Skip to main content

Kilimo Bora cha Matango



Utangulizi
Matango ni zao linalopendelea hali ya hewa ya joto na hustawi vyema kati ya nyuzi joto 18°C hadi 35°C

Udongo 
Hustawi vizuri katika udongo tifutifu wenye rutuba usiotuamisha maji

Maandalizi ya shamba 
Lima shamba kwa trekta, kwa ng’ombe ama kwa jembe la mkono kwa kina cha sentimita 30 hadi 45
Weka matuta ya mwinuko yenye upana wa mita 1 hadi 1.5 kutoka kati ya tuta na tuta

Upandaji 
Zipo aina mbili za upandaji, 
  1. kupanda mbegu moja kwa moja na
  2. kupanda mbegu katika trei na kuhamisha baada ya siku 8 hadi 10.
Njia ya kupanda mbegu moja kwa moja ni rahisi lakini ile ya kupanda katika trei ni bora zaidi kwani shamba hujaa vizuri katika nafasi na hukua haraka na kuzaa mavuno mengi. Pima mashimo ya kupandia katika umbali wa sentimita 20 hadi 25 kutoka shina hadi shina mstari mmoja kwa tuta na sentimita 40 katika mfumo wa zig-zag pande zote mbili za tuta na kupanda. Mbolea kianzio iwekwe katika kila shimo na kupanda endapo miche kutoka katika trei itatumika Hakikisha shamba lina unyevu wa kutosha kabla ya kupanda

Palizi 
Palilia shamba mara kwa mara ili kuhakikisha shamba halina magugu Magugu hudhibitiwa kwa palizi ya jembe, kung’oa kwa mkono ama matumizi ya viuagugu. Njia nyingine ni matumizi ya plastiki maalum kuzuia magugu yaani ‘plastic mulch’

Mbolea 
Tumia mbolea ya DAP wakati wa kupanda na kisha tumia NPK yenye uwiano mmoja kama, 18:18:18, 17:17:17 ama 16:16:16 baada ya wiki tatu toka Usegekaji. Tumia nguzo za unene wa inchi 2 na kamba ili kuinua mimea na matunda yasiguse ardhi na kuoza

Uchavushaji
Hii ni muhimu sana kuzingatiwa kwani tango huchavushwa kwa wadudu na si upepo. Bila wadudu kama nyuki uzalishaji huathrika sana. Ni muhimu kupanda mazao kama alizeti na maua mbali mbali yanayopendwa na wadudu wachavushaji ili kuhakikisha uwepo wa wadudu hao shambani. Aidha inapo-lazimu ni vema kuweka mizinga kadhaa ya nyuki katika shamba la tango

Matumizi ya viuatilifu Katika udhibiti wa wadudu na magonjwa matumizi ya viuatilifu yafanyike kwa maelekezo ya wataalam kubaini tatizo na kiuatilifu hitajika na namna ya matumizi yake

Mavuno 
Mavuno huanza baada ya siku 40 hadi 45 kutegemea na aina pamoja na hali ya hewa.

Comments

Popular posts from this blog

Kanuni za Ufugaji Bora wa Mbuzi na Kondoo

Utangulizi Mbuzi na kondoo wanaweza kufugwa kwa gharama nafuu na kuishi katika mazingira magumu kama ya maradhi na ukame ikilinganishwa na ng’ombe. Kutokana na umbile lao dogo wanaweza kufugwa katika eneo dogo na pia wanaweza kuhudumiwa na familia yenye nguvukazi na kipato kidogo. Uzao wa muda mfupi unamwezesha mfugaji kupata mbuzi/kondoo wengi kwa kipindi kifupi. Wanyama hao hufugwa kwa ajili ya nyama, maziwa, ngozi, sufu na mazao mengine kwa matumizi ya familia na kuongeza kipato.  Kanuni za kuzingatia Ufugaji bora wa mbuzi na kondoo uzingatie kanuni zifuatazo:- Wafugwe kwenye banda au zizi bora, Wachaguliwe kutokana na sifa za koo/aina na lengo la uzalishaji (nyama, maziwa au sufu), Wapatiwe lishe sahihi kulingana na umri na mahitaji ya mwili, Kuzingatia mbinu za kudhibiti magonjwa kama inavyoshauriwa na mtaalam wa mifugo, Kuweka na kutunza kumbukumbu sahihi za uzalishaji; na  Kuzalisha nyama, maziwa au sufu yenye ubora unaokidhi mahitaji ya soko Zizi au Banda la Mbuzi/Kond...

Kilimo Bora cha Alizeti - Uzalishaji, Uangalizi, Uvunaji na Uhifadhi

Utangulizi Alizeti hulimwa kwa wingi katika mikoa ya Shinyanga, Singida, Dodoma, Iringa, Tabora, Morogoro, Ruvuma, Mbeya, Arusha, Manyara, na RukwaZao hili hulimwa kwa ajili ya chakula na biashara. Mambo muhimu ya kuzingatia wakati wa uzalishaji Kuchagua aina bora ya mbegu Chagua aina bora ya mbegu inayovumilia magonjwa, wadudu, inayotoa mazao mengi na kiwango kikubwa cha mafuta. Vilevile chagua aina ya mbegu ambayo hukomaa kwa wakati mmoja ili kurahisisha uvunaji. Kuweka mbolea Rutubisha udongo kwa kutumia mbolea za mboji na samadi ili kupata mazao mengi na bora. Kudhibiti wadudu na magonjwa Alizeti hushambuliwa na magonjwa ya majani, mizizi na masuke ambayo husababisha upungufu wa mavunoHivyo ni muhimu kuyadhibiti ili kupata mavuno mengi na boraPia ndege hupunguza mavuno kwa kiasi cha asilimia 50 au zaidiNjia ya kudhibiti ndege ni kwa kuwafukuza na kupanda mbegu zinazokomaa mapema. Maandalizi kabla ya kuvuna;  Ukaguzi  Kagua shamba kuona kama alizeti imekomaaAlizeti hukomaa ...

Utengenezaji wa Chakula cha Kuku wa Nyama (Bloilers)

Utangulizi Kuku wa nyama wana mahitaji yafuatayo ya viinilishe katika chakula ili wakue vizuri Viinilisha vya wanga 60-65%   Protini 30-35%   Madini 2-8% Chakula cha Vifaranga Chakula hiki hutengenezwa katika namna ya kumsaidia kifaranga aweze kumeza vizuri na hivyo hakitakiwi kuwa katika punje punje. Hata kama utanunua pumba, ni vema kuzipitisha kwenye mashine ili ziwe laini zaidi.  Mahitaji (kgs)  Unga wa dona wa nafaka kama mahindi au mtama 40  Pumba za mtama au mahindi au uwele 27  Mashudu ya alizeti au ufuta, au pamba au karanga n.k. 20  Unga wa mifupa au chokaa ya kuku (DCP) 2.25  Dagaa au mabaki ya samaki (sangara fish meal) 10  Chumvi ya jikoni 0.5  Virutubisho (Broiler premix) 0.25  Jumla utapata 100Kg. Chakula cha kukuzia – growers mash Mahitaji (Kg) Mahindi yaliyobarazwa au mtama au uwele 25   Pumba za mtama au mahindi au uwele 44   Mashudu ya alizeti au ufuta, au pamba au karanga n.k. 17   Unga wa mifupa a...