Skip to main content

Kilimo cha Miti ya Mbao - Uwekezaji wa Muda wa Kati na Mrefu


Utangulizi
Kilimo cha miti ni uwekezaji wa muda wa kati na mrefu (mid & long term investments). Ila kwa kawaida jamii nyingi hasa za kiafrika huwa hazivutiwi na uwekezaji wa muda mrefu. Hata hivyo kama una mpango wa kuwa imara kiuchumi inashauriwaau yakupasa kufikiria na kujifunza aina za uwekezaji wa muda mrefu. Miti hutumika kwa matumizi mengi mfano mbao, nguzo za umeme na kujengea, mapambo, kuni na mkaa, kuzalisha matunda, mitishamba na madawa,  utengenezeaji wa karatasi n.k. 

Mchanganuo
Ekari moja ya shamba unaweza kupanda miti mia sita (500) mpaka mia saba (700). Gharama za kununua mashamba au maeneo ya kupandia miti hutegemea na eneo. Kwa  sehemu nyingi za vijijini maeneo kwa ekari moja hayazidi laki 5. 

Miche ya kununua mfano Mitiki huuzwa kuanzia elfu moja (1000) kwa mche mmoja
Gharama ya kununua miche = 1000 * 600 = 600,000 

Pia unaweza kuokoa gharama za kununua miche kwa kuioteshe mwenyewe ktk vitalu na kuiamishia shambani baada ya kustawi vizuri na kuwa imara. 
Mf. Mbegu za Mitiki huuzwa 12,500 tu kwa Kilogram moja (Kg1)
Kg1 inaweza kutoa zaidi ya miche mia tisa (900) ambayo unaweza kuipanda katika eneo la ekari moja na nusu.

Faida
  • Ikiwa umefanikiwa kupanda miche 600 na bei ya kuuza mti mmoja ni elfu hamsini (bei ya mfano) = 600 * 50,000 = 30,000,000
  • Shamba la Miti pia ni rasilimali au hazina inayoweza kukufanya upate mkopa ktk taasisi za fedha na kufanya mambo mengine ya msingi kama kutakuwa na ulazima wa kufanya hivyo. Hii iamaanisha unaweza kuazima fedha za kukuwezesha kufanya uwekezaji wa muda mfupi
  • Kutunza mazingira
Gharama Utakazoingia
  • Kutafuta eneo au shamba - Bei hutegemea na eneo
  • Kutunza shamba kwa mwaka mmoja- Unaweza kuwalipa vibarua laki na nusu au laki mbili, gharama hii mara nyingi utaingia miaka ya mwanzo. Pia miti ikishafika shambani haihitaji matunzo mengi kama mazao mengine
"He who plants a tree, plants a hope." - Lucy Larcom

"The best time to plant a tree is twenty years ago. The second best time is now.”  - Chinese Proverb

"The secret of getting ahead is getting started. " - Mark Twain

Comments

  1. Umebwabwaja weee mwisho was siku tumeona gharama tu faida hatujaona

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

Kanuni za Ufugaji Bora wa Mbuzi na Kondoo

Utangulizi Mbuzi na kondoo wanaweza kufugwa kwa gharama nafuu na kuishi katika mazingira magumu kama ya maradhi na ukame ikilinganishwa na ng’ombe. Kutokana na umbile lao dogo wanaweza kufugwa katika eneo dogo na pia wanaweza kuhudumiwa na familia yenye nguvukazi na kipato kidogo. Uzao wa muda mfupi unamwezesha mfugaji kupata mbuzi/kondoo wengi kwa kipindi kifupi. Wanyama hao hufugwa kwa ajili ya nyama, maziwa, ngozi, sufu na mazao mengine kwa matumizi ya familia na kuongeza kipato.  Kanuni za kuzingatia Ufugaji bora wa mbuzi na kondoo uzingatie kanuni zifuatazo:- Wafugwe kwenye banda au zizi bora, Wachaguliwe kutokana na sifa za koo/aina na lengo la uzalishaji (nyama, maziwa au sufu), Wapatiwe lishe sahihi kulingana na umri na mahitaji ya mwili, Kuzingatia mbinu za kudhibiti magonjwa kama inavyoshauriwa na mtaalam wa mifugo, Kuweka na kutunza kumbukumbu sahihi za uzalishaji; na  Kuzalisha nyama, maziwa au sufu yenye ubora unaokidhi mahitaji ya soko Zizi au Banda la Mbuzi/Kond...

Kilimo Bora cha Alizeti - Uzalishaji, Uangalizi, Uvunaji na Uhifadhi

Utangulizi Alizeti hulimwa kwa wingi katika mikoa ya Shinyanga, Singida, Dodoma, Iringa, Tabora, Morogoro, Ruvuma, Mbeya, Arusha, Manyara, na RukwaZao hili hulimwa kwa ajili ya chakula na biashara. Mambo muhimu ya kuzingatia wakati wa uzalishaji Kuchagua aina bora ya mbegu Chagua aina bora ya mbegu inayovumilia magonjwa, wadudu, inayotoa mazao mengi na kiwango kikubwa cha mafuta. Vilevile chagua aina ya mbegu ambayo hukomaa kwa wakati mmoja ili kurahisisha uvunaji. Kuweka mbolea Rutubisha udongo kwa kutumia mbolea za mboji na samadi ili kupata mazao mengi na bora. Kudhibiti wadudu na magonjwa Alizeti hushambuliwa na magonjwa ya majani, mizizi na masuke ambayo husababisha upungufu wa mavunoHivyo ni muhimu kuyadhibiti ili kupata mavuno mengi na boraPia ndege hupunguza mavuno kwa kiasi cha asilimia 50 au zaidiNjia ya kudhibiti ndege ni kwa kuwafukuza na kupanda mbegu zinazokomaa mapema. Maandalizi kabla ya kuvuna;  Ukaguzi  Kagua shamba kuona kama alizeti imekomaaAlizeti hukomaa ...

Utengenezaji wa Chakula cha Kuku wa Nyama (Bloilers)

Utangulizi Kuku wa nyama wana mahitaji yafuatayo ya viinilishe katika chakula ili wakue vizuri Viinilisha vya wanga 60-65%   Protini 30-35%   Madini 2-8% Chakula cha Vifaranga Chakula hiki hutengenezwa katika namna ya kumsaidia kifaranga aweze kumeza vizuri na hivyo hakitakiwi kuwa katika punje punje. Hata kama utanunua pumba, ni vema kuzipitisha kwenye mashine ili ziwe laini zaidi.  Mahitaji (kgs)  Unga wa dona wa nafaka kama mahindi au mtama 40  Pumba za mtama au mahindi au uwele 27  Mashudu ya alizeti au ufuta, au pamba au karanga n.k. 20  Unga wa mifupa au chokaa ya kuku (DCP) 2.25  Dagaa au mabaki ya samaki (sangara fish meal) 10  Chumvi ya jikoni 0.5  Virutubisho (Broiler premix) 0.25  Jumla utapata 100Kg. Chakula cha kukuzia – growers mash Mahitaji (Kg) Mahindi yaliyobarazwa au mtama au uwele 25   Pumba za mtama au mahindi au uwele 44   Mashudu ya alizeti au ufuta, au pamba au karanga n.k. 17   Unga wa mifupa a...