTUNZAJI WA KITALU
Miche haina budi kutunzwa. Mwagilia maji kila siku, palilia kila majani yanapoota, kuweka samadi, na kuzuia mashambulizi ya wadudu na maradhi.
UCHAGUZI WA MWISHO
Miche iliyo tayari kuhamishiwa shambani. Acha iliyo dhoofika, zeru zeru, na iliyochelewa kuota ing'olewe na ichomwe moto.

Comments

Popular posts from this blog

Utengenezaji wa Chakula cha Kuku wa Nyama (Bloilers)

Utangulizi Kuku wa nyama wana mahitaji yafuatayo ya viinilishe katika chakula ili wakue vizuri Viinilisha vya wanga 60-65%   Protini 30-35%   Madini 2-8% Chakula cha Vifaranga Chakula hiki hutengenezwa katika namna ya kumsaidia kifaranga aweze kumeza vizuri na hivyo hakitakiwi kuwa katika punje punje. Hata kama utanunua pumba, ni vema kuzipitisha kwenye mashine ili ziwe laini zaidi.  Mahitaji (kgs)  Unga wa dona wa nafaka kama mahindi au mtama 40  Pumba za mtama au mahindi au uwele 27  Mashudu ya alizeti au ufuta, au pamba au karanga n.k. 20  Unga wa mifupa au chokaa ya kuku (DCP) 2.25  Dagaa au mabaki ya samaki (sangara fish meal) 10  Chumvi ya jikoni 0.5  Virutubisho (Broiler premix) 0.25  Jumla utapata 100Kg. Chakula cha kukuzia – growers mash Mahitaji (Kg) Mahindi yaliyobarazwa au mtama au uwele 25   Pumba za mtama au mahindi au uwele 44   Mashudu ya alizeti au ufuta, au pamba au karanga n.k. 17   Unga wa mifupa a...

Aina Za Miti ya Minazi

AINA ZA MINAZI Inafaa mkulima kufahamu kuna aina mbali mbali za minazi na ina mahitaji tofauti katika ukuaji. Ujuzi huu utamsaidia katika kuchagua aina ya minazi itakayofaa kwa eneo lake na kwa kiwango chake cha utunzaji. KUNA AINA TATU ZA MINAZI Minazi mirefu ya asili Minazi mifupi Minazi chotara MINAZI MIREFU YA ASILI (EAT) Minazi ya aina hii ndiyo inayojulikana na wakulima wengi kwa vile ni ya kiasili na imezoea mazingira yetu. Minazi hii huchukua miaka 6-8 tangu kupandikizwa hadi kuzaa. Minazi ya aina hii huvumilia ukame na inao uwezo wa kutoa wastani wa nazi 40 kwa mwaka. Nazi huwa kubwa na zenye nyama nene ambayo inafaa kwa kupikia na kukamua mafuta. Minazi hii huishi kad ya miaka 60 na kuendelea. Nchini Tanzania, minazi hii hustawi vyema ukanda wa pwani sehemu zisizo na mawe na ambazo hazituamishi maji. MINAZI MIFUPI (DWARF) Minazi ya aina hii huzaa mapema kuanzia miaka miwili. Huzaa nazi nyingi na ndogo. Nazi hizi huwa na nyama nyembamba hivyo hutumika kwa nnadafu. Minazi huhit...

Kilimo Bora cha Migomba

UTANGULIZI Hapa Tanzania kilimo cha migomba kimekuwepo Kwa miaka mingi. Kilimo hiki ni maarufu sana kwa sababu zao la ndizi limekuwa likitumika kama chakula kikuu kwa baadhi ya mikoa kama vile Kagera, Kilimanjaro na Mbeya na hivyo kulifanya muhimu, kufuatia mazao ya mahindi, mpunga, mtama, muhogo,viazi na mazao ya jamii ya kunde kama vile maharage. Zao la ndizi linaweza kuwa moja kati ya mazao ya biashara iwapo litazalishwa kwa kufuata kanuni bora za uzalishaji wa zao hilo, ikwa ni pamoja na kupanda aina bora ya migomba inayozaa ndizi zinazotambulika katika masoko ya kimataifa. ASILI YA MIGOMBA Asili ya migomba ni nchi za Malaysia na India ambazo ziko Kusini Mashariki mwa Asia. Migomba inayolimwa sasa imetokana na migomba ijulikanayo kama Musa balbisiana ambayo asili yake ni India, na Musa acuminata ambayo asili yake ni Malaysia. Kutoka Malaysia na India migomba ilifika Afrika Mashariki katika karne ya tano MAENEO YANAYOLIMWA MIGOMBA NCHINI Nchini Tanzania mikoa inayoshughulika na kili...