Kilimo cha miti ni uwekezaji wa muda wa kati na mrefu (mid & long term investments). Ila kwa kawaida jamii nyingi hasa za kiafrika huwa hazivutiwi na uwekezaji wa muda mrefu. Hata hivyo kama una mpango wa kuwa imara kiuchumi inashauriwaau yakupasa kufikiria na kujifunza aina za uwekezaji wa muda mrefu. Miti hutumika kwa matumizi mengi mfano mbao, nguzo za umeme na kujengea, mapambo, kuni na mkaa, kuzalisha matunda, mitishamba na madawa, utengenezeaji wa karatasi n.k.
Mchanganuo
Ekari moja ya shamba unaweza kupanda miti mia sita (500) mpaka mia saba (700). Gharama za kununua mashamba au maeneo ya kupandia miti hutegemea na eneo. Kwa sehemu nyingi za vijijini maeneo kwa ekari moja hayazidi laki 5.
Miche ya kununua mfano Mitiki huuzwa kuanzia elfu moja (1000) kwa mche mmoja
Gharama ya kununua miche = 1000 * 600 = 600,000
Pia unaweza kuokoa gharama za kununua miche kwa kuioteshe mwenyewe ktk vitalu na kuiamishia shambani baada ya kustawi vizuri na kuwa imara.
Mf. Mbegu za Mitiki huuzwa 12,500 tu kwa Kilogram moja (Kg1)
Kg1 inaweza kutoa zaidi ya miche mia tisa (900) ambayo unaweza kuipanda katika eneo la ekari moja na nusu.
Faida
- Ikiwa umefanikiwa kupanda miche 600 na bei ya kuuza mti mmoja ni elfu hamsini (bei ya mfano) = 600 * 50,000 = 30,000,000
- Shamba la Miti pia ni rasilimali au hazina inayoweza kukufanya upate mkopa ktk taasisi za fedha na kufanya mambo mengine ya msingi kama kutakuwa na ulazima wa kufanya hivyo. Hii iamaanisha unaweza kuazima fedha za kukuwezesha kufanya uwekezaji wa muda mfupi
- Kutunza mazingira
Gharama Utakazoingia
- Kutafuta eneo au shamba - Bei hutegemea na eneo
- Kutunza shamba kwa mwaka mmoja- Unaweza kuwalipa vibarua laki na nusu au laki mbili, gharama hii mara nyingi utaingia miaka ya mwanzo. Pia miti ikishafika shambani haihitaji matunzo mengi kama mazao mengine
"He who plants a tree, plants a hope." - Lucy Larcom
"The best time to plant a tree is twenty years ago. The second best time is now.” - Chinese Proverb
"The secret of getting ahead is getting started. " - Mark Twain
Umebwabwaja weee mwisho was siku tumeona gharama tu faida hatujaona
ReplyDeleteMbona naona faida hapo kaandika
Delete